MAELEKEZO YA KISHETANI


Na Mchungaji Bryson Lema, Ufufuo na uzima Morogoro.
Utangulizi: Shetani anao uwezo wa kuingia ndani ya mtu kama ‘maelekezo’. Ukumbuke kuwa Mwanadamu ana akili,  lakini mwandamu siyo akili.  Sasa mwanadamu  ni  kitu gani?
Mwanadamu ni roho yenye nafsi, inayokaa katika nyumba na hiyo nyumba inaitwa mwili. Mwanadamu Anazo sehemu kuu tatu: nafsi, mwili na roho. Pia taarifa za mbalimbali za huyu mwandamu zinahifadhiwa ndani ya moyo (siyo huu wa moyo nyama,  lahasha‼). Kila taarifa ninayoiona au kuisikia hukaa moyoni.
Shetani anafahamu  kuwa hawezi kukamata kwa kukutia tu pepo, bali hukukamata kwa kukuingizia taarifa. Yesu alisema,  manaeno niwaambiayo ni roho, tena ni  uzima”. Ina maana maneno ya Yesu Krsito yamebeba roho ya uzima. Kuna roho inaingia ndani ya mtu, kwa jinsi anavyokuwa anakaa na wenzake na kusikiliza maneno yao. Inategemea maneno hayo ni ya kimungu au  ya kishetani.

1 NYAKATI 21:1… [Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.]… Daudi aliletewa taarifa na shetani naye akakubaliana naye, huku akijua Mungu alishakataza Israeli kuhesabiwa. Kwa nini Daudi ahesabu watu wake? Ni kwa sababu alikuwa akishinda kataika kila vita aliyopigana, akadhani ushiindi wake unatokana na ukubwa wa jeshi alilo nalo. Kinachomfanya Daudi amkosee Mungu ni ile taarifa iliyoingia moyoni  mwake. Shetani anao uwezo wa kumpumbaza mwanadamu.
 
MATHAYO 13:15…[Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.]…Ndiyo  maana wapo watu ingawa hawapendi kufanya uovu,  lakini kutokana na taarifa walizojaza mioyoni  mwao,basi hutenda uovu.

2KORINTHO 4:4..[].. Mioyo ya watu inakuwa inefungwa ili  wasiamini.

WARUMI 1:21…[kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.]…Shetani anajua kwenye  moyo wako, ndiyo kitovu cha kukupatia taarifa.

MATENDO 28:27…[Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia,  Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya.]….
Ushindi wa mwanadamu upo  moyoni. Yafaa ujifunze ni nani umsikilize  na nani usimsikilize. Kila unachosikiliza ni  roho, na unapobaki peke yako yale maneno yanaanza kukusemesha. Maneno ya kuzimu yakeshaingia ndani  yako, yanaweza kukupeleka usipotaka.
Moyo  wa mwanadamu ni kama sumaku. Kinachomfanya mtu awepo kanisani na siyo disko ni kwa sababu mtunhuyo hana taarifa za disko. Haiwezekani kusikiliza nyimbo za Bongo flavor tokea asubuhi halafu  unatarajia uwe mchungaji wa kanisani. Taarifa ndiyo  maarifa, pasipo taarifa hakuna maarifa.
Ukimuona mtu  aliyefanikiwa, ni kwa sababu alitumia taarifa iliyokuwepo moyoni mwake.
JOSHUA 14:17…[Mimi nilikuwa mtu wa miaka arobaini umri wangu, hapo Musa mtumishi wa Bwana aliponituma niende kutoka Kadeshbarnea ili kuipeleleza hiyo nchi; nami nilimletea habari tena, kama ilivyokuwa ndani ya moyo wangu.]…. Haya ni maneno ya Kalebu, akikumbushia kuwa alitoa taarifa sawasawa na moyo wake. Maana yake nikuwa, pamoja na kuyaona yale majitu,  lakini hayakumtisha bali taarifa zao  hakuziweka moyoni mwake, bali aliazimia kuiweka taarifa ya Mungu Baba aliyewavusha toka Misri kupitia Bahari ya Shamu. Taarifa unayoiweka ndani  ya moyo  wako,yaweza kukufanya uingie Kanaani au la. Ndiyo  maana Daudi alisema, “Bwana nimeliweka neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi”.
Hayupo wa kukuzuia kwa sababu Yesu ni  kila kitu katika vyote. Silaha kubwa ya shetani ni hofu. Je, wewe umeweka taarifa gani moyoni  mwako?  Tunaye Mungu aliye mkuu kuliko miungu yote.  Ufufuo na Uzima ni Yesu mwenyewe. Muweke Mungu  Mkuu katika moyo wako. Huyu ni  Yule aliyewingia katika msiba wenye huzuni akabadilisha taarifa yao ya msiba ikawa taarifa ya furaha. Hayupo mtu wa kuizuia Ufufuo na Uzima hapa duniani, kwa sababu Ufufuo na Uzima ni Yesu mwenyewe. Taarifa nzuri ni  za Yesu Kristo. Kalebu akamwambia Joshua,  sikuaangalia yale  majitu, bali nilitoa taarifa kulingana na moyo wangu”.
Neno la Mungu ni taa ya miguu yako.ukiona inafikia mahali  unakata tama, unakuwa na wasi wasi, na maswali ya aina hiyo ujue moyoni mwako kuna kitu  ambachohakipo. Kila vita inapoinuka,  Mungu huibeba silaha iliyoko moyoni mwako ili kukushindia. Vita unayotaka uipiga inategemeasilaha ulizo nazomoyoni mwako. Wakatiwa amani,nsiyo wakati wa kutengeneza silaha. Wakati wa vita ni wa kuchukua silaha ulizo nazo ghalani na kuzitumia. Badhi ya Wakristo hupigiga simu wachungaji wakitaka maombi nyakati zile mambo yanapowakwamia.
EFESO 6:11…[Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.]…. Kuna siku ya uovu, ambayo mashetani wanakuwa wameweka kituo, kuwa leo ni kawa ajili ya ndoa ya mtu  fulanii. Hiyo ndiyo siku ya uovu. Inabidi ufahamu kuwa, shetani  anakufuatilia usiku na mchana.  Nchi na nchi zinapopigana,majeshi yao huanza kwa kushambulia maghala ya silaha. Ili adui asikushinde, weka vizuri ghala lakola  silaha moyoni mwako. Usisubiri vita iibuke kazinimwakoau katika ndoa yako. Maneno ya Mungu mkuu yawepo mioyoni mwetu. Weka silaha ya moto ndani ya moyo wako,  achana na silaha ya mwaka jana ambayo tayari ina kutu.
Wokovu tulio nao siyo wa mazoea. Samsoni alijidanganya, hata baada ya kunyolewa,aliendelea kudhani kuwa nguvu zake zitamrudia kwa kujinyoosha tu. Mbinu anazotumia shetani ni  mpya  kila siku. Yale  ya jana hayatakusaidia leo, kwa sababu leo ni siku mpya na ya tofauti. Kuna tofauti ya chakula cha jana kilicho kwenye frijina chakula kilichoivishwa leo. Silaha iliyopo  moyoni,ukiweza kuinoa vizuri, inakuwa na makali yale yale.
Njia nzuri ya kuweza kuwa na silaha moyoni mwako ni yaw ewe kuokoka na kumkabidhi Yesu Kristo maisha yako.

                          © Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)

Mtaa wa Nguvu Kazi, (Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.

 /or

Contact our Senior Pastor:

 Dr. Godson Issa Zacharia

 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)

Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778

Comments