KATIKA WITO WAKO,UMEPEWA UJUMBE GANI?

Na Moses Chapa.

Mtumishi yoyote aliyeitwa ktk wito Fulani anapewa ujumbe na Mungu juu ya wito wake..Huo ujumbe unakuwa ndo msingi wa huduma yake,utakuwa ndo neno la kumuongoza katika njia zake ili atende sawasawa na neno la huo ujumbe..Hata kama akipita ktk maagumu ataangalia hilo neno la ujumbe wake nalo litampa Imani ya kusonga mbele apate kushinda,na kupitia hilo neno la ujumbe atatembea ktk nguvu za huo ujumbe ili liweze kutimia na afanye kwa usahihi..Na huo ujumbe utakuwa na kama ngao ya kumlinda ili adui asiharibu kusudi la neno,kwani Mungu ataliangalia neno alilokupa ili apate kulitimiza kusudi lake..
Mwaka 2009 nilikuwa ktk kikundi Fulani cha wapendwa km Fellowship,tulikuwa tunakusanyika ktk nyumba ya mama mmoja...Ktk kile kikundi tulikuwa na vita kali sana haipiti miaka 5 bila mpendwa mmoja kufa,tena waliokufa ni wapendwa wale wenye moto na Injili,akianza kuchipuka kidogo basi mara ataanza kuumwa marelia kisha anakufa,tulichukulia jambo la kawaida bila kufikiria nyuma ya mauti yale kuna nini?Ilipofika zamu yangu ya kuondolewa uhai ndipo nikajua kipi kipo ktk kile kikundi,usiku mmoja baada ya maombi nikaona nimekufa na maiti yangu ipo uchi wa mnyama ktk mto wenye maji mengi kisha maiti yangu ikaondoshwa na maji...Nikasikia sauti ikiniambia TABIRI UHAI JUU YA WATU WANGU...Baadae nikawa natafakari juu ya ujumbe niliopewa TABIRI UHAI Je unamaana nifufue watu waliokufa,sikuelewa ujumbe unamaana gani?Nitafufuaje mtu aliyekufa?Kwanza nimejiona nimekufa harafu napewa ujumbe tabiri uhai juu ya watu wangu..Wakati naendelea na tafakari nikapewa neno linalohusu huo ujumbe,katika EZEKIELI 13;17 Kuwa si kuwafufua marehemu kama nilivyokuwa nafikiri bali ktk jamii za wapendwa kuna wapendwa wapo mawindo ktk madhabahu za adui wametabiriwa laana ya mauti,ndo maana nikaambiwa huo ujumbe wa TABIRI UHAI JUU YA WATU WA MUNGU unaendana na neno la EZEKIELI 13;17-23 Kwamba sio unakulupuka na ujumbe bila kuelewa vizuri na kuanza kuombea maiti zifufuke,EZEKIELI 13;17 unasema,
Na wewe, mwanadamu, kaza uso wako juu ya binti za watu wako, watabirio kwa akili zao wenyewe; UKATABIRI JUU YAO.... useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ILI WAWINDE ROHO ZA WATU; je! MTAZIWINDA ROHO ZA WATU WANGU, na KUZIHIFADHI HAI ROHO ZENU WENYEWE?...Kumbe ujumbe niliopewa si wa kufufua watu waliokufa km nilivyofikiri bali ulikuwa unataka NIKATABIRI juu ya wakuu wa giza wanaotabiri mauti juu ya watu wa Mungu kwa kuwawinda kutumia hirizi na kila aina ya vifungo ili kuwamaliza watu wa Mungu...Mstari 19-20 anasema kazi ya adui,...... ili KUZIUA ROHO ZA WATU AMBAO HAIWAPASI KUFA, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.................. Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.
Kupitia neno hili sasa nikaelewa ujumbe vizuri wa kutabiri uhai juu ya watu wa Mungu,kuwa ktk kundi letu tunawindwa km ndege ndo maana haipiti miaka mitano anakufa mpendwa tena Yule mwenye moto wa Injili,adui alikuwa ametegesha mitego yake juu yetu,hivyo nilipopewa ujumbe wa kutabiri uhai kwa watu wa Mungu waliopo ktk mawindo ya adui wale waliotabiriwa laana ya mauti watolewe ktk mikono yao wasiwe mawindo tena,ndo maana Mstari 19 anasema, walikuwa wanauwa roho za watu wa Mungu ambao haikuwapasa kufa....
Mstari 21 anasema, Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
Nilipoanza kuufanyia kazi ujumbe hakika neno la ujumbe lilianza kutimia ktk lile kundi mauti ilikoma,na hawakuweza kuzihifadhi roho zao wenyewe nao walikufa kama neno lilivyosema ktk mstari 18 kuwa
je! MTAZIWINDA ROHO ZA WATU WANGU, na KUZIHIFADHI HAI ROHO ZENU WENYEWE?..
Lakini Vita yake haikuwa ndogo nkwani siku moja baada ya kumaliza maombi nililala nikaona, ndege mdogo alipita ktk dirisha langu,akapenya ktk chandarua akatua ktk kifua na kuudonyoa Moyo wangu,kuondoa uhai wangu,nilipata wakati mgumu sana kipindi hicho,ni ushuhuda mrefu ila nataka uone kuwa kama umepewa ujumbe basi utafakari kwa makini,je unaendana na wito uliopewa usikulupuke ktk huo ujumbe bila kuuelewa vizuri,unahusu nini?
Kwani ukianza kutekeleza huo ujumbe vita yako itatokana na huo ujumbe uliopewa..Adui atapambana na wewe ili ujumbe uliopewa usije ukatimia..Lakini hawataweza kukushinda maana MUNGU anaangalia neno lake alilikupa apate kulitimiza..MBARIKIWE....

Leo tuishie hapa,Siku nyingine tutamuangalia YEREMIA tutaona jinsi alivyoteswa sababu ya ujumbe wa wito aliopewa

Comments