BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la hai la MUNGU.
Mwanzo 19"17b '' Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea.''
Jiponye nafsi yako, hkika huu ni wakati wa kuziponya roho zetu na nafsi zetu, roho ni muhimu sana kupokea uzima sasa, dunia itapita na hakuna wa kudumu hapa.
Katika maisha ya leo kwa wanadamu wengi kuna tatizo kubwa.
Tatizo hilo ni Watu siku hizi Badala Ya Kuhangaikia Zaidi Roho Zao Wao Wanahangaikia Zaidi Miili Yao.
Mwanzo 4:7 '' Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. ''
Mtu Yuko Tayari Kumsikiza Kwa Makini Sana Mganga Wa Tiba Mbadala Akielezea Aina Za Vyakula Ambavyo Ukila Unanenepa Na Kuwa Na Nywele Ndefu Kama Za Wahindi Lakini Mtu Huyo Huyo Hayuko Tayari Kusikiliza Neno La MUNGU Ambalo Kwa Hilo Akitii Atapata Uzima Wa Milele. BWANA YESU anasema
Marko 8:35-37 '' Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?''
Kuna saa ya dunia kuharibiwa lakini walio na KRISTO haitawahusu. BWANA YESU anawaambia wanaomtii ''Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.-Ufunuo 3:10-11 ''
Ndugu Yangu, Mwili Wako Hata Kama Ukiupamba Na Kuurutubisha Kiasi Gani Ipo Siku Utatengana Nao, Mwili Utazikwa Na Wewe Utavaa Mwili Mpya Tayari Kwenda Uendako, Kama Unavigezo Vya Mbinguni Utaenda Na Kama Si Mbinguni Basi Jehanamu.
Ndugu, Yangu Rutubisha Zaidi Roho Yako Na Sio Mwili. Mwili Huu Unajua Wenyewe Hauendi Mbinguni Ndio Maana Unakutumikisha Wewe. na pia ukienenda kimwili katika maisha yako Biblia inakuonya, 1 Kor 3:3 '' kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?''
MUNGU hataki sisi tuwe watu wa mwilini.
Ndugu,Nakushauri Rutubisha Roho Kwa Kuokoka,
-Kumtii KRISTO.
-Kuliishi Neno La MUNGU.
-Kwenda Ibadani Kanisani.
-Kufunga Na Kuomba.
-Kujifunza Neno Kila Siku.
-Kujitenga Na Dhambi Zote.
Siku Ya Mahesabu I Karibu. BWANA YESU anasema katika Ufunuo 22:11-12 '' Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. ''
-Kila Mtu Siku Hiyo Atalipwa Sawasawa Na Alichotenda Wakati Akiwa Hai Dunia. Kumkataa YESU Ni Kukataa Uzima Wa Milele.
Kila Jambo Lina Majira Yake.
Mhubiri 3:1-2 '' Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; ''
-Kuna Wakati Wa Kuzaliwa Na Wakati Wa Kufa.
-Kuna Wakati Kupanda Na Wakati Wa Kung'oa.
-Wakati Wa Kubomoa Na Wakati Wa Kujenga.
-Wakati Wa Kulia Na Wakati Wa Kucheka.
-Wakati Wa Kuomboleza Na Wakati Wa Kucheza.
- Wakati Wa Kuongea Na Wakati Wa Kunyamaza.
1 Kor 6:2 '' Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa ''
Tatizo La Watu Wengi Ni Kushindwa Kujua Kwamba Wakati Huu Ni Wakati Wa Nini?
-Ndugu yangu, wakati huu ni wakati pekee wa wokovu.
-Hakuna anayeweza kuokoka baada ya kufa.
-Huu sio wakati wa kucheka bali kulia katika maombi, huu sio wakati wa kucheza ni wakati wa kuomba maombi na kutubu.
-Wakati Wengine Wanazaliwa Kiroho Kuna Wengine Wanakufa Kiroho.
Ndugu Huu Sio Wakati Wa Kufa Kiroho Ni Wakati Wa Kuzaliwa Upya Kiroho Kwa Damu Ya YESU.
Warumi 5:9-11 '' Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na MUNGU kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika MUNGU kwa BWANA wetu YESU KRISTO, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.''
-Kuna Watu Wakiambiwa Wakati Huu Ni Wakati Wa Maombi Wao Ndio Kabisa Wakati Huu Ni Wa Anasa,
-Kuna Watu Wanacheka Sasa Ukiwaambia Habari Za Kuokoka, Hawataki Kuokoka Wala Hawamtaki YESU Lakini Wasipotubu Utafika Wakati Wao Wa Kulia Wakiwa Jehanamu, Sasa Wanacheka Wakati Wanatakiwa Walie Sana Kwa Uchungu Unaoambatana Na Kutubu.
Yohana 3:17-20 '' Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. ''
-Huo Sio Wakati Wa Kuishi Duniani Kama Hakuna Kuondoka. Siku Ya BWANA I Karibu Sana, Huu Ni Wakati Wa Kutubu Sio Kutenda Dhambi.
Mathayo 3:2 '' Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. ''
-Ndugu Yangu, Siku ukifariki Hakuna Atakayeweza Kukusikia Kwa Lolote. Ndugu Watalia Sana Lakini Hautawasikia. Wakati Huo Wewe Utakuwa Umefika Eneo Lako Sahihi. Kama Ulimcha MUNGU Katika Wokovu Wa BWANA YESU Utakuwa Mbinguni, Kama Ulimkataa YESU Na Kuishi Maisha Ya Dhambi Utakuwa Kuzimu Wakati Huo.
Mathayo 25:31-34 ''Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na BABA yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; ''
Wakati Wa Kutengeneza Njia Yako Ni Leo, Kama Unatengeneza Njia Ya Mbinguni Ubarikiwe Na BWANA YESU, Kama Unatengeneza Njia Ya Kuzimu Kwa Kufanya Machukizo Badilika Maana Mbingu Inakuhusu Kama Tu Ukimpokea BWANA YESU Leo Na Kuanza Kuishi Maisha Ya Wokovu.
Matendo 16:30-31 '' kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini BWANA, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako''
Kuokoka Sio Dini Mpya Ila Ndio Dini Ya Biblia, Tena Wokovu Ndio Dini Ya Mwanzo. Mtu Anayesema Dini Au Dhehebu Lake Ni La Mwanzo Hajui Alisemalo, Injili Ya Wokovu Ndio Injili Iliyofundishwa Na BWANA YESU Mwenyewe Pamoja Na Mitume Wake.
Zaburi 32:1-2 ''Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila. ''
Kwahiyo Wokovu Ndio Dini Ya Kwanza. Ndugu, Huu Ndio Wakati Wa Kutengeneza Njia Yako, Jambo La Kwanza Hakikisha Jina Lako Limeandikwa Kwenye Kitabu Cha Uzima, Okoka Na Jina Lako Litaandikwa Kwenye Kitabu Cha Uzima.
BWANA Yu Karibu.
Luka 15:7 '' Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu. ''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments