BAADHI YA KWELI AMBAZO NI MSAADA KATIKA MAISHA YA WOKOVU Sehemu ya sita.

Na Nickson Mabena
Bwana Yesu asifiwe ndugu mpendwa katika Bwana....
Nakukaribisha tena kwenye mfululizo wa somo hili,

Tayari sehemu tano za somo hili zimeshapita, na kwenye somo hili nakuletea sehemu ya Sita. kwenye utangulizi wa somo hili nilisema, kwamba imetumika misemo na mafumbo lakini yenye maana kubwa kibiblia!
....tuendelee na kweli ya nane!
8.UKISHINDWA KUPANGA, UNAPANGA KUSHINDWA
Msemo huu ni wa kawaida tu pengine umewahi kuusikia sehemu kama mimi nilivyowahi kuusikia. Lakini kumbe una ukweli ndani yake tena ki-Biblia, kwani neno la Mungu ndio kweli,
kwani Imeandikwa “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli” YOH 17:17
Hebu tuone Biblia inachokisema kuhusu hilo;-
“Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.” MITHALI 16:1

Hilo neno Maandalio ya moyo maana yake ni MIPANGO. Kwenye tafsiri nyingine ya Biblia huo mstari unasomeka hivi “Mipango ya moyo ni ya mtu wa udongo,lakini jibu la ulimi hutoka kwa Yehova” (tafsiri ya ulimwengu mpya)
Kwa hiyo mwenye kupanga mipango ni mwanadamu, lakini Mungu ndiye mwenye kutoa Jibu la Mwisho!, ingawaje kusubiri Jibu la Mungu kunahitajika Uvumilivu wa Hali ya JUU!!.
Kabla ya kufikia jibu la Mungu, kuna mambo mengi sana katikati yanayokatisha tama na kuvunja moyo!, lakini ashukuriwe Mungu kwa Roho wake Mtakatifu anatupa stamina ya kuweza kuvumilia hadi kupata jawabu!.
Najua umepanga uoe, au uolewe (hiyo ni mipango ya moyo wako), lakini Mungu ndiye atakaye kupa jibu kama utaendelea kutulia Miguuni Pake!
Ni muhimu sana kuwa na mipango (Maono), kwani ukishindwa kupanga mipango, ujue unapanga kushindwa!!.

Ngoja nikuulize swali, lakini itabidi ujijibu Mwenyewe……
“Umepanga nini kuhusu kumtumikia Mungu!?, Umepanga nini kuhusu familia yako!?, Umepanga nini kuhusu maisha yako ya Baadaye!?.”
Jiulize Maswali hayo alafu chukua hatua!
ROHO MTAKATIFU YUPO KUTUSAIDIA
Mungu akubariki sana!
....Somo litaendelea...

Comments