MCHUNGAJI MITIMINGI AZUNGUMZIA UONGO ALIOZUSHIWA.

Mchungaji kiongozi Peter Mitimingi wa huduma wa VHM
Mtumishi wa MUNGU Mchungaji Peter Mitimingi ambaye pia ni mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministry(VHM) amelielezea tukio la kuandikwa vibaya tena kimakosa na mwandishi wa habari. Mchungaji Mitimingi amesikitishwa na habari hiyo na kisho kumuombea tu neema ya wokovu mwandisho huyo.
Maelezo ya Mchungaji Peter Mitimingi ni haya.

SHETANI ANALENGO LA KUHARIBU HUDUMA NA KUPOTOSHA JAMII ILA AMESHINDWA!
Nimesikitishwa sana na huyo mwandishi aliyeandika habari zangu na kupotosha jamii. Mwandishi amechukua ujumbe wangu uliorushwa kama mwezi mmoja uliopita na kituo cha WAPO radio wenye kichwa kilichosema KUEPUKA ROHO YA KUJIHURUMIA. Ambapo nilizungumzia juu ya washirika wanaopenda kujihurumia na kutotoa sadaka kwa kusingizia madeni, ada za shule na matatizo yasiyoisha ili hali pesa za vocha wanapata, soda wanakunywa maisha yao yanaendelea vema ila tu inapofika wakati wa sadaka wao ndio wanakuwa hawana kitu. Mwandishi amechukua baadhi ya maneno katika ujumbe huo na kuongezea mambo yake mwenyewe kwa manufaa ya kuboresha habari yake na kupotosha kile ambacho ujumbe huo ulilenga. Kwanza nilipoona kichwa cha habari kabla sijakisoma ndani kilinivutia na nikawa nakimbilia kucomment ghafla nikashtuka kuona jina langu. Mwandishi amefanya kama shetani anavyofanyaga kuchukua ukweli kidogo na kuongezea na maneno ambayo hayakutoka kwenye kinywa changu. Kuna njia nyingi za kuuza gazeti lakini sio kwa njia ya kunichafua na kuniwekea maneno mdomoni mwangu maneno ambayo siku yasema. Namuombea neema ya Mungu na kwamba Mungu amsaidie. Atubu na kumrudia Bwana. by MITIMINGI P


Uongo wenyewe ni huu hapa.

 

Comments