JE UMEKUFA PAMOJA NA KRISTO?

Na Emmanuel Kamalamo.

Shalom.
Mpendwa, Najua unafahamu siku ya leo wengi tunaadhimsha/kukumbuka kifo cha YESU KRISTO pale msalabani. Jambo la mihimu sana hakikisha kukumbuka kwako kusiwe kwa "HASARA" badala ya "FAIDA"....Utauluza, kwa nini nasema hivyo?
Ebu soma na mimi Wakolosai 3:1 anasema hivi,," Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko ameketi mkono wa kuume Mungu."

Sasa angalia hili neno.."...MMEFUFULIWA PAMOJA NA KRISTO" maana yake ni nini? Ni kwamba, kama ujafa pamoja na Yesu na ukazikwa naye wewe hujafa na wala hujafufuka na Kristo. Utauliza Kamalamo una maana gani? angalia FIKRA/MOYO wako umekamatwa kwa kiasi gani na dhambi (mambo ya dunia). Maisha yako yanaenda sawasawa na dunia hii, na wakati maandiko yanatwambia tuyatafuteni yaliyo juu (Ufalme wa Mungu na haki yake)
Huwezi kusema unakumbuka "KUFA KWA YESU MSALABANI" na wakati mwenyewe hujafa katika dhambi, ndivyo maandiko yanasema kasome Biblia yako utaambiwa..,,"..SISI TULIOIFIA DHAMBI TUTAISHIJE KATIKA DHAMBI? (Warumi 6:2)

Kwa mantiki hiyo kama umekufa pamoja na Kristo lazima na wewe umekufa katika maisha ya dhambi, maana Yesu alikuja kuiaifia dhambi na dhambi aimtawali tene yuko mbinguni ameshinda kifo na mauti.
Hivyo PASAKA hii hakikisha umekufa pamoja na Kristo kama hujafa naye,ili akufufue uketi naye katika ulimwengu wa roho aliko ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba.
PASAKA WETU YESU KRISTO NI UKOMBOZI WA ULIMWENGU WOTE.
PASAKA NJEMA.
MUNGU AKUBARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments