ONDOA SANAMU KATIKA MAENEO YAKO YOTE.

Na Peter M Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la kuponya na kufungu.
Kama Unajihusisha Na Kusujudia Sanamu Au Jiwe Harafu Unajiita Mteule Wa MUNGU Tambua Neno Hili,
 Matendo 17:29 "Basi, Kwa Kuwa Sisi Tu Wazao Wa MUNGU, Haipasi Kudhani Ya Kuwa Uungu Ni Mfano Wa Dhahabu Au Fedha Au Jiwe, Vitu Vyote Vilivyochongwa Kwa Ustadi Na Akili Za Wanadamu."
- Haipasi Kudhani Kwamba Uungu Unaambatana Na Sanamu Wala Jiwe. 
-Fanya Maamuzi Mazuri Hata Kama Waumini Wenzako Watakushangaa. 
-Amua Kumpendeza MUNGU Wa Mbinguni Na Sio Kupendezesha Sanamu Na Midoli. 
Kumb 7:5 '' Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga. ''
 -Tangu zamani MUNGU anaagiza wateule wake kutokujihusisha na
 sanamu.

-Tangu zamani MUNGU anaagiza wateule wake tuharibu sanamu za kuchongwa au kutengenezwa na wanadamu ambazo zinatumika katika ibada.

Siku ya mwisho  Kuna Watakaolipwa Mshahara Uitwao Uzima Wa Milele Kwa Sababu Wameamua Vyema Na Kuna Watakaolipwa Mshahara Uitwao Jehanamu Kwa Sababu Ya Dhambi Zao. 

Gideoni Alikuwa Mwanadamu Kama Wewe Akaambiwa Aziteketeze Sanamu Zote Hekaluni Kwao Walikokuwa Wanaabudu, Akaziteketeza
Waamuzi 6:25-32 ''  Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; ukamjengee BWANA, MUNGU wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata. Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama BWANA alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku. Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa. Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Hata walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili. Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu nayo. Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa wakishindana naye, Je! Mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea na auawe hivi asubuhi; kama yeye ni Mungu, na ajitetee nafsi yake, kwa sababu mtu mmoja ameibomoa madhabahu yake. Basi akamwita Yerubaali siku hiyo, akisema, Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake, kwa sababu ameibomoa madhabahu yake.'' 
-Mchakato wa Gidioni ni mchakato ambao anatakiwa aufanye kila mteule.
-Kuna koo wana madhabahu zao ambazo zinatakiwa kubomolewa.
-Unakuta familia ina mti na mti huo umewkewa maagano yote ya familia, hiyo ni sanamu na inatakiwa kuharibiwa.
-Kuna watu ili maombo yaende vizuri lazima waombe kuelekea sanamu ambayo iko mbele yao iwe ni nyumbani au kanisani, hayo ni makosa makubwa.
-Ndugu yangu, Ondoa Sanamu hata Moyoni Mwako.
- Ondoa Sanamu Kwenye Mwili Wako. ondoa sanamu unazovaa.
-Ondoa Sanamu Kwenye Familia Yako Na Ukoo Wako. 
-Ondoa Sanamu Kanisani Kwenu Na Jitenge Na Ibada Ya Sanamu.
1 Kor 10:14-15 '' Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. ''


Bado Kitambo Kidogo Safari Yetu Ya Duniani Itafika Mwisho. 
Sanamu hatitakuwa na maana siku hiyo. sanamu hazitakuwa na uzima siku hiyo. Sanamu hazitakuwa na msaana siku hiyo.
Bado Kitambo Kidogo Safari Ya Kila Mtu Duniani Itafika Mwisho, Hata Kama Utaishi Miaka 70 Ijayo Ukiwa Hapa Duniani Hiyo Ni Kitambo Kidogo Ukilinganisha Na Maisha Ya Milele Ijayo Ambayo Ama Utakuwa Uzima Wa Milele Ama Jehanamu Ya Moto. Hata Kama Utaishi Miaka 2 Au 20 Bado Ni Kitambo Kidogo Ukilinganisha Na Milele Ijayo. 
dhambi zinawakwamisha wengi kuingia uzimani, na moja ya dhambi hizo ndio hii ambayo leo naizungumzia yaani sanamu.
MUNGU hahitaji kuunganishwa na sanamu katka mazingira yeyote yale.
 Kutoka 23:24 ''  Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande. ''
=MUNGU hataki sanamu.
-matambiko ni sanamu.
-kupiga ramli ni sanamu
-Kuabudu wafu ni sanamu.
-kusujudia sanamu yeyote iwe sanamu ya wataklatifu wa zamani hiyo ni dhambi.
-Chochote ambacho utakitumia katika ibada ambacho ni kinyume na MUNGU hicho ni sanamu.
-Wanaoabudu mungu mwengine nje na MUNGU katika KRISTO YESU hao wanaabudu sanamu.

Ndugu Yangu, Kesho Yako Inaamuliwa Na Leo Yako. BWANA YESU Yuko Jirani Kabisa Na Moyo Wako Ili Ukiufungua Moyo Wako Unampokea Na Anakupa Uzima Wa Milele
Ufunuo 3:20 '' Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. '' 
-Kuokoka ni njia mojawapo ya kujitenga na sanamu.
-Kuokoka ni njia ya kujitenga na ibada ya sanamu au ibada ya kuabudu wafu.
Hakuna Uzima Wa Milele Nje Na YESU KRISTO
Matendo 4:12 ''Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.''
 -YESU Anaokoa, Ukimpokea Leo Unaokoka.

Kataa sanamu maana BWANA MUNGU hapendi wala hahitaji kuunganishwa na sanamu yeyote. Kuna watu husema kwamba hawaiabudu sanamu ila wanaiheshimu tu? 
Agizo hilo la kuwaagiza kuheshimu sanamu wanalitoa wapi?
MUNGU wa mbinguni ndiye mtoa maagizo na katika agizo lake hataki tujihusishe na sanamu. JEHOVAH MUNGU anasema.
Kumbu 12:3 ''nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo.''
-BWANA amesema na neno lake ni ndiyo na amina. hatutakiwi tuilazimishe Biblia itufuate sisi badala ya sisi kubaki kwenye wajibu wetu wa kuifuata Biblia. 
Ndugu, kumbuka kwamba kuna adhabu kwa waaubudu sanamu.
Ufunuo 21:7-8 '' Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa MUNGU wake, naye atakuwa mwanangu. Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. ''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments