NYOKA WA SHABA TAYARI AMEINULIWA MTAZAME

Na Geoffrey Mwanza, Mombasa Kenya.
(Hesabu 21:4-9 "Waisraeli walifunga safari kutoka mlima Hori wakapitia njia inayoelekea bahari ya Shamu ili waizunguke nchi ya Edomu....''

Wakiwa njiani wakaanza kumnung'unikia MUNGU na pia Musa wakisema kwa nini mmetutoa Misri tuje kufia humu jangwani? Humu hamna chakula wala maji,nasi tumechoshwa na chakula hiki duni....

MUNGU akapeleka nyoka wenye sumu miongoni mwa watu,wakawauma hata watu wengi wakafa....wakatambua baadaye kuwa walikuwaa wametenda dhambi mbele ya MUNGU na Musa pia,wakamwendea Musa wakimtaka awaombee.Musa akawaombea na Mungu akamwambia"tengeneza nyoka wa shaba,umtundike juu ya mlingoti.Mtu yeyote atakayeumwa na nyoka akimtazama nyoka huyo wa shaba atapona.Basi Musa akatengeneza nyoka wa shaba akamtundika juu ya mlingoti.Kila mtu aliyeumwa na nyoka mwenye sumu akimtazama huyo nyoka wa shaba,mtu huyo ALIPONA.

"Leo Kristo Yesu ndiye nyoka wa shaba na ameinuliwa ili unapomkubali akusamehe dhambi na uanze maisha ya uadilifu utapona magonjwa yako,utapata ndoa,utapata kazi,ulevi na usherati utaisha na upate maisha mazuri.YESU KRISTO anasema (Mathayo 11:28)"Njooni kwangu enyi msumbukao na wenye kulemewa na mizigo mizito nami nitawapumzisha".

Usidanganywe na mtu,baraka za Yehova haziwezi kukujia ukiwa bado dhambini.Hata waisraeli walipotambua shida yao ilitokana na uovu wa uasi wao,walimlilia MUNGU na Musa na baada ya kutubu walipona.MUNGU wetu Yehova amejawa na rehema,atakusamehe na kukufanya chombo kipya.Ni vizuri pia kutubu dhambi,kuoka na kuacha dhambi maana hakuna ajuaye kifo kitamjia siku gani,wakati gani na utakuwa wapi(Mhubiri 3:1"...Kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa.....". 
Tubu leo na utapona dadangu.
Mkubali Yesu leo,upokee baraka za kiungu. 

TUOMBE PAMOJA 
"BWANA YESU NATUBU MBELE ZAKO,NIMEKUWA MTENDA DHAMBI,LEO NIMEACHA DHAMBI NA NIMEOKOKA KWA JINA LA YESU KRISTO NIMEOSHWA DHAMBI NA NIMETAKASIKA,AMEN".

MUNGU ANAKUPENDA SANA- 
Utatupata kupitia "THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES -Rununu 0724 656 653.

Comments