MNAOTOA MIMBA SIKILIZENI

Na Godfrey Miyonjo.

Imeandikwa “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, kabla hujatoka tumboni nalikutakasa, nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” YEREMIA 1:5.
BWANA YESU asifiwe,
Mpendwa unapaswa kujua kuwa mimba zote zinajulikana mbele za Mungu.
Hivyo unapochukua uamzi wa kutoa mimba unapaswa kutambua kuwa wewe ni muuaji kama walivyo wauaji wengine.
Unapotoa mimba ujue kuwa umeamua kuivunja amri ya Mungu, Kwa maana imeandikwa “Usiue” KUTOKA 20:13.
Na kwakuwa wewe ni muasi, tambua kuwa waasi wote sehemu yao ni JEHANAM,
Na ili usiende JEHANAM unatakiwa kukutana na Yesu leo kabla haijaja siku ile ya kutisha.
Haijarishi hata kama unaitwa Mkristo lakini wewe ni mtoa mimba tambua kuwa wewe bado haujakutana na Yesu.
Kwa maana imeandikwa “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa maana dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo haimo ndani yake, kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona” 1YOH 3:4-6.
Waliokutana na Yesu hawatoi mimba, kwa maana wanajua kuwa kutoa mimba ni uuaji.
Ndiyomaana Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
MKIYAJUA HAYA HERI NINYI MKIYATENDA, WATOA MIMBA WOOTE, TUBUNI LEO MJISALIMISHE KWA YESU.

Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu)

Comments