MTEGO WA MWINDAJI


Mwili wako ni Hekalu la Mungu!
Na Mwl Conrad Conwell.
Zaburi:91:3’’Maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,..’’
Namshukuru MUNGU aliye nipa kibari cha kushiriki na wewe somo hili la MTEGO WA MWINDAJI, ambalo naamini linakwenda kukusogeza hatua nyingine kabisa katika imani yako.
KIKAWAIDA MTU UNAPO SEMA KWAMBA umeokoka yani umejiunga na uzao mteule wa mwanakondoo, MOJA KWA MOJA huwa unakuwa umetangaza uadui na UFALME WA GIZA.

Hivyo acha nikuite kuwa wewe ni mwana vita au mpiganaji au mpambanaji(ni mwanajeshi wa jeshi la mwana kondoo). WAEFESO:6:12 ‘’Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu na roho’’. HAPO UNAWEZA GUNDUA KITU KUMBE WEWE NI MTU wa mashindano LAKINI hayo mashindano hayapo juu ya DAMU na NYAMA, yapo katika ULIMWENGU wa roho, HIVYO kama mkristo ni muhimu uwe na uwelewa wa ULIMWENGU wa roho ili uweze KUPAPAMBANA vilivyo la sivyo UNAWEZA UKAPIGWA NA ADUI.
Sasa twende kwenye somo letu rasmi, MTEGO WA MWINDAJI: Hapa kwanza kabisa na mzungumzia MWINDAJI pamoja na mtego alio utega kwaajili ya anacho kiwinda(anaye windwa). Lakini pia tumwangalie na MWOKOZI(Anaye okoa) wa hii mitego iliyo tegwa na mwindaji.
Katika kufuatilia kwangu nimegundua ya kwamba TUNA WAKRISTO wengi makanisani wanaohudhulia ibada vizuri sana, na niwatoaji wazuri sana wa mafungu ya kumi, LAKINI WAKRISTO wengi wana fikiliaga kwamba kuitwa mkristo peke yake inatosha, WANASAHAU yakuwa adui(SHETANI) Huwa bado anaandaa mitego ya kuwatoa kwenye imani walizo nazo, 1PETRO:5:8 ‘’ Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.’’

Unaona sasa kumbe bado kuna mtu anatafutwa ili amezwe, sasa hapa unaona kutokana na mawindo ya SHETANI anafananishwa na SIMBA aungurumaye akitafuta mtu ammeze, hivyo yupo mawindoni, yeye hali swala, nyati wala punda milia, ndiyo utofauti ulipo hapa wa huyu mfano wa simba, yani yeye chakula chake ni watu tu. So anaweza akakumeza wewe au mimi TAKE CARE.
TUNA MZUNGUMZIA SHETANI kama mwindaji sasa, ambaye ametega mitego yakutosha kwa ajili yako, ili akurudishe nyuma kiimani, aivunje ndoa yako, akurudishe nyuma kiuchumi n.k

Labda acha nikupe kitu kidogo kinacho weza kukusaidia juu ya mwindaji. SHETANI mawindo yake hayakuanza leo, alianza tangu pale EDENI, alimuwinda ADAM kwa muda mrefu ili amtoe kwenye kusudi la MUNGU, na kuuharibu uhusiano uliopo kati ya ADAMU na MUNGU. Aliubadilisha UKWELI kuwa UONGO ili tu ADAMU aingie mtegoni, na kweli alifanikiwa katika hilo. Soma MWANZO:3
NOTE:SI KILA JAMBO LIJALO KAMA BARAKA, NI LAKULIKUMBATIA NA KULIONA LA FAA SANA; MAMBO MENGINE YAMEKUJA KAMA BARAKA KWETU LAKINI NI MTEGO HALISI WA MWINDAJI.
Nimeona watu wengi kutokana na hali ambazo wamekuwa wakizipitia katika maisha yao wamejikuta wakinaswa na mtego wa mwindaji, wengine ni kweli walisimama kiimani lakini walisahau ya kuwa bado walikuwa wanawindwa na mwisho wake ukawa nikuangukia katika mtego wa mwindaji.
NIOMBI LANGU KWA MUNGU AKAITEGUE MITEGO YOTE ILIYO TEGWA DHIDI YA KILA ENEO LINALO HUSU MAISHA YAKO KATIKA JINA LA YESU KRISTO ALIYE HAI.

Naomba nikukumbushe kitu mwana wa MUNGU, shetani hajakutega katika hii leo yako unayoiona ni ya baraka kwako au ni ya furaha kwako, LAKINI NAUONA mtego alioutega kwa ajili yako ni KWAAJILI YA KESHO yako, maana amekutazama akagundua kwamba wewe ni mtu watofauti sana, na mwenye impact(matokeo) kubwa sana kwa wakati ujao wa maisha yako, KWAHIYO NI MUHIMU KUJUA KWAMBA taabu unayoipata leo ni matiokeo ya mtego uliowahi kutegwa na ukategeka kwa wakati huo ulio pita.
HEBU tusogee mbele zaidi sasa. 1Samweli:18:21 ‘’ Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena mkono wa wafilisti uwe juu yake.’’
Hapa sasa unaweza kuona sasa kumbe kunawatu wana ndoa zilizo mitego kwao, Hapa utamwona SAULI anamwozesha binti yake kwa DAUDI si kwamba awe mke bali awe mtego kwa kwa DAUDI. Anhaa.. Kumbe MUWINDAJI anaweza akakuletea mume/mke ambaye ulikuwa ukimwomba MUNGU kwa muda mrefu, nawewe ukajipa moyo kwamba tayali MUNGU amejibu maombi yako, kuumbee ni MUWINDAJI amekuletea mfano wa mume/mke ili apate kukuingiza au kukunasa mtegoni, HATAKAMA UTASUBIRI KWA MUDA GANI JUA KWAMBA MUNGU NDIYE ATAKAYE KUPA MWENZA WAKO, JIANGALIE USIJE ANGUKIA MIKONONI MWA WANYANG’ANYI..

Comments