HAKIKISHA UNAKUWA CHUMVI YA DUNIA.

BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno hai la MUNGU.
Leo tunazungumzia Chmvi ya dunia.
Wateule wa MUNGU Ni Chumvi Ya Dunia.
Mathayo 5:13 '' Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. ''. 
-Chumvi Ni Kitu Kinayobadilisha Ladha.
-Chumvi Hubadili Chakula Kutoka Kuwa Chakula Cha Kawaida Na Kuwa Chakula Kitamu. 
-Dunia Haina Chumvi Na Inahitaji Chumvi. 
-Chumvi Ya Dunia Ni Wateule Wa KRISTO. 

Watu Wa Dunia Hufanya Dhambi Na Wamejaa Kila Aina Kazi Za shetani.
 Lakini Wateule Ni Chumvi Na Chumvi Hii Ina Ladha, Ladha Ni Matendo Mema.
-Kama chumvi hakikisha unakuwa na matendo memo.
Kama chumvi ni lazima ladha ambayo ni matendo mema lazima yaonekane.
-Lazima iwepo tofauti ya chakula chenye chumvi na kile ambacho hakina chumvi. Kama sehemu fulani ya dunia watakaa watu wengi ambao hawajaokoka tambua kwamba eneo hilo mauaji, wizi, na kila matukio mabaya lazima yatokee sana maana wengi katika eneo hilo hawajafanyika chumvi ya dunia.
 Luka 14:34-35 "Chumvi Ni Kitu Chema; Lakini Chumvi Ikiwa Imeharibika, Itiwe Nini Ikolee? Haiifai Nchi Wala Jaa; Watu Huitupa Nje. Mwenye Masikio Ya Kusikia, Na Asikie."
-Chumvi kama ikiharibika inakuwa takataka, na mteule kama amejichafua kwa uzinzi au dhambi yeyote maana yake huyo ni chumvi iliyoharibika.
-Chumvi ya dunia lazima wawe watu ambao ni wakweli, ndio yao ni ndiyo na sio yao ni sio.

Kuna Watu Hufanyika Wateule Wa MUNGU Kwa Muda Tu, Baadae Hurudi Nyuma Na Kuwa Chumvi Iliyoharibika, Hao Hutupwa Na Kuwa Kundi Moja Na Watenda Dhambi. 

Ndugu Hakikisha Unakuwa Chumvi Yenye Ladha Yaani Hakisha Unakuwa Mteule Mwenye Matendo Mema. 
NINYI NI CHUMVI YA DUNIA. 
Hakikisha Unaambatana Na Matendo Mema maana wewe mteule ni chumvi ya dunia.
-Kizuie Kinywa Chako Kutamka Matusi.
-Zuia Mwili Wako Usitende Dhambi.
-jitenge Na Anasa Za Dunia.
-Usitekwe na mitindo ya kipepo.
-Usitekwe na wanaovaa nusu uchi na kuacha matiti nje, usitekwe na tabia hiyo ya kidunia.
-Usitekwe na wanaojichubua maana hayo ni machukizo.
Wewe ni mteule tena mteule ni chumvi ya dunia hivyo.
-Usiibe
-Usiseme uongo.
Usitamani mke/mme asiye wako.

Chumvi Lazima Iwe Na Ladha, Mteule Lazima Awe Na Matendo Mema.
Mke wa Lutu aligeuka nguzo ya chumvi maana alipata neema ya MUNGU lakini hakumtii MUNGU katikati ya neema hiyo.
Hata leo wengi wamepata neema ya BWANA YESU na kuokoka lakini wasipoitumia vizuri neema hiyo ya wokovu wao wanaweza kugeuka nguzo ya chumvi.
Mwanzo 19:26 '' Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi. '' 
-Amri ya MUNGU kwa wateule hawa ambao walitakiwa kuokoka na moto wa sodoma na gomora ilikuwa ni kusonga mbele bila kuangalia nyuma. lakini mke wa Lutu aligeuka na kuwa nguzo ya chumvi.
-Hata leo akina mke wa Lutu ni wengi, watu hawa huokoka kisha baada ya muda hugeuka na kuangalia nyuma kwa shetani, hugeuka na kurudi dhambini. Ni hatari sana kwa mtu wa MUNGU kuichezea neema ya BWANA na kurudi kwenye dhambi. 
Hata leo amri ya BWANA YESU ni kwamba tuendelee mbele bila kuangalia nyuma.
Marko 13:10,13 '' Na sharti Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote.   Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye atakayeokoka. '' 
-Mwenye kuvumilia hadi mwisho ndiye ataokoka.
-Tunaokoka sasa lakini wokovu huo lazima tuulinde hadi mwisho.
Mke wa Lutu alikuwa ameokoka kabisa maana hadi Malaika wali walimshika mkono ili kumuondoa atoke katika maangamizi, hakika alikuwa ameokoka lakini alitakiwa kuulinda wokovu wake hadi mwisho kwa kutii amri ya MUNGU ya kutokuangalia nyuma.

 Ni Muda Wa Kuukomboa Wakati Tena Ni Muda Wa Kuamka Kutoka Kwenye Usingizi Wa Dhambi, Kama wewe sasa sio tena chumvi ya dunia kama zamani siku unaokoka hakika geuka.
Waefeso 5:14-21 ''  Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na KRISTO atakuangaza. Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya BWANA. Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe ROHO; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia BWANA mioyoni mwenu; na kumshukuru MUNGU BABA sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake BWANA wetu YESU KRISTO; ''. 

-Ndugu Kumbuka Kwamba Kuwa Rafiki Wa Dunia Ni Kuwa Adui Wa MUNGU. Mtu Wa Dunia Hawezi Kuyafanya Mapenzi Ya MUNGU, Mtu Wa Dunia Hawezi Kuukomboa Wakati. 
-Wateule Ni Wale Ambao Wameshaamka Usingizini, Zamani Walikuwa Wamekufa Kwa Sababu Ya Dhambi Lakini Sasa Baada Ya Kumpokea YESU Wamefufuka Kutoka Dhambini Na Kuingia Uzimani. Wateule Wamekuwa Wateule wamekuwa Chumvi ya dunia tena ni nuru ya ulimwengu .
 Waefeso 5:6-10  ''  Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya MUNGU huwajia wana wa uasi. Basi msishirikiane nao. Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika BWANA; enendeni kama watoto wa nuru, kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; mkihakiki ni nini impendezayo BWANA. ''
-Ni Nuru Katika Wema Na Ni Nuru Katika Haki. 

-Ndugu Zangu Huu Ni Muda Wa Kuukomboa Wakati Maana Zamani Hizi Ni Za Uovu. Hakikisha Unakuwa Nuru Ulimwenguni Na Hakikisha Unakuwa Chumvi Yenye Ladha Yaani Mteule Mwenye Matendo Mema. 
BWANA YESU Anakupenda Sana Na Anaendelea Kukuandalia Makao Mbinguni, Dumisha Utakatifu Na Mtii ROHO MTAKATIFU.

 -Unaweza Ukabaki Na Baraka Moja Tu Kutoka Kwa MUNGU Kwa Sababu Akili Yako Siku Zote Inawategemea Wanadamu Tu. Chumvi ya dunia haitakiwi kuwa hivyo.

- Kama Huwezi Kuwa Karibu Na MUNGU Huwezi Kupata Ufunuo Kutoka Kwa MUNGU. Mteule ambaye ni chumvi ya dunia lazima alitambue  hilo.

- Kitu Muhimu Katika Huduma Ni Bidii,Maombi, Utakatifu Na Utii. YESU Aliwapa Huduma Mitume Lakini Kulikuwa Na Tofauti Ya Bidii Kati Yao, Sio Wote Walifanya Kazi Viwango Sawa, Naamini Kabisa Kuna Waliofanya Kazi Zaidi Ya Wenzao Kwa Sababu Ya Bidii Na Utii. Hilo nalo wewe Chumvi ya dunia hakikisha unalitambua na kulitendea kazi.

Wateule Wanatakiwa Wajitenge Na Dunia. Wawe Mzao Mteule.
1 Petro 2:11-12 '' Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze MUNGU siku ya kujiliwa.''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments