MAOMBI YA LEO TUNAITA USHINDI KUPITIA JINA LA YESU KRISTO.

BWANA YESU asifiwe.
 '' Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;-Mathayo 7:7'' 
Kama muombaji unayehitaji matokeo mazuri baada ya maombi yako lazima uombe kwa imani huku ukiwa mtakatifu. Haya ni maombi ya vita ambayo kama kikundi cha maombi tukikuwa tunaomba usiku. Unaweza ukaona na kujifunza kuombea baadhi ya maeneo ambayo unadhani yanahitaji msaada wa BWANA YESU. Sio lazima uombe maombi kama sisi ila naamini MUNGU ataweka nyongeza yako ambayo ndiyo inayohitajika sana ili kupokea majibu yako mazuri ubarikiwe.

 ''ombeni bila kukoma;1 Thesalonike 5:17''


Leo tunaomba maombi ya kupokea kutoka kwa MUNGU.
MUNGU hajipingi na neno lake hivyo tuombe sawa sawa na mapenzi yake.
Tena tuombe kwa imani kupitia jina la YESU KRISTO.
Leo tunaomba tukitumia Zaburi 20"1-9. Biblia inasema

'' BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la MUNGU wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la MUNGU wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote. Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu. Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, MUNGU wetu.Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.
BWANA, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.''

-Omba kwa kinywa cha mamlaka ukitumia maandiko hayo.
Mwambie BWANA YESU aiondoe dhiki ambayo inakuandama, kwa jina la YESU KRISTO zikatae dhiki zote.
Kwa jina la YESU KRISTO kataa dhiki za magonjwa na madeni, kataa ajari na mabalaa yote.
Mwambia MUNGU azikumbuke sadaka zako, na kwa damu ya YESU akufute kila neno baya ulilotamkiwa na wanadamu.
Damu ya YESU iite ili ifute kila laana uliyotamkiwa.
Kama wengine wanataka waganga wao wa kienyeji wewe litaje jina la YESU KRISTO na utawashinda. wakija kukuroga na kukunenea mabaya liite jina la YESU KRISTO la msaada.
BWANA akukumbuke kutoka mbingu zake takatifu.
Wewe mteule wa KRISTO ni masihi wa MUNGU na hakikisha unamwambia BWANA akuokoe wewe mtumishi wake.
Omba na ushindi ni lazima kupitia jina la YESU KRISTO.
Mimi nakuombea nguvu na BWANA akukumbuke kupitia maombi yako leo.



Waambieni Wenye Haki Ya Kuwa Watakuwa Heri, Kwa Maana Watakula Matunda Ya Matendo Yao-Isaya 3:10.

Iko nguvu katika kumkaribia MUNGU.
* Kuna nguvu ya uponyaji katika kumkaribia MUNGU.
* Kuna maisha ya ushindi katika kumkaribia MUNGU.
* Kuna nguvu ya ukombozi katika kumkaribia BWANA.
* Kuna nguvu ya kumshinda adui yako katika kumkaribia MUNGU.
* Kuna ukuaji wa kiroho katika kumkaribia MUNGU.
* Kuna kuinuliwa katika kumkaribia MUNGU.
* Kuna kuongezeka kiwango cha imani katika kumkaribia MUNGU.
* Kuna nguvu ya ufunuo katika kumkaribia MUNGU.
* Nguvu ya kukutoa hapo ulipo kwenda mahali pengine/hatua nyingine Ipo katika kumkaribia MUNGU.
* Huwezi kumpendeza MUNGU usipomkaribia MUNGU Kwa maombi kupitia jina la YESU KRISTO tena kwa imani.
* Uponyaji wa mioyo/nafsi zilizoumizwa upo katika kumkaribia MUNGU.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments