ZIJUE SABABU ZA WEWE KUTIWA NURU NA UTUKUFU WA MUNGU UNAOKUJILIA NA KUWA PAMOJA NA WEWE. (SEHEMU YA II)

Na Emmanuel Kamalamo.
Bwana Yesu adifiwe
Tunaendelea na somo letu. Kama ndiyo mara ya kwanza kulisoma jitahidi kutafuta sehemu ya kwanza.
Wenye mwili wote wanaweza kuuona UTUKUFU WA MUNGU. Na kama tulivyoangalia maana ya utukufu wa Mungu unavyooneka kwa njia ya KIMATENDO au KWA DALILI ZA NGUVU ZAKE.
Ukisoma Injili ya Yohana 2:11 "MWANZO HUO WA ISHARA YESU ALIUFANYA HUKO KANA YA GALILAYA, AKAUDHIHIRIDHA UTUKUFU WAKE, NA WANAFUNZI WAKE WAKAMWAMINI"

Sasa Anglia jambo hili, Wanafunzi wa Yesu hawakuwa na Imani na Yesu kwa Mara ya kwanza japo walikuwa wakitimbia naye. Lakini walipoona "ISHARA" ya "UTUKUFU WAKE" yaani matendo yaliyotendeka machoni pao kugeuza "MAJI" kuwa "DAVAI" ndipo wakamwamini.
Kama wewe umeokoka na unahubiri habari za Yesu, hakikisha una "NURU" na "UTUKUFU JUU YAKO" Nuru unapewa ndani yako...."MACHO YA MIIYO YENU YATIWE NURU" maana yake mtu wa ndani ana macho hivyo anapewa nuru. "UTUKUFU WA MUNGU" unakuwa juu yako (yaani nje) ili watu wauone.
Kama uamini Anglia mtu aliyekuwa ameokoka vizuri akafanya dhambi na kumuacha Bwana, anaondolewa "UTUKUFU WA MUNGU" juu yake na hali yake ya nje inabadilika, anachakaa, kwa nini?....UTUKUFU haupo. Ndiyo maana maandiko yanasema..."TUNABADIRISHWA UTUKUFU HADI UTUKUFU" Maana yake tunabadilishwa kila siku katika mwenendo wetu, Ndipo hapo watu wataona MATENDO yetu ni tofauti na wao kila siku
TUNAHUBIRI KUPITIA UTUKUFU WA
MUNGU ULIYO JUU YETU.

Isaya 66:19-21. "Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa....Nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa yote...Na baadhi yao nitawatwaa kuwa makuhani na Walawi, asema BWANA"
Ili uwe muhubiri mzuri hubiri UTUKUFU WA MUNGU. Mungu amewaota watu "WALIOOKOLA" akawatuma wahubiri "UTUKUFU WAKE" kwa watu wasio mjua.
Swali, je! Walihubiri utukufu gani uliowafanya wakubari kumwamini Mungu wao hadi baadhi yao walioikoka kufanywa "MAKUHANI NA WALAWI" fahamu kwamba walibeba "MATENDO YAO" yanayotoa utukufu wa Mungu, ndiyo maana alisema..."WAKAHUBIRI UTUKUFU WAKE"
Kama huamini nenda kahubiri popote ambapo "MATENDO YAKO HAYANA UTUKUFU" uwe na uhakika hakuna atakayekusikiliza, maana wanakujua kwenye ULEVU, UZINZI, UMBEA, NK umo hapo hakoki mtu. Kasome biblia yako maandiko yatakwambia..."BALI KAMA YEYE ALIYEWAITA ALIVYOMTAKATIFU, NINYI NANYI IWENI WATAKATIFU KATIKÀ MWENENDO WENU WOTE" 1 Petro 1:15.

Mwenendo wa UTAKATIFU ni UTUKUFU WA MUNGU uliyojuu yako. Maana yake unayadhihisha maisha ya ufalme wa Mungu katika ulimwengu wa mwili na ndipo watu watayaona "MATENDO/ISHARA" na kujua wewe ni mtumishi wa Mungu.
Kama ilivyo mwanamke ni "UTUKUFU" Kwa mumewe (mwanamke akifanya vizuri mume anadifiws). Kadharika kanisa limebeba "UTUKUFU WA BWANA"......"LAKINI SISI SITO, KWA USO USIOTIWA UTAJI, TUKIURUDISHA UTUKUFU WA BWANA, KAMA VILE KATIKA KIOO, TUNSBADILISHWA TUFANANE NA MFANO HUO, TOKA UTUKUFU HATA UTUKUFU, KAMA UTUKUFU UTOKAO KWA BWANA, ALIYE ROHO." 2 Wakorintho 3:18.

Comments