![]() |
Na Mtumishi Geofrey Mwanza, Mombasa Kenya. |
Biblia inaonyesha kuwa matendo yetu ya kila siku yanaandikwa kwenye vitabu fulani na ambavyo kuna siku ya mwisho ambayo vitabu hivyo vitakuja kufunguliwa na kila mmoja kusomewa hukumu yake kulingana na matendo yake hapa duniani.Kabla ya hukumu hii kuna usingizi ambao kila mmoja atalala
(Ufunuo 14:13"Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema'Andika heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana .....".

Huwezi pumzika kwa amani ukiwa nje ya Yesu,maana Yesu mwenyewe ndiye "AMANI".Ningewaomba watu wa MUNGU kila mmoja wetu tuzichunguze njia zetu na tumkaribie YESU atupe pumziko la uzima wa milele.Huwezi ingia mbinguni ukiwa na uchafu wa dhambi heti unaenda kanisani kila siku.
Barikiwa sana na uokoke kama bado hujaokoka na kama umeokoka ambia Mungu azidi kutupa funuo zaidi.
"THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES- Kenya Call 0724 656 653.

Comments