TATIZO LA KULA KUCHA ZA VIDOLE VYA MIKONO! - Party 1

Na Mchungaji Peter Mitimingi.
Tatizo la kula kucha kwa kitaalam linajulikana kama "onychophagia".
• Ni tabia ya kawaida ya kuondoa msongo wa mawazo au sterss.
• Ni njia ya kujishughulisha wakati ukiwa hauna kazi ya kufanya.
• Hii inaweza vile vile kuwa ni tabia ya kujifunza kutoka kwa wanafamilia.
• Kula kucha ni moja ya tabia za kuonyesha kuwa mtu anaogopa au kuwa na wasiwasi.
• Kula kucha inajumuisha kunyonya dole gumba la mikono, kushika shika pua, kushika shika au kuvuta nywele, kung’ata meno.
• Unaweza kula kucha zako bila wewe mwenyewe kutambua kuwa unafanya hivyo.
• Unaweza ukawa umejihusisha katika kazi tofauti kabisa kama vile kusoma, kutazama televisheni, au ukawa unaongea katika simu yako na ukawa unaendelea kula kucha zako bila hata kujitambua.
• Kula kucha inajumuisha kung’ata sehemu laini za pembeni mwa kucha na hata kungata kucha yenyewe.
Wakina nani ndio huwa wanakula kucha zao?
NITAENDELEZA SOMO HILI KESHO!
Kama umepata kitu au una maswali nijulishe hapo kwenye commen

 
DONDOO NYINGINE NI HII.

 
HAKUNA UGALI UNAOPIKWA NA MAJI BARIDI!
1. Ugali ili uitwe ugali ni lazima upikwe kwa maji ya moto tena yaliyochemka vizuri.
2. Hakuna maono yanayoiva kwa kupikwa na maji baridi
3. Unataka maono makubwa usikimbie maji ya moto
4. Usipende maono yako yapikwe kwa maji ya baridi hayataiva wala kutimia.
5. Usikurupuke acha maji ya maono yako yachemke kwanza kabla ya kuweka unga wa maono.
6. Ukiweka unga wa maono kabla maji ya maono hayajachemka sawa sawa huwezi kuivisha maana maono yataharibika.
7. Nachemsha maji, nataka maji yaendelee kuchemka, siogopi maji ya moto maana hayo ndio yataivisha ugali wa maono yangu!
SEMA AMINA!

Comments