MAMBO YANAYOWEZA KUKUTENGENEZEA MAZINGIRA YA KUFANYA MAAMUZI YATAKAYOLETA MAFANIKIO.

Bwana Yesu Asifiwe.
Mambo yanayoweza kukutengenezea mazingira ya kufanya maamuzi yatakayokuletea mafanikio.

-Jihadhari na wale wanaokuzunguka ambao maisha yao hayana matunda mazuri, wasikunyang'anye uwezo wako wa kuamua. Zaburi 1:1 inasema: "Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa wenye mizaha"


 -Jihadhari na wale wanaochochea utekeleze mawazo mabaya yaliyo ndani yako au yaliyo ndani yao. Mithali 1:10 inasema: Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi,wewe usikubali." Usije ukawa kama Amnoni aliyembaka dada yake Tamari kwa ushauri wa rafiki yake aliyeitwa Yonadabu(2 Samweli 13:1-20)

-Jizoeze kuuliza ushauri kwa Mungu kabla ya kufanya maamuzi, kama Daudi alivyofanya katika 1 Samweli 30:8. " Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! nikiwafuata jeshi hili,nitawapata? Naye(Bwana) akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote"

 -Jifunze kuitambua amani ya Mungu au amani ya Kristo ndani ya moyo wako,maana ni njia mojawapo anayotumia Roho Mtakatifu kukuongoza kufanya maamuzi mazuri.
"Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu"(Wafilipi 4:6,7)

Comments