TENGENEZA MAMBO YA MOYO WAKO, HUTAKUFA, UTAISHI


BWANA YESU apewe sifa ndugu.
Karubu tujifunze neno la MUNGU.
Isaya 38:1 '' Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. '' 
-Tunamsoma Mfalme Hezekia Kwamba Aliugua Akawa Katika Hatari Ya Kufa, Neno La BWANA Likamjia Kusema "TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO MAANA UTAKUFA". 
 -Ndugu Zangu, Hezekia Wa Leo Ni Mimi Na Wewe. Neno La MUNGU Linatutaka Tutengeneze Mambo Ya Nyumba Zetu Maana Ipo Siku Tutakufa. 

Biblia Iko Rohoni Hivyo Nyumba Tunazotakiwa Kutengeneza Ni Mioyo Yetu. Mithali 4:23 '' Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. '' 
Cha kulinda ni moyo, moyo ndio nyumba ambayo inatakiwa itengenezwe maana kuna kuondoka.
Ndugu, Tengeneza Mambo Ya Nyumba Yako Maana Ipo Siku Utakufa. Nyumba ni moyo.

Hata Kama Utakufa Miaka 80 Ijayo Ndugu Tengeneza mambo Ya Nyumba Yako. Kama Kwenye Nyumba Yako Kuna Buibui(mawazo Machafu) Ziondoe, Kama Nyumbani Mwako Kuna Uchafu(dhambi) Ziondoe Ndugu. Tengeneza Mambo Ya Nyumba Yako.  
Waefeso 5:3 '' Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; ''
-Hakikisha Moyo Wako Uko Safi. MUNGU Anasema Tengeneza Mambo Ya Nyumba Yako, Ni Upendo Wa Ajabu Sana MUNGU Anauonyesha Kwa Wanadamu, Angeweza Angekaa Kimya Lakini Kwa Upendo Anakutaka Utengeneze Moyo Wako, Mpokee YESU Na Kuanza Kuishi Maisha Sahihi Ya Wokovu Utakuwa Umetengeneza Mambo Ya Nyumbani Mwako. TENGENEZA MAMBO YA MOYO WAKO, HUTAKUFA, UTAISHI. 
Matendo 3:19 '' Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; ''

- Tengeneza Maisha Yako, Hutakufa Bali Utaishi, Mkaribishe BWANA YESU Ili Atawale Maisha Yako. 
-Tengeneza Kwa YESU Mambo Ya Ujana Wako.
-Tengeneza Kwa YESU Mambo Ya Ndoa Yako.
- Tengeneza Mambo Ya Moyo Wako.
-Tengeneza kwa  Samehe Watu Wote.
- Jitenge Na Sanamu.
-Jitenge Na Masengenyo.
-Jitenge Na Dhambi.
-Jitenge Na Uchungu Mbaya.
-Jitenge Na Umbea.  
 1 Kor 6:9-11 ''  Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la BWANA YESU KRISTO, na katika ROHO wa MUNGU wetu. ''

Tengeneza Maisha Yako Kwa YESU KRISTO. 
 Usifanye Wema Wako Machoni Pa Wanadamu Ili Wakupigie Makofi Wakati Moyoni Mwako Ni Mtenda Dhambi.
- Ya Dunia Yatapita Lakini Amchaye BWANA Atadumu. Tengeneza Mambo Yako Kwa YESU KRISTO. 
-Tangaza Msimamo Wako Wa Wokovu. 
-Kataa Marafiki Wabaya Na Jitenge Na Anasa Za Dunia.
-Mkiri BWANA YESU siku zote. 
BWANA YESU anasema ''Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za BABA yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za BABA yangu aliye mbinguni. -Mathayo 10:32-33'' 
-Ndugu mkiri  BWANA YESU na hakikisha  matendo yako hayamkani BWANA YESU siku zote.

Kubali Kuwa Karibu Na MUNGU Kwa Maombi Kila Siku. Upende Wokovu Maana Ni Mtamu Kuliko Asali. Vumilia Magumu Na Katika Mambo Yote Mche BWANA YESU huku ukiongozwa na kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU.
Warumi 8:14 '' Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''

 Usiibe Wala Kudhulumu, Uzinzi Na Uasherati Usitajwe Kwako. Usiabudu Watakatifu Wala Malaika Yeyote, Kataa Kutumiwa Na Dhambi Na Ukatae Kwa Namna Yeyote Uwakala Wa shetani. BWANA YESU Yuaja Na Ni Heri Anayejitakasa Sasa.
Ufunuo 22:11-13 ''Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.   ''

 Uambie Moyo Wako "TULIA KWA BWANA YESU". 
-Utiishe Moyo Wako, Usikubali Moyo Wako Kumwacha MUNGU BABA. Moyo Una Ugonjwa Wa Kufisha Ni Nani Awezaye Kujua? 
 Yeremia 17:9-10 '' Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake. ''
 Moyo Usipotiishwa Unaweza Kuangamiza Mwili Mzima.
- Kwa Moyo Mtu Huamini Hata Kupata Uzima Wa Milele Lakini Pia Kwa Moyo Mwanadamu Hutenda Dhambi. 

Ndugu, Linda Moyo Wako Kuliko Yote Uyalindayo Maana Maamuzi Mazuri Au Mabaya Hutokea Moyoni. Nidhamu Njema Na Nidhamu Mbovu Hutokea Moyoni. shetani Akitaka Kukutumikisha Au Kukutumia Katika Malengo Yake Hukamata Moyo.  Yakobo 4:7-8 ''Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.    ''

Ndugu, Uambie Moyo Wako "TULIA KWA BWANA YESU". Wengi Leo Wanadanganywa Na Moyo Na Kujikuta Wako Kuzimu, Moyo Unawafanya Watu Wengi Kuwaza Tu Dhambi Na Sio Utakatifu. 
 ''Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; -Wakolosai 3:9''
Ndugu Utiishe Moyo Wako, Usiwaze Dhambi, Kataa Dhambi, Ikimbie Dhambi, iogope Dhambi Na Usifanye Dhambi. 
 ''Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.- Warumi 12:17 ''
Tiisha Moyo Wako Kwa Damu Ya BWANA YESU. 
BWANA YESU Anakuhaitaji Leo. Mpokee Ndugu Na Utakuwa Umepata Nafasi Ya Jina Lako Kuandikwa Mbinguni Kwenye Kitabu Cha Uzima. Kisha Anza Kuishi Maisha Ya Ushindi Dhidi Ya Dhambi.
 ''lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la MUNGU na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za MUNGU- 2 Kor 4:2''.
-Ndugu,TENGENEZA MAMBO YA MOYO WAKO, HUTAKUFA, UTAISHI. 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments