BAADHI YA KWELI AMBAZO NI MSAADA KATIKA MAISHA YA WOKOVU Sehemu ya tano.

Na Nickson Mabena
Bwana Yesu asifiwe ndugu yangu popote ulipo, Habari za Mapumziko ya sikukuu ya Pasaka, Ninamshukuru Mungu kwa nafasi hii nyingine tena kwa ajili ya Kujifunza Maneno ya Mungu.
Karibu tuendelee na somo letu, ambalo niliishia sehemu ya nne, ambapo nilielezea kweli ya sita......
7.UWE MWEPESI WA KUSIKIA, UWE MZITO WA KUSEMA.
Mara kadhaa ninapopata nafasi ya Kuongea na Viongozi huwa nawaambia “Hakikisha kiongozi unajua kutunza siri”, Mkristo yeyote anatakiwa kujua jambo hili la Muhimu sana kwenye maisha yetu ya kumtumikia Mungu wetu,
Mara nyingine nawashangaa watu wanaotafuta ushauri au ufumbuzi wa Jambo Fulani kwa kuuliza kwenye mitandao ya kijamii au kwa kuwauli watu wengi, bila kujua kwamba kuna wengine sio sahihi!,
Wakati angetulia Mungu angeweza kumjulisha Mtu ambaye ana msaada wake .
Au mwingine kila unachoambiwa unanataka kukisema!, wakati vingine vilitakiwa viwe vya kwako peke yako!, hebu twende kwenye Maandiko ili tutafute ukweli wa Jambo hili,

Tunasoma
“Hayo mnajua ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;” Yakobo 1:19

Hata kama umesikia, maneno mabaya juu yako, jifunze tu kukaa kimya wala sio ujinga!,
Maneno mengine yanauchafua tu Moyo wako.... ni heri ukakaa kimya tu!
Kuna Mtu mmoja baada ya kusikia maneno mabaya yaliyosemwa juu yake, na mimi pia nikihusishwa kwenye maneno hayo, akaamua kunifuata ili kutaka kujua mimi nitaamua nini juu ya huyo Mtu, Cha ajabu nilimwambia kwa kifupi tu, “Achana naye!”,
Alinishangaa sana, na akalazimisha ili amfuate, mimi nakamwambia achana naye, naye hakuelewa sana kwa nini nilimwambia hivyo, Mimi sikufatilia tena jambo hilo kwani lisingenisaidia chochote!
Mkumbuke hata Yesu, alisingiziwa makosa mengi sana lakini, Alinyamaza kimya!, Sio kwamba alikosa cha kusema, lakini aliamua “AWE MWEPESI WA KUSIKIA, UWE MZITO WA KUSEMA”.
Mwimbaji mmoja anaitwa Ambele Chapanyota, aliwahi kuimba wimbo flani, akasema “Usijitetee, muache Yesu akutetee, usijipiganie, muache Yesu akushindie!”
Wewe, unalionaje Jambo hili!?,
Biblia tena inasema “Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.” Mithali 17:28
Sasa kama Mpumbavu anahesabiwa yote hayo pindi anaponyamaza, JE! Si zaidi sana wewe Usiye Mpumbavu!?
MAANA YANGU HASA KWENYE UJUMBE HUU NI KWAMBA, SIO KILA KITU NI CHA KUSEMA KWA KILA MTU!, SAWA MENGINE YANAUMIZA ILA KUNYAMAZA PIA NI JIBU!
Ubarikiwe na Mungu!.
....Somo litaendelea......

Comments