KATIKA KIYAMA HAWAOI WALA HAWAOLEWI, BALI HUWA KAMA MALAIKA MBINGUNI.

Na Godfrey Miyonjo

MATHAYO 22:30.
BWANA YESU asifiwe.
Ninatamani watu wote tulio chini ya jua tulijue hili,
Wale wote tunaomcha Mungu tutambue kuwa mambo ya kuoa na kuolewa mwisho wake ni hapahapa duniani.
Ninatamani tuyajue haya ili kila mmoja wetu awe na picha harisi juu ya kule tunakoelekea,
Pia ili kila mmoja wetu asimwache Mungu Eti kwa sababu ya KUOA au KUOLEWA.
Kwa maana nimewaona wengi wamekwenda na maji (wametekwa na shetani) kisa kuoa na kuolewa.
Watu wameamua kumuasi YESU na kuidharau ile kazi kubwa aliyoifanya pale msalabani kisa mume au mke,
Watu wameacha ibada kisa wamezuiliwa na waume au wake zao.
Wengine huenda mbali zaidi na kupeana ahadi za uongo na wenzi wao kuwa “mimi ni wako hapa duniani hadi mbinguni (wa milele)”
Ninayasema haya kwasababu niliwahi kukutana na baadhi ya watu walio na matumaini ya kuoa na kuolewa katika kiyama.
Baadhi yao waliniambia kuwa wataoa wake wazuri, wengine wakasema kuwa wataolewa na wanaume wazuri kule akhera.
Haya ni mawazo ya wanadamu, lakini Bwana wetu YESU KRISTO kwa maneno ya kinywa chake ametamka:
“Lakini wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi” LUKA 20:35.
Kwa maneno haya BWANA YESU anatutaka tusimwasi Mungu kwa sababu ya mume au mke, ndiyo maana mahala pengine alisema, mwenye kumpenda mume au mke kuliko mimi anistahili.
Akatutaka tujikane, kila mmoja ajitwike msalaba wake yeye kama yeyena aamue kumfuata YESU:
“wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata hanistahili” MATHAYO 10:38.
Mtume Paulo alilijua hilo ndiyo maana akasema hakuna wa kutufanya tujitenge na upendo wa Mungu ulio ndani ya KRISTO YESU. RUMI 8:38-39.
Nami ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Maneno haya ni hakika na ni kweli, asomaye na afahamu kuwa KATIKA KIYAMA HAWAOI WALA HAWAOLEWI, HIVYO SIWEPO WA KUMUACHA YESU KWA SABABU YA MUME AU MKE.

Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu).

Comments