KITABU CHA UFUNUO NI MUHIMU SANA KWA KILA MTU KUKIJUA.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu ujifunze ufahamu mzuri wa uzima.
Leo nazungumzia kitabu cha mwisho katika Biblia kinachoitwa ufunuo, natoa dondoo tu chache ambazo zitakusaidia sana.
Ufunuo 1:3 '' Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.'' 

Kitabu Cha Ufunuo Hakifundishwi Sana Katika Baadhi Ya Majengo ya ibada  Kwa Sababu Kiko Wazi Sana Kuwaonya Wanadamu. Kitabu Cha Ufunuo Kinatoa Siri Za Ajabu Sana.

=Kinatoa Na Kufafanua Yote Yaliyokuwa Yamebaki Kuandikwa na kinafafanua katika kuonyesha mwisho wa mambo ambayo yaliandikwa zamani na manabii wa MUNGU. Mtume Yohana katika kitabu cha Ufunuo aliambiwa aandike aliyoyaona, yaliyopo na yatakayokuja baada ya hayo.
Ufunuo 1:19 ''  Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo. ''

=Kina Siri Za Ajabu Sana, Kinasema Kwamba Kuna Wanadamu Wanamsujudia Mnyama Kutoka Kuzimu Wakidhani Ni MUNGU Wa Mbinguni. ni dhambi hiyo na kama watauelewa ujumbe huu basi watubu na kumpokea BWANA YESU maana mnyama wa kuzimu anawadanganya ili awapeleke motoni.
Biblia inasema kuhusu uongo wa shetani wa kutuma roho ya kuzimu ambayo wanadamu wataiabudu na sasa kuna maelfu wanaiabudu huku wakidhani wanamwabudu MUNGU wa mbinguni kumbe wanamwabudu shetani bila kujijua.
Ufunuo 13:4-9 '' Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane MUNGU, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Mtu akiwa na sikio na asikie. ''
-Kuna watu humwita mungu wa mwenyezi mungu au mungu mwenyezi lakini kumbe wala sie MUNGU aliyeumba mbinguni na nchi.
-Kuna watu humwabudu mungu wao na kumsifia kila siku kumbe wanaabudu mnyama toka kuzimu wala sio MUNGU wa mbinguni.
-MUNGU wa kweli na anayestahili kuabudiwa anapatikana katika KRISTO YESU pekee, nje na hapo ni kuabudu mnyama. Biblia hapo juu imesema kwamba wale ambao majina yao hayapo katika kitabu cha uzima cha YESU KRISTO hao humtii mnyama bila wao kujijua.
-Mnyama ambaye ni mungu kamili kwa baadhi ya watu atanena makufuru na kwa sababu yeye haonekani basi wanaomtii ndio watakaoongea makufuru kwa BABA wa mbinguni.
-Mnyama huyo yuko kivita zaidi na vita hiyo haifanyi yeye ila wanaifanya hao wanaomtii.
-Kuna watu huua watu na kudhani kwamba wanampendeza MUNGU wa mbinguni kumbe wanampendeza mungu wao ambaye ni mnyama toka kuzimu na ukimpendeza mnyama huyo maana yake umempendeza shetani. ukimwabudu mnyama huyo toka kuzimu maana yake umemwabudu joka aliyemtuma huyo mnyama.
Kitabu cha ufunuo kina siri za ajabu sana na ni kitabu muhimu sana kujua maana kinazungumza yaliyopo, yatakayokuja baada ya haya na yatakayokuja baada ya siku ya mwisho.
-Mwenye sikio na asikie.

=Ufunuo Kinasema Kwamba Kuna Watu Wanasujudia Sanamu Na Kudhani Wanampendeza MUNGU. Kuna mnyama mwingine atatoka kuzimu na kuja kuwafanya watu watengeneze sanamu na kuzisujudia.
Ufunuo 13:15-17 ''Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.''

=Ufunuo Kinafafanua Kuhusu Mwisho Wa Mashetani Na Shetani Mwenyewe.
Ufunuo 19:20 '' Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;''
-Nabii wa uongo ni yule aliyewatoa watu kwa BWANA YESU na kuwahamishia kwa mnyama, huyu atatupwa siku ile ndani ya ziwa la moto.
-Nabii wa uongo ni yule aliyewafundisha wanadamu kusujudia sanamu na kuwakosesha uzima. huyu atatupwa ziwa la moto.
-Nabii wa uongo ni yule anayewafanya wanadamu waipokee chapa ya mnyama katika nyuso zao, huyu atatupwa katika ziwa la moto.
Hata shetani mwenyewe ambao maelfu wanamwabudu sasa siku hiyo atatupwa jehanamu.
Ufunuo 20:10 ''  Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. '' 

 =Ufunuo Kinasema Juu Ya Watu Wanaoleta Mafundisho Ya Uongo Na Kuwakosesha Wengine. 
Ufunuo 2:20 '' Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. '' 
-Hakuna roho chafu kama ya yezebeli, roho hii inawakosesha maelfu wa watu. ukiona nywele bandia, kucha bandia,wanja, rangi za kucha na mengine mengi basi tambua kwamba Yezebeli  yuko kazini. Siku moja BWANA YESU akinipa kibali nitafundisha tu juu ya roho ya yezebeli, pia siku moja nitafundisha mafundisho ya wanikolai ni mafundisho gani(Ufunuo 2:15), Pia kama kibali kitapatikana siku moja nitafundisha, pia siku moja kama nikipata kibali nitafundisha mafundisho ya balaamu ni mafundisho gani(Ufunuo 2:14)

=Ufunuo Kinaeleza Juu Ya Mwisho Wa Mawakala Wa Shetani Na Wanaomtumikia Shetani.
Ufunuo 20:12-13 ''  Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. '' 

-Ndugu, nafasi ya wewe kuandikwa katika hicho kitabu cha uzima ipo leo. jambo la kufanya mpokee YESU kama BWANA na MWOKOZI wako kisha anza kuishi kama neno la MUNGU Biblia itakavyo, ishi maisha ya wokovu na hakika utashinda.



 =Ufunuo Inawataka Waabuduo Halisi Kusonga Mbele Na BWANA YESU. 
Ufunuo 20:4-6 '' Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa YESU, na kwa ajili ya neno la MUNGU, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na KRISTO miaka elfu. Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.  Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa MUNGU na wa KRISTO, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu. ''
-Hii miaka 1000 ya kutawala na KRISTO ni mwanzo tu ya uzima wa milele maana miaka hiyo 1000, na katika miaka hiyo 1000 kuna mambo yatakuwa yanaendelea ambayo sitayazungumzia leo maana leo nadonoa tu. 

=Ufunuo Inazungumzia Mbingu Mpya. 
Ufunuo 21:1-4 '' Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa MUNGU, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya MUNGU ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye MUNGU mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.''
-Waliotakaswa kwa damu ya YESU KRISTO pekee ndio watakaoingia katika mbingu  mpya, watakatifu wasio na mawaa tu ndio wataingia. 

=Ufunuo Inazungumzia Madhara Ya Dhambi. 
Ufunuo 22:14-15 ''Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.'' 

-Huko nje maana yake huko jehanamu ndio kutakuwa na watenda dhmabi. ndugu unayo nafasi ya kutubu leo kwa BWANA YESU na utafutiwa dhambi zako zote na jina lako litaandikwa kwenye kitabu cha uzima kisha jiunge na kanisa la kiroho wanaoihubiri kweli ya MUNGU na anza kujifunza neno la MUNGU na washirika wengine huku ukiishi maisha  matakatifu.

=Ufunuo Inamzungumzia BWANA YESU Mwenye Mamlaka Yote. 
Ufunuo 5:5-14 '' Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia MUNGU kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa MUNGU wetu; nao wanamiliki juu ya nchi. Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele. Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu. '' 
-Malaika wote humsujudia BWANA YESU.
-Wazee 24 na wenye uhai 4 humsujudia BWANA YESU.
BWANA YESU ni MUNGU mwenye nguvu sana.

Wanaohubiri Makanisani Kwao Mahubiri Ya Tamaa Na Matamanio Yao Huku BWANA YESU Wamemuacha Hao Hawajui Na Hawajaielewa Ufunuo. 

Ndugu yangu, Shika Ulichonacho Asije Mwingine Akachukua.
Ufunuo 3:11 BWANA YESU anasema '' Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.'' 
-Mteule shika sana wokovu asije mtu akakuondoa kwa YESU na ukakosa uzima.

 Musa Aliandika Vitabu 5 Vya Mwanzo Vya Uumbaji Wa MUNGU Na Mtume Yohana Aliandika Vitabu 5 Kikiwemo Kitabu Cha Ufunuo Ambacho Kimeandika Mambo Ya Mwisho Wa Dunia. Mambo Mengi Yanafanana Katika Watumishi Hawa Wawili. Kubwa Zaidi Wote Waliambiwa "PANDA JUU" Angalia Kutoka 19:20 Na Ufunuo 4:1. 
-Musa Alipanda Juu Kwenda Mlima Sinai Katika Mwili Lakini Yohana Alipanda Mbinguni Akiwa Katika Roho. 
KUPANDA JUU Ni Kukua Kiroho. 
 -Pia Watakatifu Lazima Wapande Juu Kabla Ya Dhiki Kuu. 
-Dhiki Kuu Haitakuja Hadi Watakatifu Wawe Wamepanda Juu Mbinguni. 
-Kitabu Cha Ufunuo Kimekusanya Mambo Ambayo Yalikuwa Hayajafunuliwa Mwanzo. 
-Kumbe Yaliyobaki Tangu Mwanzo Yaliandikwa Katika Kitabu Cha Ufunuo. 
Ndugu zangu, MUNGU Hakutuweka Kwa Hasira Yake ila tujitahidi kuingia katika ufalme wa Mwana wa pendo lake YESU KRISTO mwokozi wetu.

Ufunuo 22:16 ''Mimi YESU nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.   ''
 Ndugu zangu,Tuko Kwenye Wakati Wa Neema Au Wakati Wa Kanisa, Ni Wakati Wa Kumpokea YESU Kwa Uhiari Bila Kulazimishwa, Neema Ikiisha Ni Hatari. 
Tuna Uhiari Wa Kuchagua Uzima Au Jehanamu Lakini Ni Heri Kuchagua Uzima Kwa Kuokoka Leo. Ndugu Itumie Vizuri Neema Ya MUNGU Kwa Kumpokea YESU.
Ufunuo 22:12,13,20,21 '' Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, BWANA YESU. Neema ya BWANA YESU na iwe pamoja nanyi nyote. Amina. '' 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments