TAMBUA NYAKATI NA MAJIRA


Na mtu wa MUNGU, Nabii Samson Mboya,Kwa Maombi na maombi piga +255756 809 209
  • UTANGULIZI.TAMBUA NYAKATI NA MAJIRA 
Utangulizi 
Hatima ya mwanadamu imefungwa katika nyakati na Majira usipotambuwa wakati na majira ya Mungu juu ya Maisha yako hilo ni tatizo
Tunapozungumza kwa habari ya nyakati na majira tuna maana hii;


  • Majira: Ni vipindi mbalimbali ndani ya wakati ulioamriwa; mfano masika, kipupwe, kiangazi, n.k



  • Nyakati: Ni vipindi kulingana na matukio ya makusudi; mfano asubuhi, jioni, nyakati za mwisho, nyakati za utandawazi, wakati wa kupanda, kuvuna, n.k
Ni muhimu sana kufanya kila jambo kwa wakati na majira yake, mfano kupanda wakati wa kupanda, kuvuna wakati wa kuvuna, n.k
Siku zote ukifanya jambo nje ya wakati wake utaonekana kituko, na matokeo yake ni kutokufanikiwa. Kila jambo huonekana la busara mbele ya wenye hekima likifanyika ndani ya wakati wake, kwa lugha nyingine, "Everything is right at right time". Maana yake ni kwamba ukifanya jambo nje ya wakati hata kama jambo hilo ni jema, litabadilika kuwa baya. Wakati una 'impact' kubwa sana katika jambo lolote. Tazama formula ifuatayo;


  • Luka 19:42 42  akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
  • Kila jambo kuna majira yake na wakati wa kila kusudi,

 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu” (Muhubiri 3:1)
9,000,000 +Nyakati isiyo sahihi = 0


  •  Kitu sahihi +Muda usiyo sahihi = sifuri
Kitu sahihi +wakati sahihi= na Mazidisho yaani mafanikio
Kwa hiyo unaweza kuona ni jinsi gani wakati unavyoweza kuathiri mamboyako  hii ndiyo Kwa hiyo jambo ni jema sana likifanywa ndani ya muda wake. Kwa mfano, tendo lile lile linalofanywa na wanandoa likifanywa na watu ambao si wanandoa linakuwa si sahihi.


  • Wala tendo halijabadilika, ni lile lile lakini kwa nini likifanywa na wanandoa ni sahihi na likifanywa na watu ambao si wanandoa sio sahihi? Tena limepewa na jina jingine kabisa, uzinzi; na ukifanya jehanamu unakwenda kwa miguu yote miwili. Tatizo hapa ni wakati!


Mhubiri 3:1-3

Hapa mwandishi anajaribu kutueleza kuwa kila jambo lina wakati na majira yake, tena kila kusudi. Anasisitiza kwa kuonesha mifano kadha wa kadha, wakati wa kuzaliwa, wakati wa kufa, wakati wa kupanda, wakati wa kuvuna n.k.

2Nyakati 1:7-10

Hapa tunamuona Sulemani anafanywa mfalme, akaona hekima na maarifa aliyo nayo hayamtoshi, yalikuwa yanamtosha wakati akiwa kijana, raia wa kawaida; ila wakati huu ni mfalme, hivyo akitazama kazi aliyonayo na kiwango cha hekima na maarifa aliyonayo, haoni uwiano. Mungu anamtokea na kumuuliza, "...omba lolote utakalo nikupe..." Mara Sulemani akakumbuka kiwango chake cha hekima na maarifa wakati huo, akamwambia Mungu, "...nipe sasa hekima na maarifa, nijue kuingia na kutoka mbele ya watu hawa..." Nataka uone jambo hili mahali hapa, si kwamba Sulemani hakuwa na hekima ama maarifa; alikuwa nayo, ila ya kujiongoza mwenyewe. Sasa wakati huu amekuwa mfalme, hivyo anahitaji hekima na maarifa ya kuwaongoza watu wengine.

Daniel 9:2,3

"...mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalitambua hesabu ya miaka, ambayo neno la Mungu lilimjia Yeremia nabii, ya kutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani miaka sabini."
Daniel anaposoma kitabu cha nabii Yeremia anatambua kuwa, wakati waliopo hawapaswi kuwepo Babeli, ila wanatakiwa kuwa wameondoka. Kilichokuwa kimeendelea kuwaweka Babeli ni kutokujua nyakati na majira ambayo wanatakiwa kuondoka Babeli.

Kwa hiyo baada ya Daniel kutambua kuwa walipaswa kukaa Babeli kwa miaka sabini ndipo akamlilia Mungu kumweleza kwamba wanatakiwa waondoke hapo. Kumbe kilichokuwa kinaendelea kuwaweka Babeli ni kutokujua wakati.


1 Nyakati 12:32

"Na wa wana wa Isakari , watu wenye akili za kujua NYAKATI, kuyajua yawapasayo Israel wayatende; ... na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao"
Mungu alijua umuhimu wa watu wa namna hii,watu wanaojua nyakati, kujua wakati gani Israel wanapaswa kufanya nini. Tena Biblia inasema, kwa sababu tu ya wao kujua nyakati, "...ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao". Kwa hiyo ukijua wakati gani unapaswa kufanya nini, utakuwa na ujasiri wa kufanya mambo yako na siku zote utakuwa mtu wa kufanikiwa. Hii ni kwa sababu kila jambo chini ya jua hufanyika ndani ya wakati ulioamriwa, kulingana na mazingira husika. Na ndio maana leo ukikutana na mtu na kumuuliza kwa nini unafanya unachokifanya atakwambia 'nakwenda na wakati'. Ukijua ni wakati gani kitu gani kitatokea utajiandaa kukabiliana nacho.

Mathayo 26:36-46

Yesu alipojua ama alipotambua wakati wa kusulubiwa, alijiandaa kwa kufanya maombi mazito ya kuomba ujasiri wa kukabiliana na hali halisi iliyopo. Kama unafikiri natania, kasome mwenyewe utaona kuna wakati alisema "... kama ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke..." Kwa hiyo maombi aliyokuwa anayafanya, kwa kutambua wakati alionao yalikuwa na umuhimu mkubwa sana, na ni kwa maombi hayo ndipo malaika alishuka akamtia nguvu. Sasa fikiri kama asingejua kuwa huo ndio ulikuwa wakati wa kusulubiwa, halafu asiende kuomba; unafikiri huyo malaika wa kumtia nguvu ama moyo angempata wapi! Ukijua wakati gani unapaswa kufanya nini, utakaa katika eneo husika na utajiandaa kukabiliana na jambo hilo.
Nimekupa dondoo hizo chache za Biblia ili tu uone ni jinsi gani ni muhimu kujua na kutambua nyakati na majira unayoishi.


 
Nikueleze tu kwamba mafanikio yako ya kiroho na kimwili huendana sana na wakati. Watu hatufanikiwi kwa sababu tu hatujui ni zama gani tunazoishi sasa na tunapaswa kufanya nini. Kwa mfano, kipindi Yesu yuko duniani, yaani karne ya kwanza AD, ilikuwa mtu akiwa na gari linalovutwa na punda, ndiyo alikuwa anaitwa amefanikiwa, ama kwa maneno mengine yeye ni tajiri! Lakini mtu huyo huyo kwa kipindi chetu tunachoishi sasa si tajiri tena kwani mikokoteni ya kuvutwa na punda ni kwa ajili ya kukatia majani ya ng'ombe, kuchotea maji maeneo yenye ukame, kubebea samaki kwa wavuvi, kuzolea takataka kwa maeneo ya mjini, tena uswahilini,n.k. Mafanikio ni yale yale, lakini wakati! Kimsingi kabisa, kinachofanyika leo si kitakachofanyika kesho.
ili zikusaidie kufikiri na kutenda ki – muda.  Biblia katika Mwanzo 18:14 inasema “Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume”

Kushikilia Ahadi ya Mungu,
Je umeshawahi kufikiri kwa nini ilibidi Mungu aweke wazi muda wa Sara kumzalia Ibrahimu mtoto? Mungu alitaka Ibrahimu atumie taarifa aliyopewa si tu kuifunga/kuiweka imani yake kwenye ahadi aliyopewa bali zaidi kupata alichokitarajia ndani ya muda maalum aliosema Mungu juu yao. Hivyo ni muhimu ujifunze kukishikilia kwa imani na mombi kile ambacho Mungu amekusudia kukitenda juu yako kwa nyakati husika.

Mwanzo 18:14 katika bibilia ya  kiingereza inasema  “Is anything too hard for the LORD? At the appointed time I will return to you, about this time next year, and Sarah shall have a son.” Umeona neno hili “appointed time” naam ni lazima ujue kwamba kwenye kila jambo linalopaswa kufanyika kufuatana na kusudi lako hapa duniani kuna ‘appointed time”.Unapotamkiwa neno la kinabii na Mtumishi wa Mungu  ukaambiwa  muda wa jambo kutokea ni wewe kusubiri  matokeo

Mungu si mwanadamu akasema Uongo,

Hesabu 23:19Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza? Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua.
Kumbuka appointed time yako katika mambo yako mbalimbali ni tofauti kabisa na ile ya watu wengine. Hivyo kadri unavyokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu nyakati na kushirikiana nazo ndivyo unavyoweka mazingira ya kuhakikisha appointed time yako inakuwa halisi kwa kuzaa kilichotarajiwa.  Hivyo ni muhimu sana si tu uwe na ufahamu wa kutosha wa nyakati bali zaidi sana ujue namna ya kushirikiana na hizo nyakati maishani mwako.

Tujifunze kutoka kwa Lea mkewe Yakobo

Katika Mwanzo 29:31 Biblia inasema ‘Lea akapata mimba, akazaa mwana, akampa jina lake Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa BWANA ameona teso langu; sasa Mungu wangu atanipenda’

Wewe kama ni msomaji wa Biblia utagundua kwamba haikuwa mapenzi ya Yakobo kumuoa Lea bali Raheli. Na kwa sababu hiyo upendo wa Yakobo kwa Lea haukuwa mkubwa sana (Mwanzo 29:30). Maandiko yanasema BWANA Mwenyewe akaona kwamba Lea hakupendwa ndipo akalifungua tumbo la Lea akaanza kuzaa watoto.
Naam Lea alijua na alimaanisha kwamba hata kama mume wangu alikuwa na sababu ya kutonipenda, kitendo cha Mungu kufungua tumbo langu na kuzaliwa kwa Reubeni ni appointed time ya kwangu ambayo inazaa upendo wa mume wangu kwangu. Naam jambo la msingi ilikuwa si kuzaliwa Reubeni bali ilikuwa ni kile ambacho Ruebeni anakileta yaani kuzaliwa kwa upendo kwenye ndoa ya Lea na Yakobo.

Tujifunze kutoka kwa wana wa Israeli

Hesabu 9:22 – 23 inasema ‘Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka wana wa Israeli walikaa katika kambi yao wasisafiri’. Bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; wakayalinda malinzi ya BWANA, kwa mkono wa Musa’. Naam andiko hili linatuonyesha kwamba BWANA ndiye aliyekuwa akiamua muda wa kila jambo juu ya wana wa Israeli naam muda wa kusafiri na muda wa kutulia maskani kwa ishara ya wingu. Ndiyo kwa kila muda kulikuwa kuna vitu ambavyo Mungu alikuwa anavifanya kwa watu wake.

Katika Zaburi 32:8 Biblia inasema “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu, likikutazama’. Maandiko haya mawili yanatupa kujua kwamba ili nyakati zilizoamriwa na Mungu juu yako ziweze kuzaa/kuachilia/kufunua kile kilichofichwa/kilichobebwa/kilichohifadhiwa ndani yake sharti mwanadamu ajifunze kumtumia Roho Mtakatifu kama kiongozi wa maisha yake hapa duniani. 

Tujifunze kutoka kwenye ufuno wa Yohana kuhusu Ibilisi

Biblia katika Ufunuo waYohana 12:13 inasema ‘… Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye gadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu’.  Tafakari hivi, endapo Ibilisi anajua kwamba ana muda mchache tu, uwe na uhakika amejipanga kuutumia vizuri ili kuhakikisha malengo yake yanatimizwa kwa asilimia mia moja ndani ya muda mchache uliosalia.
Naam ili malengo yake yasifanikiwe juu yako, kwenye familia yako, kanisa lako, nchi yako nk. ni muhimu sana wana wa Mungu si tu wakajua nini mapenzi ya Mungu wao kwa nyakati alizoweka juu yao bali zaidi sana wadumu katika kuyatenda. Naam jambo hili limesisitizwa pia na Mzee wetu Petro aliposema ‘Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani”         (1Petro 4:2)

Tujifunze kupitia Yezebeli

Ufunuo 2: 21“Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake’. Je umeona jambo hili, hapa Yesu alikuwa akisema na Kanisa la Thiatira kuhusu kujiepusha na Yezebeli mwanamke ambaye alikuwa analiharibu kanisa hilo. Licha ya makosa yake Mungu akatoa muda wa Yezebeli kutubu wala hakutaka kutubia uovu wake. Na ni muhimu utambue kwamba muda aliopewa Yezebeli kutubu ulikuwa na kikomo.

Hata leo bado Mungu anatoa muda na fursa nyingi sana za watu wake kutubu na kutengeneza njia zao. Ile kwamba mwenzi wako, watoto wako, ndugu zako wanaendelea kuishi hata kama ni watenda maovu haina maana kwamba Mungu anafurahia uovu wao au haoni. Fahamu kwamba kimya chake ni muda ambao anautoa kwa wanadamu kutubu na kumrudia kwa kuwa yeye hafurahii kifo cha mwenye dhambi. Naam muda aliouweka juu yako, nyumba yako nk kutubu ukipita na walengwa wakakataa mabaya zaidi yatatokea kama ilivyokuwa kwa Yezebeli, miji ya Sodoma na Gomora nk.

Hivyo kwa kuwa wewe umepata ufahamu huu ni vema ukajifunza kushirikiana na muda wa kutubu ambao Mungu ameachilia juu yako, familia yako, kanisa lako, taifa lako nk, ili kwa njia ya maombi yako uiponye nyumba yako na Taifa lako pia.
Tujifunze kupitia Paulo na Timotheo

Biblia katika 2Timotheo4:2 inasema ‘Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usikokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho’. Katika maneno haya tunajifunza kwamba kumbe kwa kila jambo kuna wakati unaofaa na usiofaa. 

Jambo muhimu kwako ni kuwa tayari kuyatenda mapenzi ya Mungu kwa kila kipindi uanchopitia maishani mwako ili ndani ya vipindi husika yatimie yale yaliyokusudiwa na Mungu kutimia. Na hii ni kutokana na ukweli kwamba nyakati zimeamriwa na Mungu, kutoa ushirikiano kwa mtu ambaye anazingatia maagizo ya Mungu na sheria zake.

Naam ningeweza kuendelea kukuonyesha maandiko mengine kadhaa ndani ya Biblia lakini ninapomaliza natamani kusisitiza kuhusu kuwaombea wale waliopewa kuwa na akili za kujua nyakati zinazokuhusu katika ngazi mbalimbali. Ukirejea1Mambo ya 

Nyakati 12:32 Biblia inasema “Na wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao vilikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao”
Kutokana na andiko hili, ni dhahiri kwamba si watu wote waliopewa akili za kujua nyakati za yale yanayokuja ili kuwaongoza wengine namna ya kuyakabili. Hata hivyo uwe na uhakika kwamba kutokana na umuhimu wa jambo hili Mungu ameweka katika kila familia, kanisa, Taasisi, Taifa nk watu ambao ndani yao kuna akili za kujua nyakati zinazohusu familia, kanisa , taasisi au taifa husika ili wawasaidie wengine kujua yawapasayo kutenda kwa kila nyakati.

Hivyo ni muhimu sana ukajifunza kuwaombea watu wa namna hiyo kwenye familia yenu, kanisa, taifa nk kwa kuwa ndani yao kuna nyakati zote ambazo unapaswa/mnapaswa kuzipitia. Naam ni muhimu sana kuwaombea ili mosi wajitambue na pili wakae kwenye nafasi zao kwa kuwa ndani yao Mungu si tu ameweka akili za kujua nyakati bali zaidi namna ya kufanya katika kila nyakati zinazokuja juu yako.

Nami nakushukuru, Baba, Mungu wa wote wenye mwili, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga
Hitimisho:
Mhubiri 7:14 Isaya 44:26    

             Kwa Maombi na maombi piga +255756 809 209

Comments