ITUMIE NAFASI ULIYONAYO NDANI YA YESU ILI UZUHIE KIBAYA CHA ADUI KISIPITE.

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!
Natumaini mpendwa umzima kabisa mwili na roho. Naposema uzima mwili na roho maana yake Rohoni uko hai na Kristo akija sasa una uhakika wa kwenda mbingu.Na upande wa mwili una afya njema kabisa,ujaruhusu mwili wako kuwa hekalu la magonjwa maana Yesu alikwisha kuyabeba.
Sasa karibu tujifunze Neno la Mungu.
Soma na mimi kitabu cha Esta 4:1-17. ila nitasoma mistari michache ila wewe waweza kusoma sura yote. Maandiko yanasema hivi...Esta 4:13 "Naye Mordekai akaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie ya kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote. Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada wa wa wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?...Bwana Yesu asifiwe!
Unaposoma habari za Esta soma kwa jicho la mtu wa rohoni utaona nafasi ya Esta ya kuwa,,"MALIKIA" katika utawala wa Ahausiero ilikuwa nafasi aliyopowe ili kupitia yeye awe msaada kwa Taifa lake. Hiyo nafasi ya Esta haikumfaa kabisa kwa vigezo vya uchaguzi wa kibinada katika kujipamba na kuwa na muinekano wa uzuri. Esta alipewa nafasi hiyo na Mungu mwenyewe ili aitumie baadae kuzuhia kibaya cha adui kisiingie kwa Wayahudi.
Wasomaji wa bibila mnajua kabisa mpango wa Hamani aliyopanga kuwaangamiza Wayahudi wote. Esta akaambiwa na mjomba wake Mordekai ya kwamba,,Atumie "NAFASI ALIYOPEWA NA MUNGU" ili Wayahudi wasiangamie na endapa hataitumia kuna madhara yatakayowakumbuka Wayahudi pamoja na yeye.
Mordekai alijua kabisa msaada wao ni kupitia Esta kwa nafasi aliyopewa kuwa.."MALIKIA"..Lakini katika ulimwengu wa roho ana nafasi iliyokubwa zadi sana ambayo inampa "MAMLAKA YA KUZUHIA KIBAYA KWA TAIFA LAKE" haijalishi ni vitisho vya aina gani, Mungu aliyenaye Esta ni zaidi ya vitisho vya Hamani. Hivyo ndivyo Mordekai alivyoona,ila Esta aliona yeye ni mke hivyo sheria ikitolewa ni kutii hata kama inawagharimu uhai wao.

Esta alipofumbuliwa macho ya "ROHONI" ili ajue nafasi aliyonayo ni kubwa, Mordekai anafumbua anamwambi,,,"WALAKINI NI NANI AJUAYE KAMA WEWE HUKUUJUIA UFALME KWA AJILI YA WAKATI KAMA HUO" (Esta 4:14b) yaani, kuchaguliwa kwako na kuvikwa "TAJI YA KIFALME" ili kwa ajili ya kuutumia wakati huu wa mabaya ambayo yako juu yetu.
Esta akaitumia "NAFASI" hiyo kwenda kwa aliyempa nafasi hiyo (MUNGU) ili kuzuhia kiapo cha Ahausiero alichomuapia Hamani,alisema hivi,,"KISHA MFALME AKAMWAMBIA HAMANI,HIYO NDIYO FEDHA UMEPEWA, NA FANYA UONAVYO VEMA" (Esta 3:11) maana yake Wayahudi wauwawe. Maombi aliyoyaomba Esta yakageuza mabaya yote.
Mimi na wewe ndiyo Esta wa mwili Krsto katika Agano jipya, ambao tumepewa.."NAFASI YA KUWA WAFALME NA MAKUHANI" kwa ajili ya kuzuhi mabaya anayokusudia Shetani juu ya Taifa,Familia,Ndoa,Kazi nk.Na vita hiyo si ya mwili ni ya kutumia nafasi uliyonayo uliyopewa ili kuzuhia mabaya. Kanisa lazima tujue kabisa jinsi ta kwenda mbele za Bwana kwa ya maombi ili ulinzi wa Ki-Mungu ujidhihirishe mahari Shetani amekusudia mabaya.
Ukisoma Isaya 62:6 anasema hivi,,"Nimeweja walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha bwana,msiwe na kimya;
Mungu anaposema "WALINZI" maana yake ndiyo wazuhia kibaya kisiingia ndani ya Yerusalemu. Hawa walinzi wakizembea(wasipotumia nafasi waliyonayo katika ulimwengu wa roho ya kuomba bila kuchoka usiku na mchana) Yerusalemu inaharibiwa. Kanisa la Tanzania Mungu anatafuta mtu asimame mahari palipo bomoka ili kupitia huyo msaada wa Mungu uonekane. Lakini tukinyamaza kimya uwe na uhakika Hamani shetani atatimiza kusudi lake kupitia Hamani ili kuhakisha NDOA YAKO INAKUFA, UFISINI KWAKO UNAFUKUZWA, TAIFA LINAPIGANA AMANI NA UPENDO VINATOWE, lakini unayo nafasi kubwa sana ambayo ukisima kama mmoja unaweza kuzuhia tasitimie kwa Taifa lako,ndugu yako,rafiko,ndoa yako nk.

OMBEA TAIFA LAKO BILA KUCHOKA.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA,BAADA YA KUFA NI HUKIMU.(Waebrania 9:27)
MUNGU AKUBARIKI.
ekamalamo@gmaili.com

Comments