Na Nickson Mabena |
Bwana Yesu asifiwe, Karibu tujifunze pamoja...
''Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.''
Yesu alizitaja Sababu kuu Mbili, za Watu Kupotea!, ambazo ni:-
1.Kutoyajua Maandiko
2.Kutokujua Uweza wa Mungu.
Maandiko(NENO), ndio Mwongozo wa Maisha ya Mwanadamu yeyote yule...
Sasa, kuna watu wengi sana Katika Dunia ya Leo Wamepotea
(Wapo Nje ya Kusudi la Mungu), Kwa sababu ya Kutoyajua Maandiko...
Binafsi Huwa Inaniuma sana, ninapowaona watu Wanahangaika, bila kupaata Msaada wowote wakati Yesu Mtenda Miujiza yupo!, Watu bado hawajajua Uweza Wa Mungu...
Nimekutana na Watu Wengi, Wakiwa kwenye vifungo mbalimbali, Wengine ni vya Miaka Mingi sana...
Yesu anao Uweza, wa Kurudisha Vitu vyako vilivyopotea...
Anao Uwezo wa Kukufungua pale Ulipofungwa...
Bado anaweza Kukuponya Ugonjwa Uliokusumbua Kwa Mda Mrefu...
Bado anaweza Kufungua Tumbo lako la Uzazi, nawe Ukakumbatia Mwana.
Mimi ni Mwalimu wa Mathematics kwa Shule za Sekondari, lakini bado nasoma Chuo. Siku moja nikiwa field tuliletewa Mwanafunzi aliyekua anasumbuliwa na Nguvu za giza, kwa kuwa tupo waalimu tuliookoka katika hiyo shule, tukaamua kumfanyia maombi, siku ya kwanza alifunguliwa lakini tatizo likamrudia tena, akaletwa tena tukamwombea tena, akafunguliwa na tatizo likamrudia tena, ikabidi nioongee naye kwa kirefu, na nikamshauri AOKOKE ili tatizo lisirudi tena…
Yale Mapepo yalikua yanadai yametumwa na moja ya ndugu zake wa karibu wa huyo mwanafunzi, ili yamtoe kafara kwani hawataki asome, pia huyo ndugu yake alikua anataka afanikiwe kwenye mambo yake kwa njia hiyo.
Lakini cha ajabu ni kwamba huyo mwanafunzi alikataa KUOKOKA, akaniambia hadi akamuulize Mama yake nyumbani, siku hiyo naongea naye ilikua siku ya ijumaa, na hayo mapepo yalidai jumapili ndiyo siku ya kumtoa kafara!, Alipoendelea kubisha, nikamuombea tu ili asife lakini nikijua hali yake itakuja kuwa mbaya zaidi….
Yule Mwanafunzi, hadi naandika ujumbe huu hali yake ni mbaya sana, na nimepata taarifa bado mama yake amebaki na Msimamo wake hataki mwanae AOKOKE, yaani yupo tayari Mwanae aendelee kuteseka, kuliko Kumpa Yesu Maisha yake!!
Najua, hakuna Mtu anayependa ateseke, au Ndugu yake ateseke…….
UNAJUA KWA NINI WANAENDELEA KUTESEKA!?, ni kwa sababu hawayajui MAANDIKO, wala UWEZA wa Mungu, kwani Yesu yupo tayari kufanya Jambo jipya, lakini wao hawapo tayari!!.
Ingawa kuna wanafunzi wengine wengi waliokua wamefungwa na nguvu za giza, wamefunguliwa na hadi sasa wanaendelea vizuri na Masomo yao!
Kwa kutoyajua Maandiko, kuna baadhi ya vijiji nilivyowahi kutembelea Mkoani Kilimanjaro, watu wangi wanatumikishwa na POMBE!, Watu wamechakazwa na Pombe, vijana wadogo wamekua kama wazee kisa POMBE, na kwa kuwa hawayajui Maandiko bado wanaitetea POMBE…
Mama Mmoja mfanyabiashara wa Pombe flani ya kienyeji nimewahi kumuuliza, kwa nini unafanya Biashara hii ya pombe!, kwani hujui kwamba Pombe ni Dhambi!?, akanijibu akisema, “Pombe siyo dhambi, hata Yesu mwenyewe aligeza maji yakawa pombe”.
Nikajaribu kumfundisha hapo kwa kutumia Maandiko mengi sana, lakini bado Moyo wake ukawa mgumu!
Sehemu nyingine, nilikaribishwa, Mama mmoja aliniambia, “Mwalimu, karibu MBEGE”, nikamwambia Mimi ni Mtumishi wa Mungu sinywi MBEGE, akaniuliza “Kwani mimi ni mtumishi wa shetani?, Yesu mwenyewe Mbona alitengeneza POMBE”.
Ndipo nilipozidi kuyaelewa Maneno ya Yesu aliposema “…..Mwapotea kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu”.
Wapo vijana wengi sana, wanatumikishwa kwenye UZINZI na UASHERATI, na wameshindwa kujitoa kwenye eneo hilo!, na Pengine wewe Msomaji wangu ni mmoja wao…!!.
Je! Umeshawahi kujiuliza, kwa nini Ndoa zisizo halali zimeongezeka!?, Je! Unajua kwa nini wanawake wengi wanapata Mimba wanazoziita za Bahati Mbaya!?
Ndugu yangu Mungu ameruhusu uusome Ujumbe huu, ili ufanye uamuzi sahihi wa kurejea kwenye Mstari wake…. Tambua ya kwamba, Mungu hapendi hata mmoja apotee, bali wote waifikilie toba.
Yesu anaweza kukusaidia pale ulipokwama, Yesu anaweza kukutendea Jambo jipya, Yesu anaweza kukuvusha. Jambo la Msingi ni kumwamini Yeye, na Imani Chanzo chake ni kusikia, na Kusikia huja kwa NENO la Kristo!.
By Nickson Mabena
<<<<<<<<<<<<<<<Mungu, akubariki sana!!.>>>>>>>>>>
Comments