KATIKA SAA USIYODHANI BWANA YESU YUAJA.

BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
 ''kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari kwa kuwa katika saa msiyodhani MWANA WA ADAMU yuaja {Mathayo 24:44}

 Ndugu Zangu,
 Siku Ya BWANA I Karibu.
Siku Hiyo Hakutakuwa Na Mwanadamu Wa Kutoa Udhuru, Hakutakuwa Na Wa Kujitetea "Kwa Sababu Mambo Yasiyoonekana Na Kufahamika Kwa Kazi Zake; Yaani, Uweza Wake Wa Milele Na Uungu Wake; Hata Wasiwe Na Udhuru-Warumi 1:20.

 Ndugu Utakaa Wapi Katika Maisha Yako Ya Milele? .
 Biblia Inasema  
"Mwenye Busara Huyaona Mabaya Na Kujificha; Bali Wajinga Huendelea Mbele Wakaumia-Mithali 22:3"
 -Ndugu Yangu Je Wewe Ni Mwenye Busara Au Mjinga? 
Wajinga Wataumia Na Wenye Busara Watajificha. 
-Ndugu Zangu, Siku Ile Pa Kujificha Ni Sehemu Moja Tu Yaani Kwa KRISTO. 
-Ndugu, Nakuuliza Tena Je Wewe Ni Mwenye Busara Au Mjinga? Hilo Unalijua Wewe Moyoni Mwako Ila Kama Unataka Kuwa Mwenye Busara
 "Mwamini BWANA YESU KRISTO, Nawe Utaokoka-Matendo 16:31"
Kama Unautaka Kweli Uzima Wa Milele KUOKOKA NI LAZIMA. -Kukataa WOKOVU Wa BWANA YESU Ni Kuukataa Uzima Wa Milele.
- Ndugu Amua Vyema Leo Na Utapata Raha Nafsini Mwako. YESU Anakuita Leo, Itika Ndugu Na Mpokee Awe BWANA Na Mwokozi Wa Maisha Yako. 
Dunia nzima wanaungojea ujio wa BWANA YESU, Na katika saa usiyodhani atakuja, mtii MUNGU na ishi kama neno la MUNGU linavyokuamuru.
Usijitenge na wokovu wa BWANA YESU maana katika saa usiyodhani kuna kuondoka. na makazi kama hujaokoka yatakuwa kuzimu ambapo haitakiwi mtakatifu yeyote afike huko.

 -Kama YESU Atakukwaza Kwa Jambo Lolote Tambua Kwamba Wewe huuhitaji uzima wa milele. Yeye anasema
'' Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami.-Luka 7:23  ''

  -Ukiwa kwa MUNGU unakuwa hauko kwa shetani. 
Ukiwa nje ya MUNGU, moja kwa moja unakuwa uko kwa shetani. Hakuna sehemu ya kati!
Na BWANA hawataki wote ambao wanasitasita.

 Ufunuo 3:15 {Nayajua matendo yako ya kuwa hu baridi wala hu moto ingekua heri kama ungekua baridi au moto] -Tunapomchagua MUNGU tuachane na ya shetani yote sio kwa MUNGU 50% na shetani 50%,
 MUNGU BABA atuwezeshe tuchague YESU KRISTO 100%
Ndugu, kuna kuitazamia hukumu mbaya kama hatutautambua wakati huu kwamba ni wakati wa kutubu na kuishi maisha matakatifu.
Kama unapanga kutubu baadae je unauhakika hiyo baadae yako utakuwa hai?
Wengi walipanga kutubu wakiwa wazee lakini hata uzeeni hawakufika na kujikuta wako matesoni kuzimu.
Waebrania 10:26-27 '' Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. '' 
Ndugu zangu, huu sio wakati wa kufurahia dhambi, kama kuna dhambi ambayo unadhani huwezi kuiacha nakuomba uende na kumweleza mchungaji wako naye atakuombea. pia okoka na kuomba maombi ya ushindi kupitia jina la YESU KRISTO. Damu ya YESU ina mamlaka ya kukuweka huru mbali na dhambi zilizokutesa miaka mingi.

  -Damu ya YESU inauwezo wa kuvunja minyororo yote ya shetani iliyokua imekufunga kama roho ya pombe, pepo la ngono,uongo,wizi na chochote cha shetani  ambacho ulidhani haiwezekani wewe kukiacha kitu hicho, muhimu ni kumpa YESU maisha yako ili uwe huru .  -mfanye BWANA YESU kuwa namba moja maishani mwako ili uishi mbali na kuonewa na nguvu za giza pia baada ya ulimwengu huu upate uzima wa milele.
-Mfanye YESU kuwa rafiki yako wa karibu zaidi.   -kwa sababu YESU ndie rafiki yako wa karibu zaidi usiache kumshirikisha chochote kinachokusibu kwani yeye ni msaada wa karibu sana. BWANA YESU anasema
Yohana 14:13-15 ''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika amri zangu.   ''

  -shetani asikuteke ndugu ukashindwa kwenda kanisani bali mshinde na kumwaibisha kwa kwenda kanisani ukiwa wa kwanza na tena tenda mema sawasawa na neno la MUNGU.
Hakuna ambacho BWANA YESU hawezi kukitengeneza na kikawa sawa. Sauli alikuwa Jambazi muuaji aliyeshindikana lakini alipokutana na BWANA YESU akageuka muhubiri wa neno la MUNGU kwa mataifa.
-Kuna siku usiyoidhani huko mbeleni utaondoka, je ukiondoka utaenda mbinguni? maana mbinguni wanaingia watakatifu tu waliomtii KRISTO enzi za uhai wao. je utakuwa mmoja wao?
-Zishinde dhambi kwa kumwita BWANA YESU akushindie.
-Zishinde dhambi kwa kuondoka katika baraza za watenda dhambi.
-Zishinde dhambi kwa kukaa mbali na picha za ngono pamoja na kuangalia filamu za nusu uchi.
 1 Yohana 2:15-17 ''  Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. ''

  -Ndugu yangu, kama YESU amenibadilisha mimi kutoka dhambi zote mbaya unazozifahamu nina hakika anaweza kukubadirisha hata wewe ili ufanyike mtoto wa MUNGU kupitia yeye. changamka ndugu kwani wakati wa wokovu ni sasa.
Yohana 3:16-21 '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU. '' 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments