KATAA POMBE MAANA POMBE NI DHAMBI.

BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la ufahamu wa kukuepusha na  jehanamu.
Leo nazungumzia pombe.
Hakuna Mbingu Ya Walevi.
Wagalatia 5:19-21 '' Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU.''
-Ndugu yangu, nakuomba utambue kwamba  Huyo Anayekuambia Kunywa Kidogo Ila Usilewe Ni Kwa Sababu Sio Tu Kwamba Hajui Asemalo Bali Hajui Hata Aonalo. 
-Hatuwezi Kuwa Wahubiri Kuliko Biblia Yenyewe. 

Kama kuna Mchungaji, Askofu Au Padri Ni Mlevi Nakuomba Asikufanye Ukose Mbingu Kwa Mafundisho Yake Manyonge. Biblia Iko Wazi Kabisa Kwamba Katika Orodha Ya Waenda Jehanamu Walevi Wote Wamo Ndani Ya Orodha.
1 Kor 6:9-10 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.''
Pombe ni moja ya dhambi ambayo Biblia inakataza.
Anayefundisha kwamba ''Kunywa kidogo ila usilewe'' huyo anakufundisha mafundisho ya kishetani.
Ndugu Zangu, Kuyajua Mafundisho Ya Mashetani Haihitaji Kufunga Na Kuomba Ili Ujue
1 Timotheo 4:1-2 '' Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;   ''. 
-Nyakati za mwisho ndizo hizi na zitakuwa na mafundisho mengi ya uongo likiwemo fundisho la kunywa pombe.
City Wine Tour_couple in window-Hakauna anayekunywa kidogo harafu asiwe mlevi au mzinzi au mvuta sigara. Kumbuka dhambi moja huchochea nyingine na ndio maana walevi wengi pia hao hao ndio wavuta sigara hodari, walevi wengi ndio wazinzi wakubwa maana dhambi moja huchochea nyingine.
-Ulevi Una Madhara Mengi Hata Kama Biblia Isingekataza.
-Maambukizi Ya Ukimwi Chanzo Chake Kukuu Ni Pombe.
-Talaka Nyingi Ni Kwa Sababu Ya Pombe.
-Familia Kuteseka Na Watoto Kushindwa Kusoma Kwa Sababu Ya Pombe.
-Watumia Madawa Ya Kulevya Karibu Wote Hata Pombe Wanakunywa.
-Wavuta Sigara Na Bangi Karibia Wote Ni Chapombe. 
Biblia Iko Wazi Kabisa Kuhusu Madhara Ya Pombe

Mithali 23:29-35  ''Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.   Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.''. 

-Ulevi huibua ugomvi.
-Ulevi huleta makelele yasiyo na sababu.
-Pombe imesababisha jeraha nyingi tu kwa watu.
-Moyo husema yaliyopotoka kwa sababu ya pombe.
Ndugu yangu, ukisikia fundisho la kuwataka watu kunywa pombe hilo halitokanani na MUNGU ila linatokana na shetani. na mafundisho ya mashetano ni pamoja na hayo.

-Ulevi Ni Ishara Kubwa Kwamb Wewe Ni Mwabudu shetani Maana Uko Mwilini Kuliko Hata Mwili Mwenyewe. 
BWANA YESU Yuaja ndugu yangu..
BWANA YESU anasema.
Ufunuo 22:12-13 '' Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.'' 
-Walevi kama hawatatubu basi kuna kulipwa jehanamu.

-Hakuna Mbingu Ya Makahaba Wala Walevi Wala Wavuta Sigara Wala Waabudu Sanamu, Wala Waongo Na Wachawi Na Wasengenyaji, Wala Watumia Madawa Ya Kulevya Wala Wezi.
Kwanza Askofu au Mchungaji au mtumishi hatakiwi kuwa mnywa pombe, Biblia inakataza kuwa mtumishi larafu mlevi.
 1 Timotheo 3:2-3 '' Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; '' 
-Askofu hatakiwi kuwa mlevi, ukiona askofu mnywa pombe huo hajui uaskofu ni nini.
Biblia inakaza ulevi kwa wacha MUNGU wote kama vile inavyokatazwa dhambi zingine zote.
Warumi 13:13-14 '' Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Bali mvaeni BWANAYESU KRISTO, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake. '' 
-Watu wengi hushindwa kuelewa maandiko maana walevi wote walio makansisani wamekariri andiko la 1 Timotheo 5:23 kama silaha yao kwa ajili ya kuhararisha ulevi.  kiongozi wa kiroho anahararisha ulevi kwa kutumia andiko hilo. Nimeshaulizwa mara nyingi sana kuhusu andiko hilo.
Ngoja nifafanue kuhusu andiko hilo. 1 Timotheo 5:23 '' Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara. ''
-Timotheo anaambiwa kutumia mvinyo kwa sababu ya ugonjwa wa tumbo uliokuwa unamsumbua mara kwa mara. Je wanaotumia andiko hilo kunywa pombe wanakuwa wanaumwa tumbo au?. Dawa ya Timotheo iliitwa mvinyo kwa lengo la kutibu tubu na Paulo hakumaanisha kwamba Timotheo awe mnywa pombe kama walevi wa leo walivyo. Hata ukiamua kuwa mtu wa rohoni tu uatagundua kwamba pombe ni dhambi.
Na Paulo huyo huyo ndiye aliyekataza kunywa mvinyo soma Waefeso 5:18 ambapo Biblia inasema
'' Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; ''
Wengine hudanganyana kwamba BWANA YESU aligeuza maji kuwa pombe kumbe ni maji yaligeuzwa kuwa juice maana hakuna hata mmoja aliyelewa katika harusi ya Kana. Kama Divai ile nyingi vile ingekuwa Pombe si tungesikia watu wengi wakianza kuombewa ili wapone baada ya kupata majeraha yaliyosababishwa na pombe maana divai ilikuwa nyingi na tena tamu sio chungu kama pombe.
 na jambo la muhimu kujua kwa kila mtu ni kwamba hata leo zipo juice nyingi za zinazotokana na zabibu/divai na  sio pombe. Ndizi ni nzuri lakini ndizi hiyo hiyo iliyoiva ukiiacha wiki 2 kisha ukaila utakuta imekuwa tofauti na inaweza ikawa na kazi tofauti na ndizo iliyiovaa kawaida maana kwa muda huu itakuwa imeoza, hata zabibu lazima tujue kwamba sio kila neno divai linamaanisha pombe. kuna juice ya zabibu na kuna pombe pia, pombe ni dhambi.

 Ndugu Yangu, MUNGU Anahitaji 
             1.   Uokoke Kwa Kumpokea BWANA YESU na kuliishi Neno la MUNGU.
           2.    Ishi Kulingana Na Neno La MUNGU.

Mathayo 18:3 ''akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni''
 Ubarikiwe Sana Na Jitahidi Kubadilika na kuacha kufanya dhambi uifanyayo, Na BWANA YESU Atakupa Uzima Wa Milele.

-Kataa pombe na usinywe pombe.

-Pombe ni ibada ya sanamu na ina madhara mengi.
Isaya 5:11 '' Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! ''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments

Unknown said…
Swala hili limekuwa miongoni mwa wakatoliki baada ya kutumia pombe na vyakula kama nyama ya nguruwe! wengi wamekuwa wakisema hayo kutokana na agano la kale lakini tuone biblia inasema nini kuhusu agano jipya na la kale!

Waebrania 8:7,13
"7Maana kama lile agano la kwanza halingalikuwa na dosari, hakungalikuwa na haja ya agano la pili,
13 kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikukuu kitatoweka karibuni,."

tuanze na VYAKULA:

Marko 7:18-23
'Naye akawaambia, "Je, hata nyinyi hamuelewi? Je, hamuelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu kutoka nje hakiwezi kumtia najisi, 19 kwa maana hakimwingii moyoni ila tumboni, na badaye kutolewa nje chooni?" (kwa kusema hivyo, Yesu alihalalisha vyakula vyote.)
20. Akaendelea kusema, "Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia najisi. 21 Maana kutoka ndani, moyoni mwa mtu, hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi uuaji, 22 uzinzi uchoyo, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, kashfa, kiburi na upumbavu. 23. Maovu hayo yote hutoka ndani ya mtu, nayo humtia mtu najisi."

Hayo ni maelezo ya Yesu kuhusu vitu vinavyoweza kumtia mtu najisi
.... Tusome tena,

Waebrania 13:9
"Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata."

Hivyo kwa kuhitimisha kuhusu chakula..
asiwepo mtu wa kumuhukumu mwenzie kuhusu chakula isipokuwa vyakula vya mtambiko kwa mkristo yeyote si vyema kushiriki!

POMBE.
Angalizo;
tunapoongelea kuhusu pombe sio kwamba tunahamasisha kutumia pombe bali tuelewe kile tunachofanya kwa mapenzi ya Mungu!
pombe haikukataliwa ila itumike kwa kiasi.

1Timotheo 5:21,23
"21 Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
23. Usinywe maji tu, bali unywe na divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako, kwani unaugua mara kwa mara."

ndugu mtume Paulo anamweleza Timotheo atumie kama dawa na sio kulewa.
hivyo ndugu unaposoma ujumbe huu basi jitahidi urekebishe tabia yako, usiwe mlevi.

Yoshua Bin Sira 31:25-29
"25 Usijionyeshe kuwa hodari wa kunywa pombe, maana imewaangamiza wengi.
26 Tanuru hupima ugumu wa chuma, na pombe hupima mioyo katika shindano la wenye kiburi.
27 Pombe ni kama uhai kwa mtu akinywa kwa kiasi, Maisha yafaa nini bila pombe?
Imeumbwa iwafurahishe watu.
28 Kunywa pombe kwa wakati wake na kwa kiasi, kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni.
29 Lakini kunywa pombe kupita kiasi, kunaleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha."

Ndugu mkristo kama huwezi kijizuia na kuwa na kiasi ni afadhali kuacha kabisa.

Wakolosai 2:16-18a
"kwa hiyo basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu VYAKULA au VINYWAJI, siku za sherehe, sikukuu ya mwezi mpya au sabato. 17 mambo ya namna hiyo ni kivuli cha yale yatakayokuja; ukweli wenyewe ndiye kristo. 18 msikubali kuhukumiwa na mtu anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee...."

Hata hivyo pia, Yesu alinenewa vibaya kama ilivyoandikwa na muinjili Luka

Luka 7:31-35
"31 Yesu akaendelea kusema, "Basi, nitawafananisha watu wa kizazi hiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani? 32 Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi kimoja na kingine:
'Tumewapigieni ngoma lakini hamkucheza!
Tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkulia!'
33 Kwa maana Yohane alikuja, akawa anafunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: 'Amepagawa na pepo!'
34 Naye mwana wa Mtu amekuja anakula na kunywa, nanyi mkasema:
'Mwangalieni mlafi huyu na mlevi; rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi!'
35 Hata hivyo, hekima ya Mungu imethibitishwa kuwa njema na wote wale wanaoikubali."