NAWE LEO TOA TAMKO JUU YA MAADUI ZAKO.

Na Geofrey Miyonjo

“BWANA YESU asifiwe sana.
Duniani imezoeleka kusikika watu mbalimbali wakitoa matamko ambayo huwa ni msimamo wao au ni msimamo wa makundi wanayoyawakilisha.
Tumewahi kusikia matamko ya wanasiasa, matamko ya magaidi, matamko ya wakuu wa dini, matamko ya wachawi, Matamko ya wapungapepo, N.K.
Matamko hayo wanayoyatoa huwa siyo bure bali huwa na maana kubwa katika ulimwengu wa damu na nyama na ulimwengu wa roho pia.
Kutokana na matamko hayo kuna mbambo hutokea katika ulimwengu wa damu na nyama na ule wa roho.
Kwa watu kutoa matamko tu watu hutetemeka na wakati mwingine hata kufa kwa hofu.
Kwa mfano, ikitokea Magaidi wakitoa tamko juu ya kuhatarisha amani sehemu flani, serikali huimalisha ulinzi sehemu hiyo, taadhari hutolewa kwa watu waishio eneo husika, N.K.
Haya ni matamko ambayo ni ya watu wasiomjua Mungu (wapagani), lakini yanawatetemesha wakuu, na watu wote.
Hayo hutokea kwasababu maneno yana nguvu sana, ndiyo maana biblia inasema mauti na uzima huwa katika uweza wa ulimi MITHALI 18:21.
Kwa maana rahisi ni kwamba ikiwa wameinuka watu wakakunenea kila siku kuwa utakufa nawe ukasikia, nawe kama hautachukua hatua yoyote juu ya matamko yao hakika utakufa.
Ikitokea unaumwa na wakatokea watu wakakunenea kuwa hutapona, nawe kama hautachukua hatua yoyote juu ya hayo matamko yaliyotolewa dhidi yako hakika hautapona.
Ikitokea umeanza huduma, na wakainuka watu na kukupinga wakisema kuwa hautafika popote, nawe ukashindwa kuchukua hatua ya imani ili kugeuza maneno yao hakika hautafika popote kihuduma.
Ndiyo maana hata BWANA YESU alitoa tamko saa ileile alipoambiwa aache kuhubiri mahala flani
“Saa ileile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahala pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. Akawaambia, Nendeni mkamwambie Yule mbweha, tazama leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika” LUKA 13:31-32.
BWANA YESU wakati anatoa tamko juu ya Herode hakuangalia cheo chake, wa kutisha kwake, bali yeye alitoa tamko ili kugeuza tamko la Herode.
Nawe mtu wa Mungu unapaswa kutoa tamko kinyume cha matamko waliyoyatoa maadui
Ikiwa wamesema utakufa wewe useme SITAKUFA
Wakisema hutapona wewe sema NITAPONA
Wakisema huwezi chochote wewe sema NINAYAWEZA MAMBO YOTE

Wakisema utakufa maskini wewe sema MIMI NI TAJIRI,
Yaani huu siyo wakati wa kunyamaza kimya,
Siyo wakati wa kuendelea kukaa kimya ukisubiri babaya yatokee ndiyo uchukue hatua.
Bali ndiyo wakati wako wa kugeuza maneno yao,
Ni wakati wa kugeuza meza zao, kugeuza mipango yao mibaya waliyoipanga juu yako.
Ni wakati wa kukiri ushindi hata kama kwa macho ya mwilini unaona kama huwezi, lakini unapaswa kukiri ushindi kwa imani.
Kwa maana imeandikwa Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake MITHALI 18:20.
Ndiyo maana Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
NAWE TOA TAMKO LEO, KINYUME CHA MATAMKO YALIYOTOLEWA NA MAADUI ZAKO.

Ni mimi ndugu yenu katika Kristo,
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu).

Comments