AMIN, AMIN, NAWAAMBIA, YEYE AAMINIYE YUNA UZIMA WA MILELE.

Na Mtumishi Peter  Mabula
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
karibu tujifunze neno la MUNGU.
Neno ''Amini' linapatikana mara 98 katika kitabu cha Yohana mtakatifu tu.
Mara nyingi BWANA YESU alilisema neno hilo kuonyesha kwamba kile akisemacho ni halisi 100%.

Neno ''Amini'' maana yake ''Ndio ilivyo'' au ''Itakuwa hivyo''.
Maana ni hii'' Hiki ninachosema ni kweli na hakuna ukweli zaidi ya huu.


Yohana 8:34 '' YESU akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. ''
-Haihitaji mjadala ila ukweli watenda dhambi wote ni watumwa wa dhambi. kumbe ni muhimu sana kutubu na kukataa kuwa mtumwa wa dhambi maana dhambi ni mbaya na dhambi huzaa mauti na mauti ya dhambi huzaa kuzimu na kuzimu huzaa jehanamu.

Yohana 5:24 '' Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. '' 

  Maneno hayo ya ''Amini Amini'' aliyasema BWANA YESU ili tuzingatie kile alichokisema kupitia Neno lake. Kile alichozema YESU ni ndio na hakuna jinsi inaweza kupingwa, na anayepinga siku ya mwisho atajikuta tu akisema hakika hakuna kama BWANA YESU.

Yohana 5:25 '' Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa MUNGU, na wale waisikiao watakuwa hai. ''


-Mara nyingi BWANA YESU alisema neno hilo ili kuuthibitisha ukweli kuhusu kile kinachotakiwa.





kwa ujumbe huu naamini kuna kitu unajifunza na nakuomba ukitendee kazi kila alichokisema BWANA YESU maana hicho ni kwa ajili yako na sio mwingine.

Yohana 7:47 '' Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele. ''

BWANA YESU anatungojea mbinguni.
Anataka tuende bila kukosa.
Ni jukumu letu kuhakikisha tunafika huko kwake.
Yeye hajawahi mkataza mtu ili asiende huko uzimani ila dhambi ndizo zinazawakataza wanadamu kufika huko mbinguni.
BWANA ametupa Neno lake ili tuishi kama neno hilo litakavyo ndipo tutafika huko uzimani.
Neno la BWANA MUNGU linakataza dhambi.
Dhambi kubwa zaidi ni kukataa kuokoka na kuanza kuliishi neno la MUNGU.
Wazinzi na waongo hawawezi kuingia huko mpaka watubu kwanza na muda wa kutubu ni kipindi wakiwa hai, wakifa bila kutubu hawawezi kuingia mbinguni.
-Wachawi na walevi hawawezi kuingia mbinguni hadi watubu kwanza ndipo wataingia, kama hawajatubu hadi wanakufa hawawezi kuingia huko uzimani.
-Makahaba na wezi hawawezi kuingia.
-Majambazi na wauaji hawawezi kuingi.
-Watoa mimba na matapeli hawawezi kuingia.
wasengenyaji na wavaa nywele za bandia wanatakiwa tu watubu na kubadilika ndipo wataingia.
BWANA YESU anatungoja mbinguni kwenye uzima wa milele ila kwanza tutubu na kuacha dhambi na kuanza kuishi maisha matakatifu ndipo tutaenda huko.


Yohana 16:23-24 '' Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba BABA neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. ''

Kuna watu husema ''Nina Dhambi Nyingi Sana Na Ni Dhambi Kubwa Mno Hata Hazisameheki".

- Ndugu Unayewaza Hivyo, Mimi Nadhani Hujaamua Tu Kutubu Na Kuacha Dhambi. BWANA YESU Anasamehe Dhambi Zote, Mkimbilie Tu Leo. Sio Kujifariji Kwamba Dhambi Zako Hazisameheki Huku Ukiendelea Kuzitenda Kila Siku. Hapo Tambua Kwamba Shetani Kakukamata Moyo Hadi Akili Ndio Maana Unajifariji Kwamba Husameheki Wakati Bado Hujachagua Kusamehewa. Msamaha Pekee Uko Kwa BWANA YESU 

Yohana 14:6-7 '' YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. ''
-Kimbilia Ukampokee YESU Na Jina Lako Litaandikwa Kwenye Kitabu Uzima, Ndugu Okoka Kabla Hujaondoka Duniani. 
YESU KRISTO Anaokoa Ukimpokea Leo Unaokoka
Yohana 11:25-27 '' YESU akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? Akamwambia, Naam, BWANA, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe KRISTO, Mwana wa MUNGU, yule ajaye ulimwenguni. ''
-Kama BWANA YESU amekuokoa na unaishi maisha sahihi ya wokovu hata ukifa utaenda kuishi mbinguni.
-Kama una YESU hakika utaishi milele katika uzima wa milele. 

Yohana 14:12-18 '' Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa BABA.
 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
 Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye ROHO wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. '' 

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com
+255714252292.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments