BWANA YESU atukuzwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
Mithali 27:1 "Usijisifu Kwa Ajili Ya Kesho; Kwa Maana Hujui Yatakayozaliwa Siku Moja" .
Natamani kila mwanadamu ausome ujumbe huu hadi mwisho.
-Biblia inatushauri kwamba tusijisifu kwa ajili ya kesho maana hatujui nini kinaweza kutokea ndani ya siku moja.
-Kama wewe umeokoka maana yake kesho yako iko mikononi mwa MUNGU, Hata hivyo MUNGU ndiye anayepanga kesho yako iweje, kuna ambao kesho hiyo watatakiwa kuondoka duniani maana muda wao wa kufanya kazi ya MUNGU umeisha.
-Kuna ambayo kesho yao iko mikononi mwa shetani maana hao hata hawataki kuwa chini ya MUNGU na kuongozwa na BWANA YESU.
Na mara nyingi sana wanaojisifu na kujipangia mambo mengi ya kesho ni wale ambao hawajaikabidhi hiyo kesho yao kwa MUNGU, Biblia inawaambia watu kama hao "Usijisifu Kwa Ajili Ya Kesho; Kwa Maana Hujui Yatakayozaliwa Siku Moja" .
Wakati Wa Nuhu Watu Walitarajia Kesho Yao, Lakini Kesho Hiyo Ikageuka Gharika La Maji. Mwanzo 6:5-7 '' BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. ''
-Ndugu hawa waliendelea na maisha kama kawaida, waliendelea na mipango yao kama unavyoendelea wewe leo na mipango yako bila kumcha MUNGU.
Ndugu yangu, ni heri kesho yako kuikabidhi kwa BWANA YESU kwa wewe kuishi maisha ya Wokovu leo.
Siku za Nuhu watu walikuwa na mipango yao kama kawaida, walikuwa wakioa na kuolewa, wakila na kunywa ila kesho yako ikaangukia kwenye kifo cha gharika. Biblia inasema '' Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.-Mathayo 24:37-39 ''
-Ndugu Usijisifu Kwa Ajili Ya Kesho.
- Usipange Kumcha MUNGU Kesho Bali Mtii MUNGU Leo.
-Leo Yako Ni Ndefu Sana Na Inatosha Kabisa Kumpa YESU Maisha Yako Na Jina Lako Likaandikwa Kwenye Kitabu Cha Uzima Mbinguni.
Kuna ndugu mmoja yeye uzinzi na uasherati umemvaa na kumtumikisha sana, kila siku anawaza uzinzi, kuna wakati akasema kwamba '' Mwaka ujao ukianza tu mimi nitaokoka na kuachana na ukahaba huu'' Mwaka mpya ulipofika alishindwa kuacha na kujisemea tena kwamba ''Kama mwaka huu nimeshindwa kuacha dhambi basi mwakani nitaacha'' Wala hakuacha na mpaka sasa bado yeye ni mtumwa wa ngono. Ni hatari maana hata tu kupanga kwamba nitaokoka mwakani ni makosa makubwa maana anayejua kwamba wewe utaishi mwakani sio wewe bali MUNGU, Je ukifa kabla ya mwakani utaenda wapi?
-Usiitarajie Sana Kesho Yako Maana Kesho Ni Kesho Na Leo Ni Leo. Kesho Ina Matukio Yake Na Leo Ina Mambo Yake. -Usiitarajie Sana Kesho.
Wakati Wa Lutu Watu Wa Sodoma Waliitarajia Kesho Yao, Lakini Kesho Hiyo Ikageuka Tanuru La Motoni. Mwanzo 19:24-25 '' Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa BWANA. Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile.''
-hawa waliipangia kesho yao mipango mingi, kumbe kesho yao ingekuwa kifo cha moto kwa sababu ya maovu yao. Biblia inaendelea kusema '' Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu. -Luka17:28-30 ''
-Ndugu, je unajua kesho kutatokea nini?
-Kwanini isiwe leo wewe kuokoka?
Ndugu Amua Njia Ya Uzima Leo.
Ndugu Wakati Wa Wokovu Ni Leo Wala Sio Kesho Maana Kesho Inaweza Kuja Na Vitu Vyingine.
Kuna wengine walikuwa kwenye Wokovu lakini wameamua kurudi nyuma, ndugu huko nyuma kuna simba na chui, huko nyuma kuna majoka na mbwa, usikubali kurudi nyuma, Endelea mbele na YESU hadi uzima wa milele, Nyuma hakufai, ukirudi nyuma unaweza kugeuka nguzo ya chumvi kama mke wa Lutu, nyuma hakufai, Siku ya BWANA i karibu sana, Luka 17:32-36 BWANA YESU anasema ''Mkumbukeni mkewe Lutu. Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya. Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. ''
-Ndugu, Wakati Wa Kutubu Ni Leo Wala Sio Kesho Maana Kesho Inaweza Kuja Na Vitu Vingine.
-Wewe mteule, Wakati Wa Maombi Ni Leo Wala Sio Kesho.
-Wakati Wa Kumtumikia MUNGU Ni Leo Wala Sio Kesho.
Wingu Limefunguka Leo Na Mbingu Ziko Wazi Leo, Kesho Ina Mambo Yake Ndugu, Amua Vyema Leo Wala Sio Kesho.
Ni heri kutubu na kumpokea BWANA YESU leo ili kesho yako yeye ndiyo aisimamie. BWANA YESU anasema juu waliompokea na wakadumu katika utakatifu wake '' Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.-Yohana 10:28''
Ndugu, Kumbuka neno hili '' Kama Unapenda Kusamehewa Na MUNGU Maana Yake Ni Kwamba Huwezi Kuisha Maisha Yako Pasipo YESU KRISTO. Ukimruhusu YESU Aingilie Maisha Yako Ni Kuruhusu Uzima Wa Milele Uingie Kwako. Hayo yote yanakufaa leo na sio kesho.''
BWANA YESU anawaambia watenda dhambi '' Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.-Yohana 5:40 ''
Ndugu Zangu, Hukumu Ya MUNGU I Karibu.
-Ninaumia Moyo Ninapowaona Wababa Na Wamama Wanatenda Dhambi Bila Hofu.
-Ninaumia Moyo Ninapowaona Wakaka Na Wadada Wakifanya Dhambi Kila Saa Na Dakika.
Ndugu Yangu Unayetenda Dhambi, Je Una Mpango Gani Na Maisha Baada Ya Kufa?
-Watu Uzinzi Na Uasherati Wamegeuza Kuwa Kama Maji Ambapo Kila Siku Lazima Wanywe Maji.
-Uongo,utapeli Na Wizi Imekuwa Kama Jambo La Kawaida Kwa Walio Wengi.
- Kwenda Kwa Waganga Wa Kienyeji Imekuwa Fashion.
Dhambi Za Kila Namna Zinawatesa Wengi.
Hawa Wote Wakifa Bila Kumpokea YESU Hawawezi Kwenda Uzimani.
Ndugu Yangu, Hasira Ya MUNGU BABA Itakaposhuka Juu Ya Wanadamu Duniani Utakuwa Wapi Mtenda Dhambi?
Ndugu, Kimbilia Kwa YESU Leo.
Mwanadamu Unayemkataa YESU Leo Elewa Jambo Hili Kwamba Siku Inakuja Ya Hukumu, Wengi Siku Hiyo Watasema "Ni Heri Nisingelizaliwa".
Ndugu Hakuna Ujanja Wala Ujuaji Utakaokusaidia Siku Hiyo Ila Mpokee YESU KRISTO Leo, Maana Hakuna Uzima Nje Na YESU . BWANA YESU anataka watu waliojikana na kuamua kabisa kwa mioyo yao yote kumtumikia, Luka 14:27 '' Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. ''
-Ndugu zangu, hakuna maoni wala majadiliano. Ni kwamba, Kama unataka uzima wa milele mpokee YESU kama BWANA na mkombozi wako, laa humtaki YESU tambua kwamba wewe uko nje na uzima wa milele. Wakati wa kuamua kupata uzima ni leo wala sio kesho.
Wakati Wa Nuhu Wanadamu Hawakujua Kwamba Kikombe Cha Ghadhabu Ya MUNGU Kilikuwa Kimejaa Na Kumwagikia. Watu Walikuwa Wakila Na Kunywa, Vijana Walipeana Promise Za Kukutana Ili Kufanya Uasherati Kama Kawaida, Makahaba Waliendelea Kujiuza Kama Kawaida Na Waabudu shetani Waliendelea Na Harakati Zao Kama Kawaida, Wasanii Waliendelea Na Pilika Zao Kama Kawaida. Wanadamu Wa Kipindi Cha Nuhu Kama Walivyo Wanadamu Wa Leo Ungewaambia Kwamba Mwisho Wa Watu Wote U Karibu Wangekucheka Na Kuona Umechanganyikiwa, Wangesema Huna Kazi Ya Kufanya, Lakini Mwisho Ulifika Wakafa Wote. Ungewaambia Kwamba Mlima Everist Au Kilimanjaro Ungezama Kwenye Maji Wangekuona Taahira, Hata Ungewaambia Kwamba Mlima Uldizungwa Ungezama Wangekuoma Kichaa Lakini Mwisho Ulifika Wakafa Wote.
Ndugu Yangu Mimi Sijui Kuna Nini Mbele Yako Lakini BWANA YESU Kwa Upendo Mkuu Anakuambia "Tubu Na Kuiamini Injili, Maana Ufalme Wa Mbinguni Umekaribia" (Marko 1:14-15).
Hizi Sio Nyakati Za Kuacha Mgongo Wazi, Ni Nyakati Za Kutubu. BWANA Yu Karibu.
Nasukumwa kuendelea kukupa neno la maonyo lakini hata kwa hiki nilichokisema kimekufaa sana na hakika utaamua vyema kwa Kumpokea BWANA YESU.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments