WASIO NA ADABU MBELE ZA MUNGU.

Na Godfrey Miyonjo.

“usiku umeendelea sana, mchana umekaribia; basi na tuyavue matendo giza, na kuzivaa silaha za nuru, kama ilivyohusika na mchana na TUENENDE KWA ADABU, si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tama zake” RUMI 13:12-14.
BWANA YESU asifiwe.
Inajulikana kuwa watoto wasio na adabu kwa wazazi wao daima huchukiwa na wazazi wao.
Watoto wasio na adabu huonywa na wasiposhika adabu hufika mahali hushikishwa adabu.
Nakumbuka enzi zilee nilipokuwa mdogo, nikiwa pale kwa Mzee Miyonjo, ikitokea nimekosea na Mzee akasema nitakushikisha adabu ilikuwa nageuka haraka na kunyenyekea.
Kwa kuonywa tu nilibadili mwelekeo, kwakuwa nilikuwa najua kuwa kama ningekaidi onyo, kile kitakachofuata ni maumivu yasiyopimika.
Kwa mazingira haya najiuliza juu ya wale WASIO NA ADABU MBELE ZA MUNGU.
Ninawaza juu yetu sisi wanadamu na Baba yetu aliye mbinguni (Mungu), tumeonywa mara ngapi na Mungu, je! Baaba ya kuonywa mara nyingi tumegeuka?.
Ninapata shida sana ninavyofikiri juu ya ghadhabu ya Baba Mungu juu ya wale WASIO NA ADABU MBELE ZAKE.
Ninajiuliza itakuaje siku ile ambayo BWANA ataidhihirisha ghadhabu yake?
Kwa maana imeandikwa, kutakuwako na kilio na kusaga meno.
MATHAYO 8:12.

Imeandikwa watu (wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana) watajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia miamba na milima tuangukie, UFUNUO 6:15-16, lakini haitawezekana.
Hapo ndipo hunifanya niwaze kushika adabu mbele za Mungu kabla haijafika ile siku ya kushikishwa adabu.
Ninatamani kila mmoja wetu leo aamue KUSHIKE ADABU,
Kila mmoja atubu dhambi leo, akimaanisha kuziacha,
Kwa maana kuishi dhambini (kutenda dhambi) ndiyo KUKOSA ADABU MBELE ZA MUNGU.
Kutenda dhambi hadharani au kwa kujifichaficha ni KUKOSA ADABU MBELE ZA MUNGU.
Haijarishi hata kama tunaenda ibadani na kuwatii viongozi wetu wa dini.
Haijalishi hata kama sisi ni viongozi wa dini lakini bado hatujatubu dhambi.
Haijalishi hata kama tunaheshimika kiasi gani katika jamii tunayoishi.
Mungu anatutazama na kutuona HATUNA ADABU MBELE ZAKE na kuchukizwa sana.
Na anataka tushike adadu mapema, ndiyo maana alimtuma BWANA YESU ili atuokoe.
YESU KRISTO ndiye atakayetufanya sisi tupone siku ya ghadhabu ya Mungu,

Mungu ni mwingi wa rehema, atatusamehe kabisa kama tutaamua kunyenyekea chini ya mkono wake, huziondoa dhambi zetu na kuziweka mbali nasi.
Ndiyo maana imeandikwa “Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhabi zetu mbali nasi” ZABURI 103:12.
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
SHIKA ADABU LEO KAMBLA HAIJAJA SIKU YA KUSHIKISHWA ADABU NA MUNGU.

Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu).

Comments