BAADHI YA KWELI AMBAZO NI MSAADA KATIKA MAISHA YA WOKOVU Sehemu ya nne.

Na Nickson Mabena.

Nina kusalimu katika Jina la Yesu popote pale ulipo!, Mungu ametupa neema tena ya kuendelea kujifunza maneno ya Mungu ili tupate kuukulia wokovu!
Leo nakuletea sehemu ya nne ya somo hili, Karibu!

.6.BILA KUPANDA MBEGU HUWEZI KUVUNA.
Kuna msemo usemao “Upandacho utavuna”, hii ni kweli kabisa! Nachotaka tuone jinsi kwenye ufalme wa Mungu kweli hii inavyotumika,
Biblia inasema hivi ‘’Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna” Galatia 6:7
Hii kweli hutumika hata mashuleni, Mwanafunza asiyetaka kujishughulisha na Masomo, kufaulu kwake mtu huyo ni ngumu.
Sasa, sijui kwa nini watu wengi hupenda kubarikiwa na Mungu lakini hawataki kujishughulisha na mambo ya Mungu!, wengine wakifundishwa masuala ya SADAKA basi watakuja na mafundisho potofu na ya uongo aletayo shetani, ya kwamba WACHUNGAJI WANATAKA HELA ndiyo maana wanafundisha kuhusu matoleo!,
nakumbuka sana Mtumishi wa Mungu mmoja aliwahi kusema, “Mtu (anayekuongoza) asipokufundisha kutoa sadaka hakupendi!”, sasa sisemi haya nikiwa na maana kwamba kila anayefundisha kuhusu sadaka basi umsikilize.
Wengi wamepofushwa fikra zao, hata hudhani wanapotoa Pesa, Mda, mali n.k kwa ajili ya Mungu wanapoteza, kumbe hapana!.
Biblia inasema hivi “Kuna atawanyae, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isiyo haki, lakini huelekea uhitaji.” Mithali 11:24
Ukitaka kuongezewa zaidi basi lazima ukubali ‘kutawanya’. Na ndiyo Maana Mungu alipotaka kumpata Mwanadamu, ilimbidi amtoe Mwanae wa Pekee Yesu Kristo, kwa maana hiyo basi kama Mungu angeamua kubaki na Mwanae asingempata Mwanadamu!.
Naomba tujiulize swali hili kwa pamoja,
Je! Unataka kupata nini toka kwa Mungu!?, na Unatoa nini Kwake (Unapanda nini)!?

Alafu, tuyatafakari Maandiko haya
“Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu”. 2Kor 9:6-7
Natamani uone upana wa Kweli hii,
hivi unajua hata Tabia au matendo unayoyafanya sasa yana mavuno!?,

ona Mungu anachokisema “……………; nawapitiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,” KUTOKA 20:5
Kwa maneno hayo naweza kusema kwamba kuna Tabia wanazo watoto zilipandwa na wazazi au mababu zao, na pia zipo tabia/matendo anayapnda leo yatachipua kwa Watoto na wajukuu wako!.
KAMA UNATAKA KUBARIKIWA, KUMILIKI NA KUTAWALA, BASI USIMZUILIE MUNGU ISAKA WAKO AKIMUHITAJI!!.
Kwa hiyo nikuombe, uyatafakari vizuri maneno hayo, pia uyatendee kazi!
Mungu akubariki sana kwa kuusoma ujumbe huu....
Yesu akutunze na azidi kukubariki!!.

Comments