NI KWA KITAMBO TU!

Na Frank Philip Seth.

"Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa? Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli, Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake; Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu, Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha" (Ayubu 7:1-3).
Nimejifunza jambo hili. Kwa kila mwanadamu chini ya jua, bila kujali cheo, umaarufu, umri na mali zake, kuna masiku ya kuchokesha sana, nayo honekana marefu na mazito, lakini hupita na maumivu yake kusahulika kabisa.

Hakuna mahali pagumu kama pa kumalizia mbio, pale ambapo mtu huhesabiwa ushindi au kushindwa. Bila shaka hatua chache za mwisho huwa nzito na karibu huonekana mbali. Jipe moyo mkuu, ni kwa kitambo tu, usizimie moyo. Lipo jeshi kubwa la malaika wanachungulia unavyopigana, naam, BWANA anaona shida yako na haupo pekeyako. 

Pale unaposikia uzito na kukata tamaa, jiambie mwenyewe, "ni kwa kitambo tu"! na ujitie nguvu na kusonga mbele, uko karibu sana na ushindi wako. Jua kwamba hakuna aliyefika juu bila kupanda, ukisikia unapanda mahali palipoinuka, jua unaelekea juu. Ni kwa kitambo tu utafika kileleni, siku za kuburudika zipo zinakusuburi, ila imekupasa KUSHINDA hapo ulipo.
Frank Philip Seth.

Comments