NI VIZURI KUTANGAZA MSIMAMO WAKO WA WOKOVU..

BWANA YESU atukuzwe.
Kila Mtu Atalipwa Sawasawa Na Kazi(Matendo) Yake. Kazi Ikiwa Nzuri Utalipwa Uzima Wa Milele, Na Kazi Yako Ikiwa Mbaya Utalipwa Jehanamu Ya Moto Milele. BWANA YESU anasema
Ufunuo 22:12 '' Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.   ''

Ndugu, Huu Ndio Wakati Wa Kuhakikisha Unakubaliwa Na MUNGU Aliye Hai. Mpokee YESU Na Anza Kuishi Maisha Ya Wokovu Huku Ukidumisha Utakatifu. BWANA YESU Yu Karibu Ndugu.
Leo nazungumzia msimamo wa wokovu ulivyo muhimu.

“Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 10:32-33).
 -Ndugu Yangu, Tangaza Msimamo Wako Ili Watu Wote Wajue Kwamba Umeokoka. 
-Wanaoficha WOKOVU Wao Ni Wale Tu Wenye Ajenda Za Siri. Yawezekana Anaficha Kusema Ameokoka Kwa Sababu Matendo Yake Ni Sawa Tu Na Ambao Hawajaokoka, Yawezekana Anaficha Wokovu Wake Kwa Sababu Anaonja Kidogo Kidogo. 
-Ndugu, Kama Kweli YESU Amekuokoa Tangaza Msimamo Wako Hadharani. 
Mithali 3:5-8 ''Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.  Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako. ''
- Tangaza Wokovu wako Kwa Matendo Na Maneno Yako.
- Tangaza Wokovu wako Kwa Uvaaji Na Kauli Zako.
-Tangaza Wokovu wako Kwa Utakatifu Na Ahadi Zako.
-Tangaza Wokovu wako Kwa Kukataa Dhambi Na Mambo Ya Aibu. 

1 Yohana 4:15 ''Kila akiriye ya kuwa YESU ni Mwana wa MUNGU, MUNGU hukaa ndani yake, naye ndani ya MUNGU.   ''
 - Usipojisimamia Huku Ukimtegemea MUNGU, shetani Lazima Atakusimamia Tu. Uwe Makini Sana Na Mtegemee BWANA YESU Daima na hakikisha unamkiri yeye popote uendako.
-Ulimpokea BWANA YESU kwa kukiri
Warumi 10:9-10 ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.  ''
 -Na inatakiwa ubaki kwenye ukiri huo milele na kwa ukiri huo ndio maana jina lako liliandikwa kwenye kitabu cha uzima mbinguni. je vipi ukimkana? maana ulipomkiri jina lako liandikwa humo kwenye kitabu cha uzima, vipi ukimkana? ni swali nakuachia.

-Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo imani pasipo matendo imekufa.
Yakobo 2:26 '' Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa ''
-Imani yako ya utii lazima iambatane na matendo, haiwezekani umkiri BWANA YESU ukiwa kanisani tu lakini ukikutana na marafiki zako kazini unasema humjui YESU, hapo unakuwa unakosea sana.
-Imani yako lazima iambatane ma matendo mema na ukiri mwema ni sehemu ya matendo mema. 
Kama unamkana YESU katika matendo yako hakikisha unaanza kumkiri leo.
Ndugu mmoja alisema kwamba, kwa sasa hafuati utakatifu kwa sababu ametengwa na kanisa. 
Naomba nitumie nafasi hii kujibu.

Hataka kama kanisa limekutenga, wewe endelea kutenda mema huku ukimiri BWANA YESU. Kumbuka kujiepusha na Wokovu wa BWANA YESU ni kuukataa uzima wa milele.

 Kutengwa Na Kanisa Kwa Sababu Ya Dhambi Mbaya Uliyoitenda Ni Jambo Sahihi Kabisa Ila Hakuwezi Kuwa Mbadala Wa Toba Bali Maana Yake Ni Kushuhudia Ulimwengu Kwamba Kanisa Halikubali Dhambi Hiyo Iendelee Kukutafuna Wewe Na Kuwatafuna Wengine. Ndugu huyo Aliniambia Kwamba "Nimeambiwa Kwamba Nikifa Kabla Miezi 6 Ya Kutengwa Haijaisha Siwezi Kwenda Mbinguni"
Ndugu Zangu,Kanisa Halina Mamlaka Ya Kumuhukumu Mkosaji, Ukihukumu Unamkosea BWANA YESU Maana "Alijeruhiwa Kwa Makosa Yetu, Alichubuliwa Kwa Maovu Yetu; Adhabu Ya Amani Yetu Ilikuwa Juu Yake, Na Kwa Kupigwa Kwake Sisi Tumepona-Isaya 53:5".  
Kanisa Lazima Likemee Dhambi Kwa Nguvu Zote, Na Wale Wanaofanya Maovu Na Kuonywa Bila Kuonyeka Hao Wakemewe Na Hata Kutengwa. Kumbuka Ndugu, Mfano Unapofanya Uzinzi Unapelekea Hata Huduma Idumae, Wewe Unakuwa Kikwazo Cha Kuongezeka. Uzinzi Wa Mtu Mmoja Unaweza Ukapelekea Hata Kanisa Lenu Kuitwa Kanisa La Wazinzi, Ni Mbaya Sana, Hata Ukitengwa Ni Sawa Kabisa. Ila Toba Sio Huko Kutengwa Bali Tubu Ndugu Na Kuacha Dhambi Hiyo.
Kisha baada ya toba ya kweli endelea kumkiri BWANA YESU maana ukijifanya hakuhusu kwa sasa basi siku ya mwisho utamhitaji bila mafaniko.

 Matendo 3:19 ''Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;  ''

ROHO MTAKATIFU ndiye msimamizi wa Wokovu wetu, ukiwa nae yeye utajikuta tu uko jasiri na haitakusumbua kumkiri YESU maana una ROHO MTAKATIFU.
- Kumpinga ROHO MTAKATIFU Ni Kumpinga MUNGU. -Kumkufuru ROHO MTAKATIFU Ni Kukataa WOKOVU Wa BWANA YESU, Ni Kukataa Kilichofanyika Calvary, Ni Kumkataa BWANA.
 1 Yohana 4:15 ''Kila akiriye ya kuwa YESU ni Mwana wa MUNGU, MUNGU hukaa ndani yake, naye ndani ya MUNGU.   ''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments