Na Emmanuel Kamalamo. |
Bwana Yesu asifiwe!
Mara nyingi watu wametafuta kumjua Mungu kupitia dini lakini wao
hawakujulikana kwa Mungu. Dini ziliwajua wao lakini Mungu hakuwajua wao.
Kwa sababu wamejaribu kwenda mbele za Mungu kwa HEKIMA, UTAJIRI na NGUVU walizonazo, na ndiposa wameshindwa kuupata wokovu (msamaha wa dhambi) kwa sababu hawataki kutubu dhambi zao na kumpokea Yesu awabadirishe maisha yao. Inawezeka wewe ni kiongozi katika ngazi yoyote katika nchi, na una HEKIMA,UTAJIRI na NGUVU fahamu kama huna YESU moyoni mwako wewe ni bure na ulivyonavyo vyote ni bure.
Neno la Mungu linasema katika Yeremia 9:23-24 "Bwana asema hivi, mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi , na kunijua , yakuwa mimi ni BWANA.."
JE UNA HEKIMA GANI?
Inawezekana una hekima ya kidunia ambayo inatokana na ELIMU YA KIDUNIA ndiyo unajisifia. Je, maandiko yanasema nini juu ya watu wenye hikima ya kidunia,wasiotaka KUOKOKA kwa sababu ya hekima zao.
1 Wakorintho 1:20-21 "...JE! MUNGU HAKUIFANYA HEKIMA YA DUNIA KUWA NI UPUMBAVU? KWA MAANA KATIKA HEKIMA YA MUNGU , DUNIA ISIPOPATA KUMJUA MUNGU KATIKA HEKIMA YAKE , ALIPENDA KUWAOKOA WAAMINIO KWA UPUUZI WA LILE NENO LINALOHUBIRIWA"
Kwa mantiki hiyo huwezi kuokolewa kwa sababu unatumia hekima yako ya kidunia. Hata kama uwe Rais, Waziri, Mbunge, Diwani mahari popote duniani kama usipotaka kumjua Mungu katika HEKIMA yake huwezi kuingia mbinguni, utapata VYEO duniani lakini mbinguni huingii,,si mimi nimesema, neno la Mungu ndilo limesema.."MUNGU ALIPENDA KUWAOKOA WAAMINIO" waaminio ni "WALIOOKOKA" kwa hiyo kama wewe hujaokoka usitegemee kuokolewa sasa maana neno hili kwako ni upuuzi.
JE! UNA JIVUNIA UTAJIRI?
Umeona utajiri wa PESA kwako ni muhimu sana hata kuona Mungu hawezi kukusaidia. Unasema"NIOMBE NINI MIMI KWA MUNGU" Maandiko yanasema nini juu ya watu wanaotumainia utajiri? 1 Timotheo 6:17 "Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini , bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha"
Kama umeuweka UTAJIRI moyoni mwako uwe na uhakika utakapokufa itakuwa vigumu kuingia mbinguni. Yesu alisema,,"KWA MAANA NI VYEPESI NGAMIA KUPITA KWENYE TUNDU LA SINDANO KULIKO TAJIRI KUINGIA UFALME WA MUNGU" Luka 18:25.
Utakapo ya acha hayo yote UKANYENYEKEA kwa Mungu, ndipo wewe utamjua kupitia HEKIMA yake ambayo ni YESU KRISTO hekima ya Mungu( Luka 11:49) na hapo utajulikana kwa Mungu.
Na ndipo utaanza "KUJISIFU" unamjua Mungu, ndivyo maandiko yanasrma.."MJUE SANA MUNGU, ILI UWE NA AMANI; NDIVYO MEMA YATAKAVYOKUJIA" Ayubu 22:21.
Utasiifu kwa sababu Yesu Kristo ni BWANA amekuokoa. Na una uzima wa milele ndani yako.
SAA YA WOKOVU NI SASA.
MUNGU AKUBARIKI
ekamalamo@gmail.com

Comments