KIRI, TUBU NA ACHA DHAMBI.

BWANA YESU asifiwe.
Tunapokuwa katika kukumbuka jinsi huruma za BWANA YESU za ajabu zilizompelekea kuja duniani ili atuokoe.
Hakuna aliye na upendo kama huo. BWANA YESU anasema 
Yohana 15:13-14 ''   Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. ''
BWANA aliupenda ulimwengu  na jukumu limebaki tu kwetu  kuingia katika upendo huu mkuu sana.
BWANA anawataka watu wote leo kumpokea na kutubu na kuacha dhambi ili wawe  katika mipango yake ya uzima wa milele.
 Mathayo 3:2 '' Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. ''
 Jukumu lako ndugu ni kuamua tu kumpokea YESU leo kwa kutubu na kuishi maisha matakatifu.

-KUTUBU ni kugeuka na kubadirika kutoka dhambini na kuungama mbele za MUNGU. 
na ili utubu ni lazima ujue kwamba wewe ni mwenye dhambi.

-BWANA Husamehe Dhambi Zote Kwa Mtu Aliyeamua. 
-MUNGU Hataki Waigizaji Bali Walioamua Kabisa Kutubu, Sio Wale Wanaoamua Kutubu Leo Kwa Sababu Ya Magumu Ili Kesho Ugumu Ukiisha Warudi Dhambini, Hao BWANA Hawahitaji. -Aliyeamua Kutubu Na Kugeuka Lazima AKIRI DHAMBI, ATUBU DHAMBI Na AACHE DHAMBI TANGU SIKU HIYO. 

MUNGU Anaagiza Leo Watu Watubu
Matendo 17:30-31 ''Basi, zamani zile za ujinga MUNGU alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu''

-MUNGU Hawezi Kukusamehe Dhambi Zako Kama Wewe Hujaomba Msamaha. 
Tunaomba Msamaha Kwa Kukiri Dhambi Na Kutubu Kisha Kuacha Dhambi
Wakolosai 2:13-15 '' Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.   ''

 Zamani Za Uovu Zinatakiwa Zipite Na Zije Nyakati Za Utakatifu Utakaoendelea Hadi Milele.
Waefeso 2:1-5 '' Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;  ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.  Lakini MUNGU, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na KRISTO; yaani, tumeokolewa kwa neema.   ''
- Ndugu Kama Unahitaji Msamaha Wa MUNGU, KIRI DHAMBI, TUBU DHAMBI NA ACHA DHAMBI.

 Tukiziungama Dhambi Zetu, Yeye MUNGU Ni Mwaminifu Na Wa Haki Anatusamehe
1 Yohana 1:9 ''9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.   ''

 Ndugu Zangu, Huu Ni Mwaka Wa Kutubu Na Kuiamini Injili Ya BWANA YESU Maana Ufalme Wa MUNGU Umekaribia.
Marko 1:14-15 ''.....  YESU akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya MUNGU, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.   ''

MUNGU Akubariki Na ROHO MTAKATIFU Akufikishe Kwenye Toba Sahihi Na Ya Kweli

 -Itamfaidi nini mtu akiupata ulimwengu wote na mali zote na umaarufu wote harafu akifa aende motoni?
Kumbe dawa ni kutubu tu na kuishi maisha mataktifu ayatakayo BWANA YESU.
Hakuna uzima nje na BWANA YESU.
Ndugu zangu, kuna hukumu ya kutisha, hukumu hiyo itamhusu kila mwanadamu anayeishi leo na yule aliyeishi zamani.
BWANA YESU ndiye atakayehukumu siku ile. Ni heri kumpokea leo na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Biblia inasema 
'' Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake-Ufunuo 20:10-13'' 
-Kuanzia shetani ataadhibiwa milele, kisha watafuata wale aliowadanganya na wakamkataa YESU nao wataadhibiwa.
-Waliokataa kuishi maisha mataktifu kama Biblia inavyotaka nao wataadhibiwa.
-Watenda dhambi wote wataadhibiwa.
-Itakuwa ni hatari kwa wanaoukataa wokovu wa BWANA YESU leo na kukataa kuishi kama neno la MUNGU linavyotaka.
Nakuomba ndugu, tubu, geuka na anza kumtii BWANA katika yote.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments