ZIJUE SABABU ZA WEWE KUTIWA NURU NA UTUKUFU WA MUNGU UNAO KUJILIA NA KUWA PAMOJA NA WEWE.

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!

Ubarikiwe wewe unapenda mafundisho ya Neno la Mungu, Ombi langu Roho Mtakatifu akufunulie upate kuelewa somo hili.
Tunaweza kuwa tumeokoka lakini tusijue ya kwamba tumepewa "NURU NA UTUKUFU" Ambavyo vitu tumepewa na Mungu kwa kusudi maalumu.

Somo letu linatoka Isaya 60:1-2 "Ondoka, uangaze,kwa kuwa nuru yako imekuja,Na utukufu wa BWANA umekuzukia.
Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako"

Kuna maneno Mungu anasema kupitia Nabii Isaya, na maneno hayo ni..."KUONDOKA" na "KUANGAZA" kwa sababu "NURU" imekujia. Maana yake kama huna "NURU" usiondoke maana huwezi kuangaza. Maana mwenye Naru ana kazi ya kufanya kupitia Nuru hiyo.
1.KABILA ZA WATU KUONDOLEWA GIZA
KUPITIA NURU YAKE.

2.MATAIFA KUPOKEA NURU YAKO
3.WASIO MJUA MUNGU KUIJILI NURU YAKO
4.KUWALETA WATU KWA KUPITIA UTUKUFU UNAOKUA JUU YAKO.

NURU INAMUIJIA NANI?

-Inamuijia aliyeokoka.
Mathayo 5:16 "Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbeleza ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni"

Ebu angalia maana yake, "NURU" iliyo ndani yako inaangaza kupitia "MATENDO YAKO" Kwa mantiki hiyo, matendo yako ndiyo yanahitajika yatazamwe na watu, hajasema NURU itazamwe bali MATENDO yatazamwe.

CHANZO CHA MATENDO NI NINI?
>Matendo yanayotokana na NURU iliyo ndani yako, ni udhihirisho wa "UTUKUFU WA MUNGU" uliyoko juu yako.
Utukufu unaweza akauona mtu yeyote. Nini maana ya "UTUKUFU"

>Ni uwezo wa Mungu unaojidhihisha kutoka ulimwengu wa Roho na tunauona ulimwengu wa mwili. Maandiko yanatwambia...."NA UTUKUFU WA BWANA UTAFUNULIWA, NA WOTE WENYE MWILI WATAUONA PAMOJA" Isaya 40:5.
Yohana 1:14 "NAYE NENO ALIFANYIKA MWILI, AKAKAA KWETU; NASI TUKAUONA UTUKUFU WAKE.." Yohana 1:14.

Comments