JE UNATARAJIA KULIPWA NINI?

BWANA YESU asifiwe sana.
Karibu tujifunze neno la MUNGU wa mbinguni.
Ufunuo 1:7-8 '' Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema BWANA Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. ''
-BWANA YESU Yuaja Na Ujira Mkononi Mwake, Kila Jicho Litamuona, Na Kila Ulimi Siku Hiyo Utakiri Kwamba YESU Ni BWANA.
 Mathayo 24:30-31 ''  ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu. ''. 
 -Siku Hiyo BWANA YESU Atawatuma Malaika Zake Ili Kuwakusanya Wateule Wako Kote Duniani.
- Dunia Nzima Itaona Wateule Wa MUNGU Wakichukuliwa, -Watenda Dhambi Wataachwa, Itakuwa Ni Hatari. 
- Watachukuliwa Watakatifu Tu.
- Atachukuliwa Dada Aliyeokoka Ambaye Vijana Wa Kila Aina Walimtaka Lakini Yeye Akasema "NABAKI NA YESU BASIII", -Atachukuliwa Mwanamke Aliyeokoka Ambaye Watu Wenye Pesa Walijaribu Kumdanganya Kwa Pesa Zao Lakini Yeye Akasema "MIMI SIO WA TYPE HIYO, NIKO NA YESU"
- Watachukuliwa Wanawake Waliookoka Wanaokataa Umbea, Masengenyo, Uchawi, Ukahaba Na Dhambi Zote. 
-Watachukuliwa Wanaume Waliookoka Wanaokataa Ulevi Na Bangi.
- Watachukuliwa Wababa Wanaokataa Nyumba Ndogo Wala Rushwa.
-Watachukuliwa Wanaume Wanaokataa Umalaya Wala Ujambazi Na Kusema "SIDANGANYIKI,MIMI. NIKO NA YESU". 

Ndugu Zangu, Siku Hiyo I Karibu, BWANA Anawajua Walio Wake Maana Wanamtii.
Marko 13:26-27 '' Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu. ''

 -Majaji Wote Siku Moja Watasimama Mbele Ya JAJI Mkuu YESU KRISTO Na Kulipwa Sawasawa Na Walivyotenda.
Ufunuo 22:11-13 '' Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. '' 
- Walipotosha Na Kuonea Watalipwa Sawasawa Na Matendo Yao Ya Sasa.
-Waliofanya Haki Nao Watalipwa Sawasawa Na Matendo Yao Ya Sasa. 
-Walimu Wote Siku Ya Mwisho Watasimama Mbele Ya MWALIMU Wa Walimu YESU KRISTO Na Kulipwa Sawasawa Na Matendo Yao Ya Sasa. 
-Wanajeshi Wote Na Polisi Wote Siku Ya Mwisho Watasimama Mbele Ya AMRI Mkuu Wa Jeshi La Mbinguni YESU KRISTO Na Kulipwa Kama Matendo Yao Ya Leo, Hakutakuwa Na Mbabe Siku Hiyo Wala Wa Kupigiwa Saluti Zaidi Ya MUNGU. 
-Madaktari Wote Siku Hiyo Watasimama Mbele Ya TABIBU Wa Kweli Watalipwa Kila Mtu Sawa Na Alivyotenda, Aliyetoa Mimba Atalipwa Na Mwema Atalipwa. 
-Wafalme Na Maraisi Siku Hiyo Watasimama Mbele Ya MFALME Wa Wafalme Na Kulipwa Kama Matendo Yao Ya Leo Yalivyo. 
-Kila Mtu Duniani Atalipwa Siku Hiyo.
-Hata Kama Sijakutaja Siku Hiyo Utalipwa.
-Siku Hiyo I Karibu Sana. 
-Maandalizi Ya Kulipwa Mema Ni Leo Ndugu. Mpokee BWANA YESU Leo Utafanya Vyema Sana.

Warumi 6:23 ''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu.''  
-Neema Ya Wokovu Wa BWANA YESU Imefunuliwa Kwa Kila Mtu, Neema Hii Ni Ya Bure Na Tena Ni Ya Muda Tu. 
-Neema Hii Inawataka Wanadamu Waokoke, Mwenye Sikio La Kusikia Atasikia Na Yule Asiye Na Sikio La Kusikia Atadharau. -Huu Ni Upendo Wa MUNGU Wa Ajabu Sana Kwamba Watu Wote Watakaopenda Kuja Nuruni Na Waje Nuruni. 
-Nuruni Ni Kuokolewa Na BWANA YESU. 
-Ni Hasara Mtu Yule Anayebaki Gizani Huku Nuru Anaiona. Mwenye Macho Ya Kuona Na Aone Ili Akimbilie Nuruni Aokolewe.
 1 Yohana 1:9 ''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote ''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments