MAOMBI YA NGUVU YENYE USHINDI



 BWANA YESU asifiwe.
 '' Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;-Mathayo 7:7'' 
 Kama muombaji unayehitaji matokeo mazuri baada ya maombi yako lazima uombe kwa imani huku ukiwa mtakatifu.
 Haya ni maombi ya vita ambayo kama kikundi cha maombi tulikuwa tunaomba usiku. Unaweza ukaona na kujifunza kuombea baadhi ya maeneo ambayo unadhani yanahitaji msaada wa BWANA YESU. 
Sio lazima uombe maombi kama sisi ila naamini MUNGU ataweka nyongeza yako ambayo ndiyo inayohitajika sana ili kupokea majibu yako mazuri ubarikiwe. 

''Ombeni bila kukoma;1 Thesalonike 5:17''

 Maombi ya siku ya kwanza.

BWANA YESU asifiwe.
Leo tunaomba mambo 7 kutoka katika Zaburi 23 Biblia inasema

'' BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.  Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele. ''


=Omba BWANA YESU awe Mchungaji wako wa kukuongoza hadi uzima wa milele.

=Omba ukidai ahadi njema ya MUNGU kwamba usipungukiwe kiuchumi, ita utoshelevu wa MUNGU katika kipato chako.
=Omba ukimwambia ROHO MTAKATIFU ahuishe roho yako yaani aifanye upya iliyo kwa jinsi ya KRISTO.
=omba maombi ya kuita haki ya MUNGU, MUNGU akupe haki popote ulipo, wanaowaza mabaya hawatafanikiwa kwako maana wewe una kibali cha haki cha BWANA YESU.
=Hata kama kuna magumu mbele yako mwite BWANA YESU akushindie. Tumia gombo la MUNGU ambalo ni Neno lake kujiweka huru.
Tumia fimbo uliyopewa ambayo ni Mamlaka ya KRISTO iliyoko ndani yako. Tumia mamlaka na neno kuharibu kila adui yako , kila upinzani na kila mitego . Tumia jina la YESU KRISTO katika maombi yako.

=Omba BWANA YESU akupake mafuta ya ushindi, mafuta ya ROHO ni kibali cha kiungu cha ushindi mkuu. ita ushindi na kikombe chako kifulike baraka za kila aina.
=Mshukuru MUNGU BABA kwa fadhili na wema wake kwako,
mshukuru MUNGU kwa kuklinda na kukupa baraka kuu. kisha Mshukuru MUNGU kwa uzima wa milele ambao uko katika KRISTO YESU pekee. Mwambie BWANA YESU akupe uzima. magonjwa na balaa yasikupate.

Hakika wewe ni mshindi kwa jina la YESU KRISTO.
Omba na BWANA YESU yuko tayari kukutendea muujiza mkuu.
BWANA YESU akubariki na kukushindia.
amen amen.


Siku iliyofuata maombi yake yalikuwa hivi.

BWANA YESU asifiwe.
Leo tunaomba tukiharibu magonjwa yote.
Zaburi 103:3-6 '' ''Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai; BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa.''

 
omba ukidai ahadi hii ya MUNGU kwako, kataa magonjwa yote. ponda majini yote ambayo hujigeuza ugonjwa na kuingia katika miili ya watu.
Ita jina la YESU la uponyaji.
haribu magonjwa ambayo bado hayajaonekana kwako ila mipango ya shetani ya kuyaleta inaendelea kwenye ulimwengu wa roho.
Magonjwa ya kutegwa yateketeze.
Magonjwa ya kurushiwa yaharibu kwa damu ya YESU KRISTO.
Magonjwa yasiyotibika hospital yateketeze kwa damu ya YESU ambayo haijawahi kushinwa.
Omba ndugu na mimi nakuombea nguvu na ushindi.
Ubarikiwe.


 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments