CHUKUA DAKIKA CHACHE LISHA ROHO YAKO USIKUBALI KULISHA TU TUMBO NA UKASAHAU KULISHA ROHO YAKO.

Na Mchungaji Peter Mitimingi, Mkurugenzi kiongozi wa huduma ya The voice of hope Ministry.

UGALI UNAULIPIA HIKI CHAKULA UNAPEWA BUREEEE!
KARIBU CHAKULA!
Marko 5:15
15 Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.

Yesu hakufurahia kumuona kijana mgerasi akiendelea kuteseka. Wanakijiji walifurahia kumuona yuele kijana akiendelea kuteseka.
Wadadamu wanafurahia kukuona ukiteseka lakini Mungu hafurahii maumivu na mateso yako.

Wanakijiji waliona mambo 4 makubwa yalliyopaswa kuwashangaza na kumshukuru Yesu kwa kazi aliyoifanya kwa kijana wao lakini badala yake wakamtaka aondoke haraka kijijini kwao.
1. Walimuona yule mwenye pepo akiwa AMEKETI
• Wanakijiji hawakuwahi kumuona mwenye mapepo akiwa ameketi yaani akiwa ametulia.

2. Walimuona mwenyepepo akiwa AMEVAA NGUO.
Kazi Tatu za Mavazi:
i. Kupendezesha
• Wanakijiji hawakuwahi kumuona kijana mgerasi akiwa amevaa nguo.
• Walimuona kijana akiwa amependeza wakashangaa sana maana Yesu alimvalisha nguo na kumpendezesha pasipo kwenda dukani.

ii. Kusitili
Walimuona kijana akiwa amesitilika kwa mavazi mazuri yaliyo msitili.

iii. Kutambulisha
Walimuona kijana akiwa katika utambulisho mpya.
• Walimuona kijana yule akiwa kwenye utukufu mwingine.
• Yesu anataka kukupandisha kutoka utukufu hadi utukufu mwingine.
• Yesu anataka kuiondoa aibu yako ya uchi na kukuvika heshima.

3. Walimuona yule mwenye pepo AKIWA NA AKILI ZAKE.
• Wanakijiji walizoea na walimchukulia kijana mgerasi kama mtu asiye na akili.
• Akili inawakilisha heshima
• Yesu anataka kukuheshimisha dhidi ya wanaokudharau.
• Wanadamu wanakuona kama mtu aliyechanganyikiwa.
• Yesu anakupandisha uonekane kama mtu mwenye heshima zake.

1) WALIMUOGOPA sana kijana yule baada ya kuyaona yale Yesu aliyoyatenda.
• Watu wanaokudharau watakuogopa sana baada ya kuona kile Yesu atafanya katika maisha yako.
• Wachawi na washirikina watakuogopa.
• Wanaokuwazia maovu watakuogopa
• Wasiopenda maendeleo yako watakuogopa.


Katika moja ya semina za  Mchungaji Peter Mitimingi.

Comments