TIBA YA NDOA YAKO NII HII.

BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze habari za tiba ya ndoa.
Ndoa nyingi leo zina matatizo.
ni matatizo mengi lakini Tatizo Kubwa Ni Wanandoa Kila Mmoja Kutokukaa Kwenye Nafasi yake aliyoagizwa kibiblia.
Ndoa bila YESU ni msiba mkubwa.

 =Biblia Inaagiza Wanawake Kuwatii Waume Zao
Waefeso 5:22, Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii BWANA wetu.
-Mwanamke lazima awe mtii kwa mmewe, ni utii katika BWANA, ni utii pekee ambao hauharibu uhusiano wa mwanamke huyo na MUNGU muumbaji wake.
-Biblia imesema vizuri kabisa kwamba Mwanamke anatakiwa kumtii mmewe, ukigeuza tu yaani ukataka mwanamume amtii mkwe hapo lazima vita itokeee. nafasi ya mwanamke ni kutii mmewe na nafasi ya mwanaume nayo ipo.
Wakolosai 3:18  ''Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika BWANA.   ''
-Mwanamke kama unataka ndoa yako iwe na furaha na amani hakikisha unakuwa mtii kwa mmeo. sio kwa sababu tu hajaleta nyama unaanza kumdhalilisha mbele ya rafiki zake. unakuta mmeo anaongea na wanaume wenzake na wewe unaanza kumgombeza, ndugu hapo lazima tu vita ianze maana kama kuna jambo mwanaume analipenda ni utii. 
Mithali 11:16 '' Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima;  '' 
mwanamume kumwambia ''nakupenda'' ni jambo dogo sana kuliko kumtii huku humwambii nakupenda, nakuhakikisha lazima mtadumu sana maana utii ndio jambo la kumpa mwanaume, lakini uwe tu utii katika BWANA. Kama mawanume anataka na wewe unywe pombe kwa sababu tu yeye ni mlevi kataa maana utii wako wote kwake lazima uwe ni utii ambao haumuchukizi MUNGU hata kidogo. Sio mwanaume anataka mfanye mapenzi kinyume na maumbile na wewe unakubali, huo ni ujinga kuliko wajinga wote duniani. usikubali kumtii katika jambo ambalo ni machukizo kwa MUNGU ila kwa mengine yote hakikisha unamtii maana ni agizo la Biblia.
 Wakolosai 3:13-14 ''Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama BWANA alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.''

=Mwanamke hakikisha unakuwa muombaji.
Yeremia 31:22  '' Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.''
-Lazima umlinde mme wako kwa maombi.
-Maombi ni silaha kuu kuliko zote ambayo inaweza kukulinda na kuilinda ndoa yako. 
-Muombaji ni mlinzi wa familia.
- kama huombi shetani atapanda magugu tu katika ndoa yako na magugu hayo yakikua lazima tu ndoa yako iwe kwenye mgogoro mkubwa.
 1 Kor 16:14 ''Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.''


Hayo ni mambo makuu mawili ambayo binafsi nimeandaa hata kama kuna mengine mengi ambayo Biblia inayazungumza kama wajibu wa mwanamke.

= Wanaume Wameambiwa Wawapende Wake Zao 
Waefeso 5:25, Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama KRISTO naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

Kama nilivyosema hapo juu kwamba kila jinsia katika ndoa wapewa jukumu lao ili maisha ya ndoa yaende vizuri.
Nimesema Mwanamke ameamuriwa na neno la MUNGU amtii mmewe katika BWANA na  mwanamume ameariwa kumpenda mkewe.
Warumi 12:9 '' Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. ''
-Kazi ya mwanaume ni kumpenda mkewe.
-Mwanamke anahitaji zaidi upendo. 
-Upendo unaanza na kauli nzuri, sio kila muda wewe mbabe tu, ndugu ubabe huo utavuruga ndoa yako.
-Kama unampenda mkeo hutamsaliti.
- Kama unampenda mkeo hutampiga wala kumtukana.
Biblia imewapa agizo kubwa zaidi wanaume maana ndio viongozi wa familia.
Mwanaume anatakiwa kumpenda mkewe kama anavyojipenda mwili wake mwenyewe.  
Waefeso 5:28  ''Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.   ''
Kipimo cha kumpenda mkeo ni jinsi unavyoupenda mwili wako.
-Kama vile wewe hutaki mwili wako ubugudhiwe, vile vile usimbugudhi mkeo maana mkeo ni mwili wako.
-Kama hutaki kunyanyaswa hakikisha na wewe haumnyanyasi mkeo.
-Mkeo sio chombo cha wewe kutumia bali ni washirika pamoja wa uumbaji wa MUNGU na washirika pamoja wa uzima wa milele kama mtaishi maisha matakatifu  katika KRISTO YESU.
Wakolosai 3:19 '' Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. ''

-Mwanaume lazima umpende mkeo.


Ndugu zangu, hizo ndio kazi na wajibu wa kila mwanandoa.
Mwanaume ana wajibu na jukumu lake na mwanamke na awajibu na jukumu lake. 
1Yohana 4:7-8  ''Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa MUNGU, na kila apendaye amezaliwa na MUNGU, naye anamjua MUNGU. Yeye asiyependa, hakumjua MUNGU, kwa maana MUNGU ni upendo.''
-Baba tunza Mkeo na sio kutekwa na wanawake wengine mwisho ulete ukimwi kwa familia yako,  ni mbaya sana.
Usitamani mke wa mwenzako bali mtunze mkeo naye apendeze kama hao wake za wengine.
-Husika na mkeo tu maana wengine wote ni sumu kwako, unaweza kukosa mbingu kwa sababu tu ya tamaa za wanawake wasiokuhusu.
Mathayo 5:28 ''lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. '' 

=Kumbuka haya na usije ukasahau.
-Kama Mwanamke Atageuza Na Kutaka Mmewe Amtii Mgogoro Mkubwa Unaibuka.
- Kama Baba Akipunguza Upendo Lazima Migogoro Ije.
Upendo Unastiri Wingi Wa Dhambi.
1 Petro 4:8 '' Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. ''

Ndugu Mwanaume katika ndoa. 
Kuzidisha Chumvi Kidogo Kwenye Ndoa Unampiga Wewe Huna Upendo Kama Agizo La Biblia Linavyokutaka, Baba Ni Kiongozi Wa Familia Hivyo Anatakiwa Abaki Kwenye Nafasi Yake Sio Mama Aichukue.
-Mama Ni Moyo Wa Familia Na Mshauri Mkuu Hivyo Asikilizwe Sana.
 BWANA YESU anasema '' Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.-Yohana 13:34''
-Tumia Udhaifu Wa Mme/mke Wako Kama Ndio Silaha Kuu Ya Kumpenda Zaidi.
-Mama Aepuke Marafiki Maana Wengi Wanataka Tu Kuvunja Ndoa.
-Msiishi Maisha Ya Kupangiwa Na Wazazi Au Watu Wowote Bali Ninyi Ni Mwili Mmoja Jitambueni Na Mpange Mipango Yenu Wenyewe.
Mwanzo 2:24 '' Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja  ''
-Jambo Kuu Kuliko Yote kwa wanandoa Ni Wokovu Na Kumtii MUNGU.
Warumi 6:23 '' Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu.''
- Kataeni Kuwa Barazani Pa Wenye Mizaha(Zaburi 1:1-3,Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. ).
-Kama wana ndoa hakikisheni hamfungwi nira ya wasio mwamini YESU wala hawaamini Wokovu wa BWANA YESU.
-Msisimane katika njia ya wakosaji yaani msiweke chochote kibaya katika ndoa yetu, msitambikie wa mmoja wenu asiende kwa mganga wa kienyeji maana huko ni njia ya wakosaji.
-Yeyote katika ndoa yetu asikubali kukaa barazani kwa wenye mizaha, barazani kwa wenye mizaha ni kwenye vikao vya umbea na masengenyo. maana ukiwa mtu wa kukaa barazabi pa wenye mizaha hukawii kusambaza siri za mkeo au mmeo na jambo hilo kupelekea ndoa yako kuwa na mgogoro au kutokuaminiana jambo mablo ni hatari.
-Mtiini MUNGU mtaishi.
-Shikeni maagizo yote ya MUNGU yanayofundishwa makanisani au kwenye mikutano ya injili na semina za kiroho au za wanandoa.
Waebrania 13:4-5 '' Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu.  Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.''
Nina mengi sana ya kusema kuhusu somo la leo lakini hapa panatosha kwa sasa, siku nyingine tutaendea.
Kumbukeni kwamba Ndoa bila YESU ni mateso makuu. 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments