JE WEWE NI MATEKA WA SHETANI?

Na Mtumishi Peter Mabula, Maisha ya ushindi.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
karibu tule chakula cha uzima wa roho zetu.
 Isaya 5:13-14 ''Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana. Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.''
-Watu wengi wamechukuliwa mateka kwa sababu hawana maarifa.
Maarifa ni elimu iliyo katika matendo.
-Wenye cheo wana njaa ya kupoteza watu.
Kwa sababu ya hayo kuzimu imeongoza tamaa na maelfu ya watu wanaenda huko.

Je ni maarifa gani wanadamu wakekosa hata waingie kuzimu badala ya mbinguni?
Wanadamu walio wengi wamekosa kumcha MUNGU, Hayo ndio maarifa wanadamu wengi wamepungukiwa. wanadamu hawana kitu kimoja tu yaani hawana kumcha MUNGU ndio maana wanakwenda kuzimu.
Mithali 1:7 '' Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.''
-Kumcha MUNGU ndio chanzo cha maarifa  ya uzima. 
-wapumbavu ndio wale ambao hawamtii BWANA na wala hawalitii neno lake na kujikuta wako kuzimu. maana walikosa muda wa kutubu. walikosa kumjua YESU ni nani na ana umuhimu gani kwa ajili ya uzima wa milele. hayo ndio maarifa waliyokosa.
 Kuna aina 3 za maarifa.
Kuna maarifa ya ki-MUNGU, kuna maarifa ya kibinadamu na kuna maarifa ya kishetani.
Maarifa ya kishetani na yale ya kibinadamu ndiyo yanayowafanya wanadamu wengi wanamsahau MUNGU muumba wao na kujikuta kuzimu.

Hosea 4:6 '' Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. ''
-Hakika wengi wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
Biblia ni maarifa ya MUNGU na hapo juu nimesma kwamba Maarifa ni elimu iliyo katika matendo. kutiii Biblia ni kumtii MUNGU.
-Kujua tu kwamba MUNGU ni mmoja haikusaidii  ila muhimu ni kumtii MUNGU huyo maana MUNGU wa kweli yuko katika KRISTO YESU pekee. kujua tu kwamba MUNGU ni mmoja haikusaidii kama humwabudu MUNGU.
-Kujua tu kwamba uzinzi ni dhambi haikusaidii maana unajua ni dhambi na bado unaitenda dhambi hiyo. kujua tu haikusaidii  ila kutubu na kuacha ndio msaada kwako na kitendo cha kutbu na kuacha ndiyo maarifa ya ki-MUNGU yaani unatene akazi elimi ya ki-MUNGU uliyoisikia.
-Kujua tu kwamba YESU KRISTO atakuja na dunia nzima wana ungoja ujio wake haikusaidii  kama humtii na wala haikusaidii kama hujampokea kama BWANA na Mwokozi wako. maana utabaki ukijua kwamba YESU atarudi lakini kama hutatendea kazi neno lake YESU utaenda jehanamu huku ukijua  kabla kwamba YESU atarudi kuhukumu wanadamu wote.
Kujua ni Elimu lakini kutendea kazi njema kile ulichokijua ni maarifa ya ki-MUNGU.
Kujua tu hakuwezi kukupa uzima  bali kutendea kazi hicho ulichokijua ambacho ni cha MUNGU.
Luka 19:43-44 '' Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.'' 
-Anayelitii neno la MUNGU na kulielewa lazima tu atajua wakati aliopo ni wa kufanya nini.
Haiwezekani mtu ana miaka 95 harafu anawaza  kuchumbia ili 
miaka ijayo afuge ndoa. Kama yuko mtu wa hivyo basi huyo hajaujua wakati wa kujiliwa kwake. Muda huu angeutumia kwa toba na maombi na kumtii BWANA YESU na neno lake ingemsaidia. Wakati huu angetubu na kuokoka ili jina lake liandikwe kwenye kitabu cha uzima mbinguni  lakini kwa kukosa maarifa ya kuujua wakati vizuri anaweza kuishia pabaya.
Wakati wa kujiliwa na kifo au janga huja muda wowote hivyo hata kama ndugu una miaka 18 usijidanganye kwamba utaokoka ukifikisha miaka 60. Ndugu sio wote watafika miaka 60 ya kuishi  na hata miaka 20 tu sio wote watafika. hivyo kama hutautumia vizuri muda wako wa sasa wa kuishi duniani hakika unaweza kuishia kuzimu.
Warumi 1:28 -32'' Na kama walivyokataa kuwa na MUNGU katika fahamu zao, MUNGU aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia MUNGU, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; ambao wakijua sana hukumu ya haki ya MUNGU, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.''
-Ndugu kama inakuhusu geuka na tubu maana BWANA YESU anakusubiri tu ugeuke na kutubu.
Kumbuka kwamba kuna jehanamu ndugu, Neno la MUNGU ndilo hilo la kukusaidia ili ugeuke na kutubu na ili usiende motoni.
-Ndugu, ishi maisha matakatifu. 
ikataa dhambi, ikimbie dhambi, uogope dhambi na usifanye dhambi.
-Usikubali kumwacha BWANA YESU kwa sababu tu ya kudanganywa na wanadmu wasio na maarifa sahihi ya MUNGU.

 2 Petro 3:3-7 '' Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la MUNGU; kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha MUNGU. ''

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com
+255714252292.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili


Comments