Scholar Mabula. Kawe Pentecostal Church. |
BWANA YESU asifiwe wapendwa.
Nawasalimu katika jina la YESU KRISTO.
Ni siku njema leo MUNGU kutupa uhai na afya njema na uzima katika maisha yetu. tuna kila sababu ya kusema asante YESU kwa maana amekuwa mwaminifu na mwema. Ninapenda kuwatia moyo wale wanaopita katika wakati mguu, wanaokatishwa tamaa na kuvunjwa moyo. Naomba waendelee kumuomba MUNGU na kumsihi BWANA ili afanye kitu kipya ndani yao kwa sababu Neno la MUNGU linasema '' BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.-Kutoka 14:14''
Kwa sababu hiyo endelea kumuomba MUNGU na ni hakika MUNGU atakupigania, simamia mstari huu kwa kuomba maombi yako, kama ni kazi kama ni hitaji, kama ni huduma na mengine yote ambayo unayahitaji yatengenezwe na BWANA.
Mbarikiwe ndugu zangu wote na nawapenda sana wote katika BWANA YESU.
Tusonge mbele kuutafuta ufalme wa MUNGU, ili alipoketi BWANA na sisi tuwepo Yohana 14:3 '' Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. ''
Ndugu, Mwamini MUNGU katika kila jambo.
Kwa maana yeye ndiye mshindi wetu na mtetezi wetu katika mambo yote.
Tangu misingi ya dunia kuumbwa MUNGU alikutambua.
Yeremia 1:5 BWANA anasema ''Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.''
kwa hiyo kila jambo unalokutana nalo BWANA analijua na analiona.
Si kila siku ni usiku kwako hata asubuhi yako inakuja.
Omba bila kukoma
( ombeni bila kukoma;-1 Wathesalonike 5:17)
wala usikate tamaa kwa sababu MUNGU anataka utamke kile unachokihitaji ili akupe.
Yohana 14:13-14 '' Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana.Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. ''
na wakati usiotegemea MUNGU atajibu kwa sababu yeye ni mwaminifu sio kama wanadamu.
Hakikisha imani yako inategemea kwamba ipo siku nitapokea kutoka kwa BWANA YESU.
Amtegemeaye BWANA amebarikiwa. Biblia inasema ''Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.-Yeremia 17:7-8''
Mpendwa, nina kila sababu ya kukusihi umtegemee MUNGU kwa sababu mimi binafsi nimemuona MUNGU katika maisha yangu, nilimtegemea na akanijibu na hata sasa namtegemea na katika mambo mengi nimemuona akinitendea..
MUNGU akubariki sana.
Ni mimi rafiki yako.
Scholar Mabula.
Maisha ya ushindi Ministry.
Mimi Scholar nikiwa na mme wangu Peter Mabula. |
Comments