MCHUNGAJI PETER MITIMINGI:NIMETEMBELEWA NA WACHAWI!

Na Mchungaji Peter Mitimingi, Huduma ya The Voice Of Hope Ministry.

Nipo hapa hotelini kwa siku mbili usiu wa jana na juzi nimekuwa nikitembelewa na wachawi usiku na nimekuwa nikipambana nao na mwishowe wanakimbia lakini baada ya masaa kadhaa ya mapambano.
Usiku wa kuamkia leo ndio yalikuwamapambano makali sana. Nimelala alfajiri. Nilipoamka asubuhi Mungu akanionyesha kwamba kwenye kitanda nilicholalia kilifanyiwa mikataba ya kichawi. Nikakishika na kuanza kukiombea na kuvunja nguvu za giza. Baada ya hapo nikajiandaa nikaondoka kwenda kwenye shughuli zilizonileta hapa.

Asubuhi mwenye hoteli akaja kitu ambacho sio kawaida yake kuja asubuhi. Akauliza nani analala chumba nanmba fulani? wafanyakazi wakamwambia. Nikajisikia kurudi tena hotelini nikaingia chumbani kwangu nikakuta wahudumu wameshasafisha chumba na kutandika kitanda vizuri. Mara mwenye hoteli akaja akasema samahani tunabadilisha kitanda. Akawaleta vijana wake wakafungua kile kitanda wakaleta kitanda kingine wakakifunga wakakichukua kile kitanda chenya mikataba. Hichi nacho nimesha kipiga pawa ndio nitakilalia usiku wa leo.
Wafanyakazi wananiambia mwenyewe anatamani uhame hoteli ila ndio nimetua hapa haondoki mtu.
TUNALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU KWANJIA YA IMANI!

Comments