WAKATI WA KUNYAKULIWA KWA KANISA LILILO MWILI WA KRISTO.


Na Emmanuel Kamalamo.
Bwana Yesu asifiwe!
Karibu katika somo hili linalohusu haswa kunyakuluwa/kuchukuliwa kwa kanisa (mwili wa Kristo) hapa duniani. Tunapozunguzumza "MWILI WA KRISTO" tunamanisha "KANISA" na Kamisa si dhehebu flani hapa duniani bali Wakristo wote waliookoka dunia nzima, waliozaliwa mara ya pili na kuishi maisha ya utakatifu na wakiwa katika kumgoja Bwana Yesu aje kuwachukua. Jambo hili linathibishwa katika Waebrania 9:28 "KADHALIKA KRISTO NAYE, AKIISHA KUTOLEWA SADAKA MARA MOJA AZICHUKUE DHAMBI ZA WATU WENGI; ATATOKEA MARA YA PILI, PASIPO DHAMBI, KWA HAO WAMTAZAMIAO KWA WOKOVU" Kwa hiyo, ujio huu wa pili wa Yesu hauji na "MSAMAHA WA DHAMBI" bali ni ujio wa kuja kulichukua kanisa lake linalomngoja.
Kanisa litakapo "NYAKULIWA" hapa duniani, wakati wa kutangaza/kuhubiri INJILI YA NEEMA NA UTUKUFU WA MUNGU utakwisha. Watu waliookoka watabadilishwa kwa dakika moja, kufumba na kumbua na kuwezeshwa kukutana na Bwana . Pia na waliokufa wakiwa na Kristo watafufuliwa na wao na kuwa katika kundi hilo. 1 Thesalonike 4:13-17 " .....Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka na kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na palapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu , ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.Basi, farijianeni kwa maneno hayo,"
1 Wakorintho 15:52 "kwa dakika moja, kufumba na kufumbua , wakati wa palapanda ya mwisho ; maana palapanda Italia , na wafu watafufuliwa , wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika"

Atakapokuja Bwana Yesu kwa mara ya kwanza katika ujio wake hataonekana kwa ulimwengu. Hapo ndipo watu ambao "HAWAJAOKOKA" watashtuka kuona waliookoka hawapo. Hivyo Yesi atakapokuja mara ya pili ataonekana duniani pote pamoja na watakatifu wake wa mbinguni na malaika wa mamlaka yake...."TAZAMA, YUAJA NA MAWINGU; NA KILA JICHO LITAMWONA..." Ufunuo 1:7. 


Mungu akubariki wewe mwenye taraja la kumungoja Bwana Yesu aje kukuchukua.Endelea kuyatunza "MAVAZI YAKO" yawe safi na ajape usiwe na lawama mbele zake...."Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo" (1 Thesalonike 5:23)
Kuna nyakati tofauti za kuja kwa Yesu kuwachukua (WALIOOKOKA) waliompokea Yesu kama Bwana na Mwokoza wao wakiwa duniani, na ni "WATAKATIFU" wanao yatunza mpaka sasa maisha yao katika "UTAKATIFU". Ujio wa kwanza ni kuwaondoa watakatifu wake, na mataifa (wasiokoka) hawatajua kinachoendelea pindi kanisa(mwili wa kristo) utakaponyakuliwa. Maneno hayo yanathibishwa na Mathayo 24:40-41 " Wakati ule watu wawili watakuwa watakuwako kondoni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa; mmoja aachwa.
Luka 17:34 "Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja ; mmoja atatwaliwa mmoja ataachwa"

Kwa maneno hayo upate picha hii, Yesu atawatwaa watu wake na wale ambao hawajokoka wataachwa, huo ni ujio wa kwanza.
Kuna swali moja, kama "KUNYAKULIWA" kwa kanisa kutakuwa..."KABLA/KATIKATI/ MWISHO WA dhiki kuu?
Maana ya swali hili ni kama kanisa litaingia katika wakati wa hukumu kabla ya kuanzia ufalme wa amani wa miaka 1000.

Wakati huo ulitabiriwa wazi na manabii wengi wa Agano la kale , na Yohana Mbatizaji na Bwana Yesu mwenyewe. Mara ya mwisho twasoma Ufunuo 6 na kuendelea.
Kujibu swali hili si vigumu sana . Tena ni jambo la muhimu kupata jibu linalothibitishwa na Biblia sawasawa. Kusudi tuweze kufahamu vizuri , na tuone kwamba Biblia inatofautisha kati ya "MIPANGO MIWILI YA WOKOVU WA MUNGU"
Upande mmoja inasema juu ya "ISRAELI" na upande mwingine juu ya "KANISA" lililo mwili wa Kristo. Mipango yote miwili imekamilika kwa peke yake .
Kuchanfanya misingi na matokeo yake inaweza kuvuruga maelezo ya maneno ya Biblia.

Kati ya maendeleo ya mipango miwili hiyo twaweza kuona muda mfupi wa katikati au WA kuingiliana. Muda wa namna hii kati ya "TUMAINI LA ISRAELI" kwa ufalme wa hapa duniani na "MWANZO WA KANISA"
Mpango wa kanisa ulidhihirishwa wazi kwa Mtume Paulo. Warumi walipobomoa Yerusalemu na Hekalu mwaka(70 B. K) na hapo tumaini la Israeli lilikwisha kwanza. Lakini hata kabla ya hayo Wayahudi walikataa ushuhuda wa Roho Mtakatifu walipomuua Stephano..

JUU YA DHIKI KUU.
Kumekuwa na maswali juu ya dhiki kuu , kila mtu amekuwa na natafsri yake, lakini tuangalia neno linasemaje.
Ni wazi kwamba wakati wa "DHIKI KUU", au WA "TAABU YA YAKOBO" ni jambo la mpango wa "WOKOVU KWA ISRAEL" Mathayo 24:21"Kwa kuwa wakati huo kutakuwako dhiki kubwa, ambayohajatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe"
Yeremia 30:7 "Ole! maana siku ile ni kuu, hata hapana inanayofanana nayo; maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewà nayo".
Ufunuo 7:14 "Nikamwambia Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndiyo wanatoka katika dhiki ile iliyokuu, nao wamefua mavazi ya kwa damu ya mwana-kondoo"
Wakati huo huo utaingia katika juma la mwaka la 70 alilodhihirishiwa Daniel. Majuma 69 ya mwaka yalikwisha kwa kukataliwa mbali kwa "MASIHI" alipokuwa hana kitu.( Daniel 29:25-26)
Alama zile za kuangamizwa mji (Yerusalemu) na patakatifu (Hekalu) zimekwisha kutimizwa. Maangamizo Yale talitekelezwa na Warumi (watu wa mkuu atakayekuja) Mwaka 70: B.K kufuatana na unabii ule wa Kale Taifa la Israeli latazamia "VITA NA MACHAFUKO" Hata Bwana alisema maneno hayo ya Daniel. Mathayo 24:1-51.....BASI HAPO MTAKAPOLIONA CHUKIZO LA UHARIBIFU, LILE LILILONENWA NA NABII DANIELI, LOMESIMAMA KATIKA PATAKATIFU PAKE (ASOMAYE NA AFAHAMU) NA NDIPO WALIO KATIKA UYAHUDI WAKIMBILIE MILIMANI..."

Katika unabii wa kale wakati wa "KANISA" haukutajwa. Maandiko yanasema...Waefeso 3:5 "SIRI HIYO HAWAKUJULISHWA WANADAMU KATIKA VIZAZI VINGINE; KAMA WALIVYOFUNULIWA MITUME WAKE WAYAKATIFU NA MANABII ZAMANI HIZI"
Wakolosai 1:26 "SIRI ILE ILIYOFICHWA TANGU ZAMANI ZOTE NA TANGU VIZAZI VYOTE, BALI SASA IMEFUNULIWA KWA WATAKATIFU WAKE"
Mungu atakapoanzisha njia za utawala wake na Taifa la Israeli tena juma la mwisho la 70 litakuwa limeanza.(Warumi 11:25 "Kwa maana, ndugu zangu,sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa mataifa uwasili"
Juma hilo la mwaka yaani "MIAKA 7" linagawika "MIAKA 3 NA NUSU" mara mbili
Dan.7:25; 12:7>> Kwa wakati na nyakati 2 na nusu wakati.
Ufu. 11:2>> Miezi 42 na nusu = miaka 3 na nusu.
Ufu.11:3>> Siku 1260= miaka 3 na nusu ya siku 360.
Ufu.12:14>> Kwa wakati na nyakati na nusu wakati
Ufu 13:5>>Miezi 42.
Katika vifungu hivyo unatajwa wakatik wa miaka 3 na nusu ya mwisho inayoitwa zaidi, wakati wa dhiki kuu" au. wakati wa taabu yake Yakobo (Yeremia 30:7)
Siku hizi waisraeli wameanza kukusanyika nao wana serikali ya Taifa lao. Hivyo wakati wa Israeli unaanzà pole pole na ushuhuda wa mabaki ya waamini wa Israeli unadokezwa kidokidogo.
Fuatana nami tujue kanisa litaingia katika. "DHIKI KUU" inayohusu taabu ya Yakobo?

MUNGU AKUBARIKI

ekamalamo@gmail.com

Comments