JIFUNZE KUKATAA MAUTI ISIYO MPANGO WA MUNGU ILI UTIMIZE KUSUDI LA BWANA

Na Emmanuel Kamalamo.


Bwana Yesu asifiwe!
Mungu anapokuwa amekusudia jambo lolote ulipate
katika maisha yako liwe là HUDUMÀ au la
KUKUBARIKI fahamu hata kifo kitazuhiliwa kwako
mpaka jambo hilo litimie maishani mwako.
Ukikaa katika mpango wa Mungu lazima mpango
wa Mungu utimie kwako. Neno linatwambia..."Kwa
maana Daudi, akiisha kulitumikia shahuri Mungu
katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na
Baba zake, akaona uharibifu.(Mdo 13:36)
Kwa hiyo, kama Daudi hakuweza KUFA kwa njia
yoyote katika mapito yake ya hatari ni kwa sababu
ya SHAHURI/MPANGO WA UTUMISHI uliokuwa juu
yake aliouweka Mungu ili autimize baadaye.
Ndicho kilitokea kwa Simioni hakuweza KUFA
MAPEMA mpaka litimie aliloambiwa na Roho
Mtakatifu alione kwa macho yake, kama uamini
soma Biblia yako ndipo utakuwa na uhakika juu ya
jambo hili.
Luka 2:25-26. "Na tazama, pale Yesrusalemu
palikuwa na mtu, jina lake Simioni, naye ni mtu
mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya
Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. Naye
alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba
hataona mauti kabla ya kumuona Kristo wa Bwana."
Sikia neno alilosema Simioni ule mstari wa 29,
alisema..."SASA, BWANA, WAMRUHUSU MTUMISHI
WAKO, KWA AMANI KAMA ULIVYOSEMA; maana
yake "NIRUHUSU NIPUMZKE / NIFE KWA AMANI"
maans nilichokuwa nakitarajia kimetimia ukitaka
kunichukua nichukue. Inawezekana huko nyuma
alipokutana na hatari za alisema.."MAUTI HUWEZI
KINICHUKUA MPAKA NIMUONE YESU MAANA
NILISHAAMBIWA MPAKA NIMUONE" uwe na
uhakika mauti ilipitilia mbali.
Pia Yakobo alimwambia Yusufu mwanae.."Israeli
akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa
nimekuona uso wako, ya kuwa ungali
hair" (Mwanzo 46:30)
Na Israeli akaona baraka za Yusufu mwanae.
Na wewe jifunze kukataa MAUTI zisizo mpango wa
Mungu kwako kabla hujayaona aliyokuhaidia Mungu
uyapate.

KAMA HUJAOKOKÀOKOKA LEO
BAADA YA KUFA NI HIKUMU
( Waebrania 9:27)

MUNGU AKUBARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments