USIMKOSEE MUNGU HESHIMA KWA KUKOSEA KUANDIKA JINA LAKE.

BWANA YESU atukuzwe ndugu.
naomba leo nikupe ujumbe huu ili ukusaidie na wewe hakikisha unawasaidia wengine.

2 Kor 4:3-4 ''Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake KRISTO aliye sura yake MUNGU.''
-Kupitia andiko hilo hapo juu utaona kwamba 
              =Kuna MUNGU yaani YAHWEH.
              =Kuna KRISTO yaani BWANA YESU.
              =Na kuna mungu yaani shetani.
Ndugu Zangu, Kuna Tatizo Bado Lipo Kwa Baadhi Ya Ndugu Zetu Hapa La Kumuandika Mungu Kwa Herufi Ndogo Zote Mfano Wengi Wanaandika Maneno Haya Wakimaanisha Mungu Wa Mbinguni "mungu, bwana, yesu, jehova, yahweh, roho mt na wengine wanaandika bwn" Hii Ni Mbaya Sana, Ndugu Zangu Hakuna Popote Kwenye Biblia Ambapo Jina La MUNGU Aliye Hai Lilianza Kwa Herufi Ndogo.
 Kwanini Tunafanya Hivyo? 
Natamani MUNGU Amkee Kila Anayefanya Hivyo Maana Hata Darasani Tu Hakuna Jina La Mtu Linaloanza Na Herufi Ndogo, Je BWANA Wa Mbingu Na Nchi Si Ni Zaidi?
 Hua Napata Mashaka Sana Mtu Akiniandikia "bwana au mungu akubariki" huwa siamini kama anamaanisha MUNGU Aliye Hai. Majina ya MUNGU aliye hai huanza kwa herufi kubwa, wanadamu leo majina yao yote huandika kwa kuanza na herufi kubwa lakini akifika eneo la kuandika meseji kwa simu au ujumbe au comment mitandaoni popote atakapoandika jina la MUNGU huandika na herufi ndogo zote, ni uovu mkuu ndugu.
Binafsi kuna ndugu zaidi ya 7 waliwahi kunishukuru kwa Neno ambalo nilifundisha lakini waliandika hivi  ''Mtumishi MABULA naomba mungu akubariki sana tena akuongezee baraka kwa roho wake mt kupitia jina ya bwna yesu kristo''
Jumbe kama hizo hunifanya hata nitake kutoa machozi maana anayeandika hata sijui anamuabudu nani? maana angekuwa anmwabudu JEHOVAH angeandika mungu kwa herufi kubwa maana mungu kibiblia ni miungu. wanadamu wameshupaza shingo, hawaonyeki lakini ndugu nakuomba uwaambie. atakayekusikiliza atafanya vyema.

 MUNGU aliye hai huandikwa kwa herufi kubwa, ona mifano hii kutoka kwenye Biblia takatifu.
-Zaburi 83:18 '' Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote. 
-Zaburi 68:20 ''Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. 

 - Wafilipi 2:10 '' ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. 

- Mithali 15:3 '' Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema. ''

  -Au Hata Kutoka 6:2-3 ''  Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao. ''

Ndugu Zangu Inaumiza Sana Kwa Hili Maana mungu ya herufi ndogo kwenye Biblia Inamaanisha shetani Soma mfano mmoja tu katika mifano mingi iliyo ndani ya Biblia 
1 Wafalme 18:25 '' Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. ''.
 -mungu hapo inamaanisha shetani.

 Ndugu Usiache Kumkemea Na Mwingine Yeyote Utakayemuona Anakosea Kwenye Hili, Mpe Ufahamu Ili Ajue Maana Hata Jina lake Kaanza Kwe Herufi Kubwa.

-Ndugu Zangu Watumishi Wa MUNGU Ni Vibaya Kufupisha Maneno Hasa Yanayomhusu MUNGU, YESU KRISTO Au ROHO MTAKATIFU, Kuna Watumishi Siku Hizi BWANA Wanaandika Bwn, MUNGU Wanaandika Mngu, Ni Mbaya Sana. Neno La MUNGU linakuwa  Gumu Sana Kulielewa Kwa Watu Ambao Nuru Ya KRISTO Haijaingia Ndani Yao maana wanasoma majina ya MUNGU yasiyo sahihi na yanaandikwa na watumishi kabisa, Sasa Wewe Mtumishi Unayetakiwa Kuwasaidia wengine wewe ndio Unaweka Madoido Yako Kwa Kufupisha Maneno Hata Watu Hawakuelewi Kabisa Yaani Ndio Unaongeza Kuwapoteza. Kumbuka Sio Wote Wana Uelewa Kama Wako Mtumishi Na Hakuna Mstari Hata 1 Wa Biblia Uliofupishwa Kama Unavyoandika Wewe.
Kwanini Usiandike Kama Biblia Ilivyo Tu? 
Yohana 1:12 Inasema "Bali Wote Waliompokea(YESU) Aliwapa Uwezo Wa Kufanyika Watoto Wa MUNGU, Ndio Wale Waliaminio Jina Lake".
 Unakuta Mtumishi Kaandika Hivi Yn 1:12 "bal Wt Wliompkea Alwpa Uwz W Kufnyka Watt Wa Mung" 

Ndugu Kwa Hili Tunakosea Sana, Kuna Mtu Hiyo Bal Atadhani Balaa Badala Ya Bali. Mimi Ndugu Wengi Wameniambia Wana-print Au Kuya-copy Masomo Yangu Sasa Najiuliza Ningekua Nafupisha Vifungu Ingekuwaje? 
Tubadilike watumishi wote maana hayo ni machukizo.


 -Moja ya makosa makubwa wanayofanya watu mtandaoni ni kushindwa kumpa MUNGU utukufu wake, ni ujinga kuandika mungu ukikusudia Mungu wa mbinguni, Hata jina lako wewe unaanza kwa kuandika kwa herufi kubwa je MUNGU si ni zaidi?
 Kwenye Biblia palipoandikwa neno ''mungu'' maana yake ni miungu. Mungu wa kweli tunatakiwa tumwandike hivi ''MUNGU au Mungu au BWANA au YESU KRISTO au  ROHO MTAKATIFU'.
Kufupisha jina la MUNGU nayo ni kukosekana  ufahamu wa Kimungu ndani ya mtu huyo, ni  hatari sana na ni moja ya machukizo kama hayo mengine unayoyafahamu wewe. wengi leo kwa sababu ya ufahamu wao kutekwa na shetani huandika mungu au M'ngu, au yesu kristo, au bwana au bna au god au roho mt wakimaanisha MUNGU wa mbinguni, haiko hivyo ndugu yangu na hata ROHO MTAKATIFU hakuna popote kwenye Biblia akiitwa roho mtakatifu.
Vitu hivi ni vibaya sana.

  Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments