WACHA UCHOYO, JIFUNZE KUTOA

Na Moses Chapa.
MARKO 6;41-42....Akaitwaa ile MIKATE MITANO na wale SAMAKI WAWILI, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; na wale samaki wawili akawagawia wote......... Wakala wote wakashiba........ Na walioila ile mikate wapata elfu tano wanaume.......
Hebu fikiri wakati kina Petro wanaenda kwa watu elfu tano na mikononi wameshika kapu lenye mikate 5 iliyokatwa katwa na samaki 2,inawezekana wakawa wanawaendea watu huku wanajiuliza sasa YESU anatuambia tutoe hivi visamaki 2 na vipande vya mikate kuwapa hawa watu haoni NI VICHACHE, si vitaisha vyote hata hiyo robo haitawatosha kwa watu hawa walio wengi? Inawezekana pia Wakawa wanaenda wakisita sita pale wanapoangalia kapu kisha wakiwaangalia watu elfu 5 akilini mwao ilikuwa haingii.Walipoanza kuchukua hatua ya kutoa kile kichache kwa watu wengi wakashangaa kile kichache kilichopo ktk kapu hakipungui,wakitoa kinatokea kingine,wakitoa samaki wawili kapu linajaa tena samaki watano,kila wakitoa maongezeko yanakuja ktk kapu ili atoe tena kwa mwingine...Wakashangaa sana hata vikawatosha watu elfu 5 waliokuwa wanaogopa kuwapa wakidhani watamaliza...
Basi nawe Jifunze kutoa wacha uchoyo,tatizo una roho ya umaskini inayokufanya uwe mchoyo,maana unafikiria nikitoa nitakosa na kama sitopata kingine,unawaza si nitakuwa muhitaji,unawaza ngoja kwanza nikipata kingi ndio nitatoa,na ukipata hicho kingi bado hutoi,napo hujiamini kwakuwa tatizo lipo ndani kuna umaskini unaokufanya uwe mchoyo,hujui kama ungetoa hicho ulicho nacho kapu lako lisingepungua unatoa laki moja unaletwa nyingine kuliplace iliyotolewa ili uweze kutoa zaidi kwa wengine...Kwani kina Petro kadri walivyotoa vile vichache ndivyo kapu lilivyokuwa linaongezeka..Kumbe Ukitoa unapanda mbegu itakayokusaidia kesho kwani utakuwa unajiwekea akiba,Mstari 43 inasema .... Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia..Tunaona kina Petro walipokusanya vipande vilivyobakia wakapata akiba ya vikapu kumi na viwili..Ukitoa leo unajiwekea akiba ya baadae itakayowafaa wahitaji wengine,kadri unavyotoa kapu lako halipungui ndivyo unavyojiwekea akiba kwa wahitaji wenye shida ...Kama kina PETRO wangegoma kutoa na kuwa wachoyo ,wangeendelea kubaki na kapu lao moja lenye vipande 5 vya mkate na vijisamaki 2,wangekosa maongezeko ya vikapu kumi na viwili vilivyojaa mikate na samaki..Basi ukiwa mchoyo utabaki na hicho hicho ulicho nacho hutopata akiba ya vikapu 12..
Kama unataka kufanikiwa wacha uchoyo,jifunze kutoa kile ulichonacho,kama utatoa pesa,nguo,chakula ndivyo unajikuta unapokea hizo Baraka,kwani uliowapa watamshukuru Mungu kwakuwa walikuwa na hitaji watasema MUNGU AKUBARIKI ina maana ubarikiwe ili upate zaidi, basi MUNGU atakupata zaidi ili uweze kuwasaidia wengine...Hata kama unakipaji kitoe kwa watu ukifundisha kwa furaha hao watu watakushukuru na kukubariki ndivyo zile Baraka zinazidi kwako na kukuongezea ujuzi ili uzidi kuwafundisha wengine....Wewe mke kama utatoa pesa yako kumnunulia mumeo viatu kisha utavishika vile viatu na kuvinenea,na kusema,''ninatoa sadaka ya hii ya viatu kwa mume wangu,akivivaa miguu yake itulie isizulele hovyo kwa michepuko wala kwenye vilabu vya pombe, miguu yake ikitoka kazini tu kituoa cha kwanza nyumbani isiwe kwa michepuko wala vilabuni ,katika jina Yesu'',unamaliza..Unampa mumeo anapokea akivaa kwa furaha anashangaa unavyomjali anakushukuru na kumshukuru MUNGU kwa kumpa mke anayemjari,furaha yake inazidi inachia Baraka kwako, utazidi kupokea upendo wake naye atakujali kwa kiasi kikubwa...
Basi wacha uchoyo sikia YESU anasema ktk

LUKA 6;38......WAPENI WATU VITU, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa
MBARIKIWE.....

Comments