JE UMECHAGUA NINI KATI YA UZIMA NA MAUTI?

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Nakukaribisha ili tule chakula cha roho zetu.
Karibu.
Mwanadamu Amepewa Kuchagua Kati Ya Uzima Na Mauti, Baraka Na Laana.
 Kumb 30:19 ''Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;''
-Kila mwanadamu mbele yake kuna ama Uzima wa milele au Jehanamu. 
-Mbele yako kuna baraka au laana.
Ni laana kwa mtu yule ambaye ataukosa uzima wa milele.
Uzima wa milele uko pekee katika KRISTO YESU.

 MUNGU Ameshauri Wanadamu Wachague Uzima Lakini Watu Wengi Hujagua Mauti, Ni Hatari Sana. 
Ni Heri Kuchagua Uzima, Uzima Ni YESU KRISTO
Yohana 14:6-7 ''  YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. ''.
-BWANA YESU ndiye njia pekee ya uzima wa milele.

 shetani kazi yake ni Kuangamiza Wanadamu,
 YESU Alikuja Ili Kuwapa Wanadamu Uzima Sasa Kisha Uzima Wa Milele.
BWANA YESU katika kulithibitisha hilo anasema 
Yohana 10:10-11 '' Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. ' '
-Ndugu, Hakikisha Unachagua Uzima.
-Siku ya mahesabu i karibu ambapo kila mwanadamu atalipwa kulingana na aliyoyatenda.
-Je kwa sasa uko upande wa YESU au uko upande wa shetani?
Upande wa shetani huwakilisha kila jambo ambalo liko kinyume na MUNGU na pia liko kinyume na KRISTO.
Dini nyingi ni njia ya shetani kuwapeleka jehanamu waumini hao. Pia kuna baadhi ya madhehebu hayako upande wa KRISTO hata kama madhehebu hayo yanaonekana mazuri kiasi gani mbele za wanadamu maana wana fuata mafundisho ya mashetani ambayo mafundisho hayo yalitabiriwa zamani kupitia Biblia Takatifu.
1 Timotheo 4:1 ''Basi ROHO anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;''
-Je Ndugu yangu bado uko katika Wokovu wa BWANA YESU au umejitenda na Wokovu?
-Je roho zidanganyazo za kuzimu umezishinda au zimekuteka na sasa umemwacha YESU?
-Je bado uko katika fundisho ambalo limejengwa juu ya injili ya KRISTO au umejitoa kwa YESU na kufuata mafundisho ya mashetani?
Andiko hapo juu linakufanya utafakari ili uamue vyema na kubaki katika KRISTO aliye pekee na uzima wako wa milele, ukimwacha YESU tambua kwamba umeuacha pia uzima wa milele.

Kama ulijikuta umechagua vibaya iwe kwa kuamua wewe mwenyewe au kwa kushawishiwa na ndugu au marafiki na ukamwacha YESU, Ndugu yangu, geuka na tubu na BWANA atakupokea. ukimkimbia BWANA YESU hakika unaukimbia uzima wa milele.
 "Kwa Hiyo, Kama Anenavyo ROHO MTAKATIFU, Leo, Kama Mtaisikia Sauti Yake, Msifanye Migumu Mioyo Yenu, Kama Wakati Wa Kukasirisha, Siku Ya Kujaribiwa Katika Jangwa- Waebrania 3:7-8". 
-Huu ndio wakati wa kumtii MUNGU.
-Huu Sio wakati wa kushupaza shingo.
-Huu sio wakati wa kufanya migumu mioyo kuhusu Kumpokea BWANA YESU.

Ndugu Mchague YESU Leo Maana Uko Uzima Wa Milele Katika Yeye Tu
Yohana 1:12-13 '' Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.''

-Dini Bila YESU Ni Upotevu Mkuu. 
-Dhehebu Bila Wokovu Ni Kuharibiwa Tu. 
-Kuhudhuria Ibada Bila Kuokoka Ni Madhara Makubwa. -Kutokumhubiri YESU Anayeokoa Ni Kuwaangamiza Waumini Wako. 
2 Petro 3:18 "Kwa Maana KRISTO Naye Aliteswa Mara Moja Kwa Ajili Ya Dhambi, Mwenye Haki Kwa Ajili Ya Wasio Haki, Ili Atulete Kwa MUNGU; Mwili Wake Akauawa, Bali Roho Yake Akahuishwa,".
-Ni YESU pekee ndiye anayeweza kutupa uzima wa milele.
Tunaisha katika nyakati mbaya sana kwa sasa maana mavumbuzi mengi yanatokea, wengi wanajitenga na Wokovu Na siku ile i karibu sana.

 Kuna Nyakati Saba Ndani Ya Biblia Kuhusu Mwanadamu, Kwa Sasa Tunaishi Katika Nyakati Ya Mwisho Inayoitwa WAKATI WA NEEMA Au Kwa Jina Jingine WAKATI WA KANISA. 

Katika Nyakati Hii Ya Mwisho Kuna Watu Wa Aina Tatu, 
-Aina Ya Kwanza Wanadamu Walio Moto Yaani Waliookoka Kisawasawa.
-Kundi La Pili Walio Baridi Yaani Waliomkataa KRISTO.
-Kundi La 3 Ni Walio Vuguvugu Yaani Kwa MUNGU Wapo Na Kwa shetani Wapo. 
Ufunuo 3:15-16 '' Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. ''

Je Uko Kundi Gani? 
Nakushauri Mpokee BWANA YESU Na Usikubali Kuwa Vuguvugu. 
Kumbuka Hii Kwamba Wapagani Wote Na Dini Zote Na Madhehebu Yote Wanaokataa Wokovu Wa YESU Hao Wako Kwenye Kundi La Baridi. 
BWANA YESU Yuaja Na Ujira Mkononi Mwake Ili Kumlipa Kila Mtu Sawasawa Na Matendo Yake.
Kwa sasa BWANA YESU anasema
''Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;Mathayo 7:24''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments