UFAHAMU KUHUSU MAOMBI YA KUFUNGA

Na Charles Francis

Kufunga maana yake ni kuutiisha mwili ili uwe na ibada kamili yenye maana mbele za MUNGU, ndiyo tunasoma pale warumi 12:1 "Basi ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake MUNGU, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza MUNGU, ndiyo ibada yenu yenye maana." Kwa hiyo kwa maana nyingine kufunga kwetu kuna onyesha ni jinsi gani tunampenda MUNGU kwa sababu YEYE hufanya kazi na wale wampendao (warumi 8;28). Kufunga ni utii, ni ibada, ni unyenyekevu, ni kubeba mzigo wa maombi ya kile kinacho kutesa. Kila huduma ina mipango yake juu ya kufunga lakini hakuna ratiba ya Kimbingu ya kufunga "unless" kuna maono mengine amepewa kiongozi wa huduma hiyo. Wengi leo hawafungi mpaka watangaziwe kanisani maana wanatamani chapati na supu ya mbuzi, wanatamani washinde wanakula tu, watu wa aina hii wakifunga utacheka sana, maana wanacho fanya wakati wa kufunga ni vituko!! Na kuna tofauti kubwa kati ya maombi yasiyo ya kufunga na maombi ya kufunga. Cha ajabu sana watu WENGI LEO WANA SHINDA NJAA HAWAFUNGI na wanao funga kuna vitu wanapishana!!
 Kwa hiyo hata wanao funga kuna vitu wana tofautiana, kwa mfano: mtu kafunga na anafanya maombi lakini anataka watu wajue kuwa amefunga huyu lazima apishane na yule ambaye amefunga kwa unyenyekevu!!

Unapofunga zingatia yafuatayo:
1. Angalia unataka kufanya maombi ya aina gani, vita au mengine. Kumbuka kama ni maombi ya vita yana hitaji utakatifu, utulivu na nguvu ya ziada sana kupambana.
2. Jifunze kusikiliza Roho Mtakatifu anasema uombe nini. Usikurupuke ukaanza kuomba kwa tamaa zako za mwili wako.
3. Unapo omba angalia sana usije ukaingiza uchungu wako wa moyoni, uliachwa na mume wako au mke wako, au uliachwa na mchumba wako sasa unaomba unaanza kulia bila sababu, MUNGU haangalii machozi ya ujinga anatazama huko moyoni kuna nini.


KWANINI TUNAFUNGA??
1. Tunaonyesha unyenyekevu wetu wa mwisho kwa MUNGU wetu.
2. Tunaonyesha kutiisha mwili na kwamba tumejitoa kwa MUNGU. (Rumi 12;1)


Watu wengi wanaona wamefunga kumbe wana shinda njaa, unakuta mtu anakuambia "aaaahhh mtumishi leo sina pesa ya kula nimeona nifunge alafu niunganishe na maombi ya kuombea huduma..." sikiliza hapa, huo ni ujinga!! Funga wakati unacho ili MUNGU aone kweli inatoka moyoni. Mwingine anakuambia mtumishi mimi nimefunga kwa sababu ni ratiba tu ya kanisa letu ila la sivyo nisinge funga.. tambua mtu huyo ameshinda njaa!! mwingine amefunga ila anakunywa maji kabla ya muda wa kufungua,,,ukimuuliza anasema "nakazia mfungo" hata hivyo maji si chakula!! ujinga!! mwingine kafunga ila akipita jirani na hoteli akihisi harufu ya chakula hatoki.. atajizungusha hapo hapo kisha anasema hii ni harufu ya pilau kuku, na hii ni ya chips kavu.. daaaahhhh Bwana YESU nitie nguvu nimefunga..HUU NI UJINGA. Mwingine amefunga lakini kutwa nzima anatembea kwa majirani, akikaribishwa chakula anasema MUNGU unanipima hata hivyo ngoja nile kidogo niache baraka zangu mji huu!!
MAOMBI YA KUFUNGA YANA AMBATANA NA KIU YA MOYO WAKO.. JE, MOYO WAKO UNA KIU GANI??

Charles Francis nawapenda sana. (0752 20 20 52).

Comments