MPANGO WA MUNGU SIO KUKUANGAMIZA ILA UTAJIANGAMIZA WEWE MWENYEWE KWA KUUKATAA MPANGO WA MUNGU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tena karibu sana tujifunze Neno la uzima.
Yeremia 29:11 ''Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.'' 
-Mawazo hayo ya MUNGU ya kukuwazia mema ndiyo yanayotenda kazi leo, yalisemwa zamani na utekelezaji wake ni nyakati ya leo.
-MUNGU ameachilia neema yake kuu na amekwisha kuuonyesha mpango wake mwema kwetu. ni jukumu letu kuufuata mpango wa MUNGU.
Ni muhimu kuujua mpango wa MUNGU juu ya maisha yako.
Kila Mwanadamu anatakiwa ajue kwamba kuna kuondoka na leo yetu ndio inayoamua kesho yetu.
Wanadamu Wakiujua Mpango Wa MUNGU Watauendea, Wakiuendea Mpango Wa MUNGU Maana Yake Wamemwendea MUNGU Maana Yeye MUNGU Yuko Katika Mpango Wake Akiusimamia. Wakifika Katika Mpango Wa MUNGU Yeye MUNGU Atasema "Tubuni Na Kuiamini Injili Maana Ufalme Wangu Umekaribia
Marko 1:14-15 '' Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, YESU akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya MUNGU, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.''.
-Kutubu ndio kumruhusu MUNGU ashughulike na wewe.
-Kutubu ndio Kumfanya MUNGU aanze kukuandalia makao mazuri ya Milele. 
-Kutubu na kumpokea BWANA YESU ndio kuujua mpango wa MUNGU na kuuendea.

Wanadamu Wakitubu Na Kumpokea YESU KRISTO, MUNGU Ataanza Kuwatawala na Watapata Uzima Wa Milele kama wakidumu katika mpango huo wa MUNGU.
Yohana 1:12-13 '' Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.''. 
- Kumbe Kuujua Mpango Wa MUNGU Ni Kuujua Uzima, Mpango Wa MUNGU Ni KRISTO
Warumi 10:13 '' kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. ''.
 -Ukiujua Mpango Wa MUNGU Utaufuata Na Ukiufuata Utapata Uzima. 
-Mpango MUNGU Wa Uzima Ni Mmoja Tu.
-Ukiukataa Mpango Huo Maana Yake Umekataa Uzima Wa Milele, -Ukijitenga Na Mpango Wa MUNGU Maana Yake Umejitenga Na Uzima. 
Ndugu Yangu, Kwanini Ujitenge Na Uzima Kwa Kuukataa Mpango Wa MUNGU? . 
Ndugu Upokee Mpango Wa MUNGU Wa Uzima Wako.
Siku ya hukumu itakuwa nzuri kwa wateule wa KRISTO walioishi kama neno lake linavyosema, lakini siku hiyo itakuwa mbaya kwa waliomkataa YESU na kuendelea na dhambi zao.
Biblia inasema hivi kuhusu siku hiyo ya mwisho.
Ufunuo 20:11-13 '' Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.   ''

 Ndugu, wakati wa kuitengeneza siku hiyo ya mwisho ili uwe baraka kwako ni leo. lakini matendo yako mabaya ya leo ndiyo yanaweza kuifanya siku hiyo ya mwisho ikawa mbaya.
-Watu Wengi Huyafanya Makubwa Kuwa Madogo Hata Sijui Kwanini. Kumpokea YESU Na Kuokoka Ni Jambo Kubwa Sana Maana Jina Lako Linaandikwa Mbinguni Na Hata Ukifa Kwenye Wokovu Huo Unaenda Uzimani. 
Lakini Jambo Hili Kubwa Kuna Watu Huliona Dogo Sana Na Yale Madogo Wao Ndio Huyaona Makubwa. 
Unaweza Ukawahubiri Watu Hadi Ukatoa Machozi Ili Tu Wampokee YESU Na Kuiepuka Jehanamu Lakini Watu Hao Wanaweza Kukucheka Na Kukubinulia Midomo Kwa Dharau, Wao Wanaliona Tukio La Kukubinulia Midomo Kuwa Kubwa Kuliko Tukio La Kumpokea YESU. 
Mimi jukumu langu ni kukueleza ila mwamuzi ni wewe, Biblia inasema 
Ezekieli 3:18-21 '' Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako. Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Bali ukimwonya mwenye haki, kwamba yule mwenye haki asitende dhambi, tena ikiwa yeye hatendi dhambi, hakika ataishi, kwa sababu alikubali kuonywa; nawe umejiokoa roho yako. ''
-Mimi ni jukumu langu kuwaambia ndugu zangu wote wanaosoma hapa. 
Ndugu Zangu, Tusiyafanye Makubwa Kuwa Madogo. Hakuna Jambo Muhimu Kuliko Uzima, Ukiwa Na Afya Mgogoro Utajiskia Vibaya Sana Na Kutamani Uwe Mzima, Vipi Ukiwa Jehanamu Hutatamani Uzima Wa Milele? Hakika Utatamani Lakini Ukiambiwa Sasa Kuokoka Unaleta Kebehi Nyingi Na Wengine Hadi Hutukana. 
Ndugu, Ifanye Kesho Yako Iwe Uzima Wa Milele Kwa Kuokoka Leo. 
BWANA YESU Yu Karibu Na Hakika Siku Ya Mahesabu I Karibu Sana. 
 Ufunuo 22:12-13 ''  Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. ''

Ndugu, Usimwache BWANA YESU Akupite Bali Mpokee Na Atakuandika Jina Lako Uzimani.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments