KWA NINI MNAMTAFUTA ALIYE HAI KATIKA WAFU?


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze siku ya leo nzuri ipendezayo.

 
Luka 24:3-5 ''  Wakaingia, wasiuone mwili wa BWANA YESU.  Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta;nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?  ''
-YESU hamuwezi tena kumtafuta kwa wafu.
-wafu ni wale walioanzisha dini lakini wakafa na kubaki kaburini hadi leo, Wala usijisumbue kumtafuta YESU huko kwa wafu.
-Wafu ni wale waliojiita Kristo na kudanganya wengi kwamba watafufuka lakini hawakufufuka na hadi leo bado wako kaburini, usithubutu kumtafuta YESU KRISTO huko.
-Wafu ni wale waliofundisha watu wao kuabudu sanamu na kudhani wakifa wataenda mbinguni, BWANA YESU hahusiki na hao.

-Wafu ni wale manabii wa uongo waliowaongoza maelfu ya watu na kuwaambia wakifa watapaa kwa gari kwenda mbinguni kumbe wako kaburini hata leo, YESU usithubutu kumtafuta huko.

Kwanini YESU hayuko kwa wafu yaani hayuko kaburini kama wengine wote walioumbwa?
Mathayo 28:5-10 '' Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta YESU aliyesulibiwa.Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa. Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia.
Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari. Na tazama, YESU akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.
Kisha YESU akawaambia, Msiogope; enendeni, mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona.  ''

-Taarifa za kufufuka kwa BWANA YESU zilitolewa na mbingu, Malaika walitoa taarifa hiyo muhimu.
-Njiani wakakutana na BWANA YESU Wakamsujudia.
Ndugu yangu kama huwa unasujudia midoli, sanamu, jiwe na miti mikubwa basi nakushauri kuanzia leo anza kumsujudia BWANA YESU Maana yeye yu hai milele.
Mawe, sanamu, midoli na miti ni wafu lakini YESU hapatikani kwa Wafu amefufuka kama alivyosema.

Ni mapema tu BWANA YESU alisema
''Lakini YESU akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao. Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. .-Mathayo 8:22-23''
-Viongozi wa dini wanaomkataa YESU hao ni wafu na kwa kuwafundisha uongo waumini wao basi wanawazika. Hao ni wafu wanazikana wao kwa wao kwa kuambiana uongo juu ya mbingu.
Hakuna uzima wa milele nje na BWANA YESU.
Ni heri kumshika YESU na kuingia chomboni mwako yaani kuingia katika Wokovu wake.
Hapo juu tunaona BWANA YESU akiwaambia wanaoutaka uzima wa milele wamfuata baada wapingakristo ni wafu na wanazika wafu wenzao kwa kuwafundhisha  kuabudu Mnyama kutoka kuzimu huku wakidhani ni MUNGU wa mbinguni.
Ufunuo 13:4-9 '' Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
Akafunua kinywa chake amtukane MUNGU, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo(YESU), aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
 Mtu akiwa na sikio na asikie. ''

-Ndugu, mimi nimekueleza ukweli ili kuanzia leo uanze Kumwabudu MUNGU aliye hai.
-Msujudie BWANA YESU na sio joka wala mnyama huku ukidhani ni MUNGU wa mbinguni.
Joka na mnyama wa kuzimu ni wafu maana BWANA YESU atawatupa jehanamu. Sasa kama MUNGU wako ataadhibiwa na BWANA YESU, wewe je?
Hakuna ujanja ila ni kumkimbilia tu BWANA YESU katika haki yake.
BWANA YESU alikuja, anaokoa ukimfuata leo na siku ya Mwisho atarudi na hapo ndipo waliomkataa ka kukataa neno lake wataadhibiwa milele.
Isaya 66:15-16 ''Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Kwa maana BWANA atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi. ''
-Wakaouawa kwa kupelekwa jehanamu milele ni wengi sana maana walimkataa.
Ndugu, Mkimbilie BWANA YESU leo kabla ya kuondoka duniani.
Usipotubu matendo yako yatakufuata, lakini ukitubu matendo yako yansamehewa na kufuta.
Ndugu amka kutoka kwenye usingizi wa dhambi na njoo kwa BWANA YESU kwenye uzima wa milele.
BWANA YESU anakuita leo na usipokbali basi siku ukifa na siku ya mwisho atasema neno hili.
Isaya 66:4 '' Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu nilipoita, hawakuitika; na niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua nisiyoyafurahia. ''
-BWANA alipokuita hukuitika, alipokuita lini? ni leo ndugu ndio YESU B anakuita ili utubu na kuancha dhambi zako na kumpokea yeye kama BWANA na Mkombozi wako.
Jehanamu ni kwa wafu na kuzimu ni kwa wafu, usije thubutu kutafuta YESU huko kwa wafu maana hayuko.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments